Mwinjilisti amvaa Rais Magufuli, amuonya

SIMU YA TOCHI

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2014
Posts
1,385
Reaction score
894

Kamara Kusupa, Mwinjilisti wa makanisa ya kipentekoste hapa nchini, amesema marufuku ya mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya upinzani iliyotangazwa na Rais John Magufuli itavuruga amani ya nchi.

Kusupa ambaye ni miongoni mwa watu walioshiriki katika harakati za kuishinikiza serikali kurejesha mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, amemuandikia barua Rais Magufuli yenye kichwa cha habari; “Msimamo wako utachochea maasi”.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kusupa amesema, kauli za Rais Magufuli ikiwemo ile kusema watakaoandamana ‘watakiona’ na kusema, ‘mimi sijaribiwi’ ni kauli zinazothibitsha namna rais huyo anavyokosa unyenyekevu wa kiuongozi.

“Ukiwa binadamu huna namna ya kuepuka majaribu, asiyejaribiwa ni Mungu pekee. Ndio maana hata mwokozi wetu Yesu alijaribiwa na pia alitufundisha kwamba tunaposali tumwombe Mungu atuepushe na majaribu.

Mheshimmiwa rais haki inayokuwezesha kuzunguka Manyoni, Singida, Nzega na Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha ukifanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi waliokuchagua, ni haki hiyo moja ndiyo waliyonayo Lowasa, Mbowe na wanasiasa wengine,” amesema.

Amemtaka Rais Magufuli, asiwaoneshe watanzania kwamba haki ya mwenyekiti wa CCM taifa inaanzia pale zilipoishia haki za wanasiasa wa vyama vingine kwani kufanya hivyo ni kuchochea maasi.

“Rais Magufuli anapaswa kuhakikisha, taifa halizalisahi wakimbizi kama yalivyotokea maafa ya tarehe 27 Januari, 2001 baada ya Chama Cha CUF kuandaa maandamano na Serikali kuyasambaratisha na kuchochea vurugu zilizozalisha wakimbizi, waliokimbilia nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,” amesema Kusupa.

Chanzo: Mwanahalisi
 
Ni ujumbe mzuri. Lakini yatatokea majibi mengi ya kuudhi toka kwa wapiga filimbi wake.
Ila nimeamini mwanadamu ni msahaulifu sana.
Yaani ukijikumbusha JPMalivyo kuwa mnyenyekevu wakati kuomba kura hunge amini ndie huyu wa leo.
Lakini viapo vyake vitamhukumu.soon
 
Anashaurika??
Je, ni kweli kwamba hadi kufikia kutoa kauli hzo hakuwa na washauri??
Ok... Labda kateleza au aliyasema hayo bila ya washauri wake kujua na wakati huo halipo ktk hotuba yake..... Je , baada ya one mistake hakuna marekebisho??.. ???.....
 
Mchungaji hongera kwa kutoa hofu na unafki na kuwa muwazi... watu siku hizi wamejawa hofu na woga kiasi cha kutofanya kazi sahihi na kufanya ili kulinda vibarua vyao visiote nyasi km wenzao.... Mungu atulindie Tanzania yetu na atupe hekima.... Amen
 
KAMARA Kusupa, Mwinjilisti wa makanisa ya kipentekoste hapa nchini, amesema marurufuku ya mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya upinzani iliyotangazwa na Rais John Magufuli itavuruga amani ya nchi, anaandika Pendo Omary.

Kusupa ambaye ni miongoni mwa watu walioshiriki katika harakati za kuishinikiza serikali kurejesha mfumo wa vyama vingi mwanzoni mwa miaka ya 1990, amemuandikia barua Rais Magufuli yenye kichwa cha habari; “Msimamo wako utachochea maasi”.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Kusupa amesema, kauli za Rais Magufuli ikiwemo ile kusema watakaoandamana ‘watakiona’ na kusema, ‘mimi sijaribiwi’ ni kauli zinazothibitsha namna rais huyo anavyokosa unyenyekevu wa kiuongozi.

“Ukiwa binadamu huna namna ya kuepuka majaribu, asiyejaribiwa ni Mungu pekee. Ndio maana hata mwokozi wetu Yesu alijaribiwa na pia alitufundisha kwamba tunaposali tumwombe Mungu atuepushe na majaribu.

Mheshimmiwa rais haki inayokuwezesha kuzunguka Manyoni, Singida, Nzega na Mwanza kwenye viwanja vya Furahisha ukifanya mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi waliokuchagua, ni haki hiyo moja ndiyo waliyonayo Lowasa, Mbowe na wanasiasa wengine,” amesema.

Amemtaka Rais Magufuli, asiwaoneshe watanzania kwamba haki ya mwenyekiti wa CCM taifa inaanzia pale zilipoishia haki za wanasiasa wa vyama vingine kwani kufanya hivyo ni kuchochea maasi.

“Rais Magufuli anapaswa kuhakikisha, taifa halizalisahi wakimbizi kama yalivyotokea maafa ya tarehe 27 Januari, 2001 baada ya Chama Cha CUF kuandaa maandamano na Serikali kuyasambaratisha na kuchochea vurugu zilizozalisha wakimbizi, waliokimbilia nchi mbalimbali ikiwemo Kenya,” amesema Kusupa.

Chanzo: Mwanahalisi
Mchungaji gani asiyejua mamlaka iliyopo inatambuli mpaka kwa MUNGU?hajielewi huyo,wala kwenye uzi huu sirudi tena
 
" watanzania niombeni, hii kazi ya urais ni ngumu sana, najuta kwanin nilichukua fomu"

Sasa em jaribu kufanya maombi hapo ulipo, utamuombea kwa lipi na lipi hutaliombea ..?!

Unyenyekevu ni muhim sana, hasa wa kufuata taratibu na sheria ..!!
 
Watumishi kama hawa wanaona kweli na kuikemea hadharani ni wachache sana wengi hasa bakwata wanaweka njaaa zao mbele lakini damu ya watu ipo mikononi mwao na uzao wao
 
Back
Top Bottom