Mwingira amlaani mchungaji Loliondo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwingira amlaani mchungaji Loliondo

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by semmy samson, Mar 16, 2011.

 1. semmy samson

  semmy samson Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani huu ni wivu wa kiimani au nini wadau?...huyu Mtu kumuonea wivu Babu anamaana gani. hebu ichekini hii taarifa ilyoandikwa na
  Elizabeth Suleyman gazeti la mwnanchi....15 march 2011

  Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

  Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. “Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.

  “Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,”alisema Mwingira.

  Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. “Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.
  Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka,” alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.

  Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.
  “Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,”alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

  “Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira. Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara."

  Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.

  Pengo alisema: “Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion’ na baadae watu wakapata madhara makubwa.

  “Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,”alisema. Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Mwingira na Kakobe wana wivu wa KIJINGA. Atalaaniwa yeye, maalun mkubwa
   
 3. J

  Jasho la Damu JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 958
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Achen wivu kwa kuwa ninyi hamponyi.
   
 4. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  wamepoteza waumini wao maana wamekwenda kuponya kwa babu baada ya wao kushindwa kuwaponya. "Maslahi binafsi" wala si ujumbe wa mungu. Mbona mwingira na kakobe hulazimisha waumini wao kutoa fedha na vito vya thamani-sasa tuseme nao wanafanya baishara??? Mungu humbariki yeye ajishushaye kama babu-shs 500 tu (200 kanisa, 200 wasaidizi kushughulikia madawa; na 100 babu). Mungu bariki hudumu hii ya maajabu uliyotushushia kupitia kwa babu ili watu wote ulimwenguni wenye magonjwa sugu waponywe.
   
 5. semmy samson

  semmy samson Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ameeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeen
   
 6. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,078
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Sikuhizi hadi viongozi wa dini wasanii... ! inamaana DECI ilikufa kutokana na Laana Zake!! ??? nampongeza Pengo at last ameongea kitu maneno ya maana yanayofaa kuongelewa na mtu kama yeye! aendelee hivohivo , siasa hazimfai zinamshushia hadhi kwa kuongea pumba
   
 7. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Bac yeye ndio balaa anamilki hadi benki kavuna kutoka huduma ya mungu.
  Conflict of interest wanashindwa kuvumilia
   
 8. Mr.Professional

  Mr.Professional JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 1,602
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nadhani Babu amewatikisa kwa kuwapunguzia wateja yeye mwingila na kakobe
   
 9. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  nakubaliana na wewe mkuu! This is typical conflict of interest. Huyo jamaa aliipinga Dec sababu ana benk na waumini walianza kuikacha na kukimbilia huko. Sasa amemrudia Babu. Watu tumechoka na usanii wa makanisa yao. Watu wamepeleka ndugu zao loliondo wakapona, wamerudi tuwewaona kwa macho yetu waliokuwa na kisukari wanakunywa chai, soda nk. Kwann tusimwamini babu. Hata Tomaso aliamini baada ya kuona! Kama ni nabii awaponye ndugu zetu tutamfuata! Aache usanii wa kuchukua mtu chanika anakuja kujifanya kapona wakati mwenge yenyewe hakuna aliyepona!!?.
   
 10. NgumiJiwe

  NgumiJiwe JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 867
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  huyu Mwingira kwa mamlaka gani anajiita Mtume na Nabii?Japo i dont support 'mizizi' ya babu,but for this ill side with him.Hawa Manabii na maaskofu uchwara wamezidi sasa,duuh..bora miye sina dini
   
 11. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  sio wivu hayo yanayosemwa yana ukweli kabisa.
  watu wengi kwa sasa wamekuwa vipofu hawasikii hawaelezwi,il nakwambia madhala yake yatajulikana baadaye kama sio kazi ya Mungu.
  Kama ni Mungu basi itadumu.
   
 12. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,404
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  That who Jah blessed,no one curse,hakuna cha babu kulaaniwa wala loliondo kuanguka,hawa wachungaji wanawivu wa kijinga,na amin nawaambieni wanaweza kwenda kutafuta uchawi ili wamuondoshe huyu babu yetu,lakini hawatafanikiwa na loliondo itasimama imara,mbona waoa kwenye huduma zao sadaka wanaitilia kipaumbele,na hizo ndizo zinazo wanunulia magari na majumba ya kifahari,angalia hali zao za kimaisha kabla ya kuanzisha makanisa na hivi sasa,ni tofauti kubwa sana,wameshafanya vichwa vya watu mitaji,na huyu babu ni mtoa huduma na anafamilia,kibinadamu haiwezekani awahudumie watu bure na wakati anawasaidizi na familia inayomzunguka,tumchangie babu yetu na tuzidi kumuombea kwa Mungu!!
   
 13. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Taratibu mkuu, je anayeposnya ni Mungu au Babu??
  hapo ndio kuna kuwa na tatizo na hiyo imani, huyo babau kama angetumia Jina la Yesu katika huo uponyaji wake nadhani kusingekuwa na mtu yeyote kuwa na shaka na huduma yake.Yeye anatumia mitishamba kama mganga wa kienyeji anavyofanya bila ya maombi wala kumtaja aliyemwezesha, je huyo ni Mungu kweli??
  Alisema kila mlifanyalo basi fanayeni kwa kumtanguliza yeye,muombe kwa jina langu nami nitawafanyia.
   
 14. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,404
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Unajua tatizo ni kwamba hata huduma za hao wachungaji wengine tunazitilia mashaka,kwani siku hizi zipo dini zinazomtaja Mungu lakini zinaongozwa na mashetani,katika mengi ya haya makanisa ya siku hizi uponyaji hupatikana kwa yule ambaye atakuwa tayari kujiunga na kanisa husika,yaani hata ukipata uponyaji ,watakubembeleza ujiunge na kanisa hilo,lakini kwa babu ni Drink and Go!!!
   
 15. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Wote wanaompinga mchungaji walaaniwe wafe wao. Sitaki mtu ampinge ili yeye ndo abaki maarufu! Babu wa ukweli,mi sina imani/yan dini yake lakini kutokea ktk imani yangu namuombea babu aendeleze utabibu huo. Enzi za mitume miujiza hii ilikuwepo,si ajabu ikirudi!
   
Loading...