mwandende
JF-Expert Member
- Feb 16, 2017
- 10,536
- 19,932
Mkuu bado unaamini ile nyumba ya Mwijaku ni 1.3 B?Naungana na wewe na kusisitiza yafuatayo. Vijana wa sasa hata waze tunatakiwa kubadilika. Kujenga majumba makubwa sio ufahari. Mwisho wake huwa hayatumiki. Nenda mbezi beach kuna mijengo inaota nyasi na kupangishwa kwa hela ndogo ili walao kuwe na watu ndani.
Kama kweli katumia 1.2bn (ingawa siamini). Angeweka fedha hizo benki angepata 120m kila mwaka. Angewaambia benki kwa miaka 3. Badala ya kumpa 360m wampe 300m tu. Angejenga nyumba nzuri sana kwa 300m. Tena kwa kununua kiwanja kizuri sana kwa 100m. Nyumba ingekamilika. 1.2bn ingebaki palepale benki na yumba angepata.
Si hivyo tu. Angejenga hoteli imzalishie. Vijana wa sasa tubadilike. Kufukia 1.2bn kwa nyumba ya kuishi ni ufahari wa muda tu.
Kwa nyumba hiyo umeme ni 300,000 kwa mwezi. Mengine je.
Ile nyumba hata 200 milioni haifiki..
Usibabaishwe na marangi pamoja na swimming pool juu ya paa.