kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,755
sasa wewe unadhani hivi unavyoropoka na kutoa siri zote ya nini kinafanyika dhidi yake ndiko kunakusaidia au ndiyo kwanza unamfanya azidi na yeye kujijenga kimbinu? mbona na wewe sasa unakwenda kinyume na medani za kijasusi na kivita? mimi nimekuambia nini na wewe unaendelea kufanya nini? huyu mtu huwezi kumpata kupitia humu mtandaoni kwani hakuna siyejua kuwa ana id's zaidi ya 10 humu na inawezekana zote zikawa zinatumika na usije ukashangaa kuna hata posts humu unaweza ukaona kama vile zinamsema au kumpinga kumbe zote zikawa ni zake hivyo mwishowe ukajikuta unajaza maji ktk pipa huku kule chini hakujazibwa. na labda nikusaidie tu katika masomo yote ya ujasusi duniani kote somo la propaganda lipo au sehemu ya kozi na nimekuambia kuwa kwa mujibu ya mtu anayetupa taarifa zake ni kwamba jamaa ni jasusi na mafia pia na yupo vizuri na unavyozidi kumsema na kumfuatilia humu ni kama unampandisha chati na azidi kujulikana labda pengine wewe ukijua unambomoa. kama hao mods unasema wana wataalam wao imekuwaje ndani ya miezi 3 / 4 walishindwa kujua kuwa anatumia password moja kwa id's mbili tofauti? na bila member mmoja humu kumshtukia na nadhani alikuwa ni mussolin5 na baadae kadoda 11 mods wasingemjua na angeendelea tu kutusumbua akili. mwisho kusema kuwa anaharibu usalama wa nchi yetu napo unatakiwa uwe na uhakika nalo kwani mpaka sasa idara zote nyeti za usalama hazijasema kuwa huyu jamaa ni tishio ila ninachokijua tu ni kwamba huyu jamaa yupo nchini kwa kazi maalum ya kuwafuatilia wale maadui watatu wa rais kagame ambao wapo nchini na baada ya kukimbia nchini afrika ya kusini baada ya kuuwawa kwa wenzao na pia yupo nchini kuhakikisha hima ya watutsi inapata ustawi hapa tanzania kisha wanunue uraia na mashamba yetu na hatimaye wajizatiti na usisahau kuwa hata sisi watanzania tuna watu wetu kama yeye tumewapenyeza huko kwao nchini rwanda. umeshaweza kujiuliza ni kwanini kagame alinyamaza mara baada ya mtafaruku ule wa rwanda na tanzania? siwezi kuanika hapa kila kitu kimaadili ila wewe fahamu tu hivyo kuwa rwanda kupitia mtu wao huyu wanatufanyia ujasusi lakini na sisi pia tunawadukua vizuri sana. ile fagia fagia ya bandarini ulijua ilitokana na nini mkuu? naomba niishie hapa ila kumtisha kupitia mtandao tena huu wala hakutasaidia kufanikisha kumjua na badala yake tunatumia mbinu zingine za msaada wa mtu / watu wanaomjua.