Mwinyi: Mabasi ya mwendo kasi ni ureda (uroda)

Mwinyi: Mabasi ya mwendo kasi ni ureda (uroda)

image.jpeg
Kama brt mwinyi anasema ni uroda.. Je hii bembea angeiita nini?
 
Hahahaaaa mzee Mwinyi bana.....huwa anapenda kutumia maneno yenye utata utata.

Neno uroda halina utata wowote Mkuu. Watumiaji ndio wameamua kuliwekea utata. Uroda kitendo chochote kinachokupa raha, kwa mfano kubembea, kupanda farasi, nk. Sasa Mwinyi akisema anasikia uroda kupanda basi tatizo liko wapi?
 
Kila mtu ana Uroda wake,ka Babu mzee mwinyi huo kwake ndo uroda wake basi tumwache jaman
 
neno uroda ndio mahali pake. watu wamegeuza maana ya neno hilo. usifikiri mzee mwinyi hajui mlivyohujumu maana ya neno hilo.
 
Nakumbuka pia sentesi kuhusu ukimwi " ugonjwa upo mahali pabaya"
 
Mwinyi asema mabasi ya mwendo kasi ni uroda! hivi nin maana ya neno uroda?

Mwinyi pamoja na kuwa rais wa awamu ya pili bado anaona mwendo kasi ni uroda.

nilichoshangaa zaidi ni:_

Rais msitafu kufunga safari kwenda kupanda mabasi ya mwendo kasi. Je mwinyi alikuwa hajawahi kupanda mwendo kazi pamoja na kuwa rais kwa kipindi cha miaka kumi au mwinyi hajawahi kusafiri na chombo ambacho ni comfortable zaidi ya mwendo kasi?

je ni kweli mwinyi hayo mabasi kwake ni uroda?

View attachment 355208
Shida yko ni neneo URODA..hamna jengine
 
Rais mstaafu Mwinyi ni mmoja wa wanagenzi wakuu wa kiswaili Tanzania na kama unakumbuka alikuwa anahojiwa sana kipindi cha nyuma huko na BBC kuhusu lugha ya kiswaili na maana ya maneno mbalimbali ya kiswaili. Neno uroda ni neno la kiswaili ambalo hapa katikati tumelitafsiri vinginevyo lakini katika utoto wangu tumelitumia hilo neno kama raha iliyopitiliza ambayo ilikuwa inapatikana kwenye bembea, ukipanda gari au ndege kutereza n.k
 
Dah,hebu wataalam wa kiswahili wanipe maana zaidi ya neno uroda FaizaFoxy

Katika kamusi ya TUKI (Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili) hakuna neno "Uroda" bali kuna neno "Ureda". Maana neno Ureda kama ilivyotafsiriwa ni hapiness, comfort, luxury.

Inawezekana kuwa mwandishi kakosea kuandika kama alivyosema rais mstaafu?!
 
Wazee wa ukanda wa pwani nawakubali sana kwa unguli wa kiswahili, hebu angalia mifano hii michache:

1. "ukitaka kula sharti uliwe"
2. "mabas ya udart ni uroda"
3."pale dodoma walisema hachomoki, nikajiuliza ah, kwani nilichomeka nini?"
 
Manake ugonjwa ule umewekwa sehemu ambayo kila mtu aipenda. Sukari imeingia sumu. I wish him long life Mzee Mwinyi.
tatizo nililoanza kuliona ni kuruhusu wahubiri wa dini kuanza kuhubiri kwenye mabasi haya
 
kama ni mwinyi ndo kasema basi itakua kweli maana ata timu ya taifa aliiita 'kichwa cha mwendawazimu' na matokeo tunayaona.... huyu mzee ni msemakweli kweli.
Hii ndio double standards ni sawa kuita timu ya taifa kichwa cha mwendazimu ila marufuku Kuwaita wanufunzi vilaza.
 
Mwinyi asema mabasi ya mwendo kasi ni uroda! hivi nin maana ya neno uroda?

Mwinyi pamoja na kuwa rais wa awamu ya pili bado anaona mwendo kasi ni uroda.

nilichoshangaa zaidi ni:_

Rais msitafu kufunga safari kwenda kupanda mabasi ya mwendo kasi. Je mwinyi alikuwa hajawahi kupanda mwendo kazi pamoja na kuwa rais kwa kipindi cha miaka kumi au mwinyi hajawahi kusafiri na chombo ambacho ni comfortable zaidi ya mwendo kasi?

je ni kweli mwinyi hayo mabasi kwake ni uroda?

View attachment 355208
Daaah we jamaa...hivi usipoandika chochote JF ni tatzo kwako?
 
ndo raha ya kuwa na raisi mstafu kutoka zenj, siku zote viswahili vyake uwa na utata,
Mkuu, kwani neno "uroda" lina utata ? Maana neno hilo linamaanisha raha anayopata mtu kutokana na kupanda kitu chenye mwendo kama vile bembea, farasi, baisikeli, bodaboda, gari, ndege n.k. Ila ile maana nyingine ambayo wewe unifikiria ndo siyo sahihi.
 
Back
Top Bottom