Mwinyi ashangaa ufisadi kumekithiri awamu ya nne | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwinyi ashangaa ufisadi kumekithiri awamu ya nne

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kaiya, May 16, 2010.

 1. k

  kaiya Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ASEMA WAKATI WAKE RUSHWA HAIKUWEPO

  RAIS mstaafu wa awamu ya pili, mzee Ali Hassani Mwinyi, maarufu kama Mzee Ruksa ameshangaa kukithiri kwa rushwa katika utawala wa awamu ya nne ikilinganishwa na tawala zote zilizopita.


  Mzee Ruksa alisema hayo jana jijini Dar e Salaam katika mahafali ya 12 ya Chuo cha Teknologia ya Habari (IIT) alikoalikwa kama mgeni rasmi.
  Alisema kuwa miongo miwili iliyopita, akiwa madarakani kama rais wa awamu ya pili rushwa ilikuwa haipo na ilikuwa haina nafasi.

  Mwinyi alibainisha kwamba, wakati anatangaza ruksa kwa kila kitu hapakuwa na rushwa wala mianya yake.


  "Kipindi mimi niko madarakani miongo miwili iliyopita, rushwa ilikuwa haipo na hata wakati natangaza kila kitu ruksa katika serikali yangu, kulikuwa hakuna mifuko ya rushwa serikalini wala katika sekta binafsi," alisema Mwinyi.

  Alisema anashangaa kuona rushwa inakithiri katika serikali ya awamu ya nne (ya rais Jakaya Kikwete) huku mianya yake ikizidi kuongezeka kwenye taasisi za umma na sekta binafsi.

  "Inashangaza kuona rushwa imeota mizizi katika sekta mbali mbali hapa nchini kitu ambacho kinakwamisha na kudumaza maendeleo ya nchi,"alieleza Mwinyi.

  Rais huyo mstaafu aliwataka vijana waliohitimu katika chuo hicho wakatumie ujuzi walioupata kujiajiri na siyo kusubiri kuajiriwa au kupata nafasi serikalini.

  Aliwataka pia kuwa wapambanaji wa rushwa ambayo imeota mizizi katika sekta mbalimbali nchini.

  Alipoingia madarakani miaka mitano, iliyopita Rais Kikwete aliahidi kuwa serikali yake itaongeza kasi ya mapambano dhidi ya rushwa na kwamba, atafanya hivyo kisayansi kwa kushambulia kiini chake.

  "Kwa kadri mapato ya Serikali yanavyoongezeka, ndivyo tutakavyoongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Tutaendelea pia kuongeza uwazi katika maamuzi ya Serikali. Tutaimarisha uwezo wa kifedha na kiutendaji wa taasisi zilizo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya rushwa, hasa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Jeshi la Polisi na mahakama. Lakini yote hayo ni bure iwapo wananchi hawatajitokeza kusaidia vyombo hivyo," alisema Kikwete.

  Kikwete alisema hayo Desemba 30, 2005 wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza mara baada ya kuapishwa kuwa Rais wa nne wa Tanzania na kuomba ushirikiano kutoka kwa wananchi kwenye mapambano hayo.

  "Naomba ushirikiano huo kutoka kwa wananchi," alisema Kikwete na kuongeza kuwa mbali ya hayo, alibainisha kuwa katika kupambana na rushwa ataangalia kwa ukaribu suala la mikataba.

  Alieleza kuwa serikali yake inakusudia kuangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji.
  Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa, hasa zile kubwa. Hata hivyo, katika juhudi za serikali ya awamu ya nne kupambana na rushwa, kesi mbalimbali za rushwa kubwa zinazofikia 25 zipo mahakamani.

  Aidha, mwaka huu serikali imerekebisha sheria na kuipa meno Takukuru ili kuipa nguvu zaidi ya kupambana na tatizo hilo, na kidhinisha sheria mpya ya gharama za uchaguzi inayolenga kudhibiti na matumizi ya fedha haramu katika uchaguzi.

  Katika mahafali hayo, Mwinyi alitoa shahada ya kwanza, stashahada na stashahada na digrii kwa wahitimu 150 katika masomo ya teknolojia ya habari, biashara na kompyuta.

  Mwananchi.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  May 16, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Haya ni matunda ya mbegu aliyopanda Mwinyi. Sasa sijui anashangaa nini.
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  May 16, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Rushwa ni kama ugonjwa ambao huzidi kukua jinsi tiba inavyo chelewesha na ugonjwa unapo kaa mwilini zaidi ndiyo matibabu yake yana kua ngumu zaidi. Hakika rushwa imeiacha nchi katika hali mahututi kwenye awamu ya nne lakini maambukizi haya kuanza leo. Prevention is better than cure kwa hiyo Mwinyi asi shangae.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  May 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jasusi,
  Maajabu ya Mussa haya jamani, hivi kweli Mwinyi hajui kwamba yeye ndiye chanzo cha Rushwa nchini?..
   
 5. P

  Percival JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2010
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Hata wakati wa Mwalimu Nyerere kulikua na rushwa - tofauiti ni kuwa Nyerere alikua akiiping vikali hadharani na alikuwa safi bila dosari ya tuhumu za rushwa. Nadhani wakati ambapo kulikuwa hakuna rishwa ni wakato wa ukoloni. Ukitaka kukomesha rushwa fuata wanavyo fanya Wachina - risasi tu.
   
 6. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Aaagh Mzee Mwinyi, hata enzi zako Rushwa ilikuwepo, Unakumbuka Loliondo gate? Uliza mbuga yetu weye!!
   
 7. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Rushwa katika nchi hii ilianza miaka ya 70 wakati wa utawala wa Mwalimu,
  baada ya kutangazwa azimio la arusha na serikali kuhodhi njia zote za kiuchumi
  ikiwemo biashara. Huduma zilianza kuzorota na bidhaa kuadimika jambo ambalo
  ni chimbuko la RUSHWA. Ili kuweza kujipatia mahitaji enzi hizo kama sabuni ya mbuni,
  sukari na hata unga wa sembe ticket ya treni ilikuwa lazima utoe kitu kidogo, hiyo imekua na sasa
  limekua jambo la kawaida kwa watendaji wa serikali hasa wanaotua huduma kwa uma
  kudai rushwa.
  Kwa hiyo rushwa hapa ni sawa na maisha itakuwepo mpaka mwisho wa dunia.
   
Loading...