Mwinyi: Mabasi ya mwendo kasi ni ureda (uroda)

Mwinyi: Mabasi ya mwendo kasi ni ureda (uroda)

Tusubiri rais mstaafu wa awamu ya nne naye atakapofanya ziara yake kwenye mabasi hayo. Sijui atakuja na neno gani la kiswahili cha Msoga la kuelezea usafiri huo. Halafu mzee Nkapa na neno la kiswahili cha Makonde, na mwisho mzee Ngosha na neno la kiswahili cha Getegete!
 
Hivi kwanini Mzee Mwinyi hajawahi kusafiri nje ya nchi?
Hata mie nashangaa wakati Kiingereza anakijua vizuri! "Sisi" wengine kila ukiwaza kuchapia basi huwa tunawatuma wadogo zetu waende. Ya nini kuumbuka bwana! Ila hiyo inferiority complex "inatusababishia" hasira na maamuzi ya kibabe. Hata wewe Elli "tukigundua" unaandika points na unauelewa mkubwa na kukubalika kuliko "sisi" basi utakula ban kwa sababu yeyote ile mfano kuweka herufi kubwa au alama ya kuuliza pasipo stahili.
 
Katika kamusi ya TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili) hakuna neno "Uroda" bali kuna neno "Ureda". Maana neno Ureda kama ilivyotafsiriwa ni hapiness, comfort, luxury.

Inawezekana kuwa mwandishi kakosea kuandika kama alivyosema rais mstaafu?!

Hakika Mzee Mwinyi alisema, "...basi lina ureda...(akageuka kama kuwauliza abiria) ...ninyi mnaita uroda eeh!'

Nashauri sasa Jiji au Makonda waanzishe mradi mkubwa wa maegesho ya magari maeneo ya Kimara. Hivi sasa baadhi ya watu wanaacha magari yao binafsi Kimara Mwisho kisha wanapanda Mwendokasi. Na wenye maeneo jirani na kituo wameanza biasahara ya parking ambapo hutoza 1,500/= kwa gari kwa kutwa.
 
Hiyo ndiyo maana halisi ya "uroda". Kwenye vyombo vya usafiri, kwenye bembea, roller-coaster, n.k. Sivyo kama ilivyoharibiwa na "mabitozi ". [emoji41]
Swadakta Mkuu hiyo ndio maana ninayo ifahamu mimi wakati tukiwa wadogo tukidandia gari tulikua tunasema tumepata uroda,tafsiri hii ya sasa walikuja kuiharibu watu wa gazeti la Sanifu ndio waliikuza hii maana na kuifanya ionekana maana ya neno hilo kuwa ni kufanya ngono,lakini walikua wana nia nzuri tu walikua wanaweka tafsida ya neno lenyewe (ngono)
 
Kwa wanaoishi Dar es Salaam, kwani hayo mabasi yanahudumia aslilimia ngapi ya mji mpaka yaonekana ndio suluhisho la matatizo yote ya usafiri!?
Lakini pia tukumbushane kuwa Mzee Mwinyi alipoingia madarakani aliikuta UDA tema ikiwa imara sana na hata IKARUSI walikuwa nazo na likafia mikonono mwake, jifunze kitu hapo na sio hizi kejeli kwa wanyonge.

Hapa umedanganya manake mwinyi alileta chai maharage baada ya kukuta UDA inatembelea magoti.
 
Rais mstaafu Mwinyi ni mmoja wa wanagenzi wakuu wa kiswaili Tanzania na kama unakumbuka alikuwa anahojiwa sana kipindi cha nyuma huko na BBC kuhusu lugha ya kiswaili na maana ya maneno mbalimbali ya kiswaili. Neno uroda ni neno la kiswaili ambalo hapa katikati tumelitafsiri vinginevyo lakini katika utoto wangu tumelitumia hilo neno kama raha iliyopitiliza ambayo ilikuwa inapatikana kwenye bembea, ukipanda gari au ndege kutereza n.k

Mwinyi mmoja wa wanagenzi? Nahisi kuna kitu ulitaka kuwasilisha ila kuna mahali issue haijakaa fresh
 
Watanzania! watu mnamkosoa mtu aliye na diploma ya Kiswahili ilhali nyinyi hata cheti hamna. Angalieni maana ya neno uroda kwenye kamusi. Au mnafikiri fikra zake zipo hicho Kiswahili chenu cha kihuni?
 
Huu ulioandika unaasilimia kubwa sana kuingia kwenye ukilaza.
Hujui maana ya Uroda???? au akili iko kwenye mapenzi zaidi.
Sasa Mwinyi angepanda mwendo kasi gani kwa miaka kumi iliyopita (alivyokuwa rais)wakati mwendo kasi tanzania imeanza mwaka huu.
Kusema mwendo kasi ni Uroda hajalinganisha na ndege/vogue, au uelewa umeubinafsisha mkuu.
Yeye kasema hayo mabasi kwake ni Uroda, Unataka nani athibitishe kitu ambacho muhusika amesha kifafanua.

Acha hizo, jaribu kujifikilia kabla haujaandika.


mkuu mim sijaongea kuhusu mapenzi! wew ndo akili yako imewaza hivyo! mstaafu alishindwa kusema usafiri mzuri mpka aseme uroda na kuacha walaji tunahangaika!
 
Watanzania! watu mnamkosoa mtu aliye na diploma ya Kiswahili ilhali nyinyi hata cheti hamna. Angalieni maana ya neno uroda kwenye kamusi. Au mnafikiri fikra zake zipo hicho Kiswahili chenu cha kihuni?


mkuu hata magafuli ana cheti cha PhD lakini hajui kilanza ni mtu gani
 
ni kauli iliyotolewa baada ya huyu mh ruksa kupanda basi la mwendo kasi mods hope sijapotea jukwaa
 
Back
Top Bottom