Mwijage: Dangote ana matatizo ya mkataba, hatujampa gesi na hatuwezi kumpa mpaka mkataba wake uwe sawa

Mwijage atakua mchawi sana,si bure
Kwenye sukari kapona,kwenye mafuta yakula kapona,hilo la cement ni mara ya pili hii
kakizidiwa kanamuingiza waziri mkuu kenyewe kanabaki pembeni
Magufuli anataka mambo yaende,huo mkataba uwekwe pembeni,saini mkataba wa muda uzalishaji uendelee mzigo ujae sokoni,mnamchosha Rais wetu
 
Dangote aliingizwa kwenye choo cha kike kizembe sana ! unawezaje kupata ujasiri wa kuwekeza nchi kama Tanzania ?
Dangote aliwekeza wakati akitumia projections za investment policies za Kikwete's regim lakini mmzee wa kufukua makaburi ndio ameharibu...kimsingi kila lawama ya sekta yoyote ile nchini kwasasa juu ya jiwe...mpoiooooooo
 
Inaonekana Dangote alifanya mkataba kwa kauli ya mdomo wa serikali iliopita nothing written,kuna wakati watu walisema alihakikishiwa na watu wa Lumumba.
Kwa lugha za kijiweni watu walimwingiza mjini na ndivyo ilivyo mikataba mingi ya huko nyuma kupiga tu.
 
Kama taifa kamwe hatuwezi kuendeleza kwa kuanzisha migogoro na wawekezaji. Ni nani alieingia mkataba na Dangote? Wawekezaji wengine wakiyaona hata wataogopa kuja kuwekeza Tanzania.
Dangote ni mtihani mkubwa sana katika uwekezaji na siasa Tanzania, kwa sababu.

1. Dangote ni tajiri wa kwanza Afrika na tajiri mkubwa sana duniani, watu wanamuangalia na kumsikiliza sana.

2. Dangote ni tajiri wa Kiafrika anayejua kufanya biashara Afrika, akisema vibaya kuhusu Tanzania, wawekezaji wengine wataona mpaka huyu mjanja wa Afrika kashindwa hapa, hili ni fupa lililomshinda fisi, sisi tunaweza "kupigwa kama mbwa koko", hatusogei hapa.

3. Dangote anaonesha jinsi gani serikali ya Tanzania isivyo na muelekeo. Aliahidiwa vitu vingi sana na Kikwete ambavyo vimerudishwa katika majadiliano upya na Magufuli. Wawekezaji wanaona kumbe serikali ya Tanzania inabadilisha makubaliano kama upepo kulingana na mtu aliyepo ofisini, si kutokana na mikataba ya maandishi au makubaliano ya kiungwana kati ya serikali na wawekezaji.

4.Serikali haiwezi kumshinda Dangote kwenye PR war hususan kwa sababu Magufuli tayari ana jina baya kimataifa kuhusu biashara, episode ya Dangote itafanya watu kama "The Economist" waweze kuandika article nyingine ya kuikejeli serikali ya Tanzania na kusema "tulishawahi kusema haya yatatokea, na yanatokea kweli".

5.Dangote alikuwa kashajipanga na kashaanza kupunguza sana ughali wa saruji, hapa impact ipo kwa watu wanaoona saruji inapanda bei, hawa ndio wapiga kura ambao serikali iliwaahidi kutatua matatizo yao na kuwapunguzia ugumu wa maisha.

Suala kama hili linahitaji weledi mkubwa na kufanya maamuzi kwa akili kubwa, si mihemuko ya serikali ya sasa ya kusema "my way or the highway".
 
mkwer.e alipiga chake kwa igwe ngote na huyu anataka kufosinayeye amegewe akannue wa kuunga mkono
nyambaf
 
Unategemea nini kwa mtu anaetafsiri cherehani nne kuwa kiwanda?

Huyu muwekezaji alipogoma mara ya kwanza hadi akaenda ikulu yakamiminwa malori mkataba haukua na matatizo?
 
"Kila mwenye akili timamu na ampinge,msizani mko salama. Akimalizana na wapinzani atakuja kwenu' Mod naomba kale ka wimbo ka hatunywi sumu hatujinyongi. Nimtumie Dangote.
 
I believe kama wangeamua kukaa meza moja kuangalia win win situation kwa pande zote wangepata suluhisho kwa pande zote zenye mkataba! Mkataba sio msahafu kusema usifanyiwe mapitio na kurekebishwa! Economic diplomacy is vital that bureaucratic aproach
In reality, particularly between governments and multinational companies, it is hardly to reach a point where the "win-win situation" will be realized; as long as there are different interests between the parties. Close to say never and ever! Is a matter of forgoing some and get more or less than some. That's where this government needs to understand in order to better regulate the economy. And in most cases, government is the one expected to get less than the "some".

Why this is the likely situation? Because government is the one enjoys spill-over effects from investments, but also has direct and indirect ways of raising revenues through that investment.

You can do all these policy inconsistencies only if you have an absolute advantage over investment attractions, a thing which doesn't exist in our country.
 
Dangote ni mtihani mkubwa sana katika uwekezaji na siasa Tanzania, kwa sababu.

1. Dangote ni tajiri wa kwanza Afrika na tajiri mkubwa sana duniani, watu wanamuangalia na kumsikiliza sana.

2. Dangote ni tajiri wa Kiafrika anayejua kufanya biashara Afrika, akisema vibaya kuhusu Tanzania, wawekezaji wengine wataona mpaka huyu mjanja wa Afrika kashindwa hapa, hili ni fupa lililomshinda fisi, sisi tunaweza "kupigwa kama mbwa koko", hatusogei hapa.

3. Dangote anaonesha jinsi gani serikali ya Tanzania isivyo na muelekeo. Aliahidiwa vitu vingi sana na Kikwete ambavyo vimerudishwa katika majadiliano upya na Magufuli. Wawekezaji wanaona kumbe serikali ya Tanzania inabadilisha makubaliano kama upepo kulingana na mtu aliyepo ofisini, si kutokana na mikataba ya maandishi au makubaliano ya kiungwana kati ya serikali na wawekezaji.

4.Serikali haiwezi kumshinda Dangote kwenye PR war hususan kwa sababu Magufuli tayari ana jina baya kimataifa kuhusu biashara, episode ya Dangote itafanya watu kama "The Economist" waweze kuandika article nyingine ya kuikejeli serikali ya Tanzania na kusema "tulishawahi kusema haya yatatokea, na yanatokea kweli".

5.Dangote alikuwa kashajipanga na kashaanza kupunguza sana ughali wa saruji, hapa impact ipo kwa watu wanaoona saruji inapanda bei, hawa ndio wapiga kura ambao serikali iliwaahidi kutatua matatizo yao na kuwapunguzia ugumu wa maisha.

Suala kama hili linahitaji weledi mkubwa na kufanya maamuzi kwa akili kubwa, si mihemuko ya serikali ya sasa ya kusema "my way or the highway".

Weledi na umakini havipatikani kirahisi Kiranga.

Pia usisahau utendaji kazi safari hii unapimwa kwa mwendo wa matamko na kuongea, cheza vizuri na media tu, kwisha kazi.
 
MWIJAGE+PIC.jpg

WAFANYABIASHARA wa vifaa vya ujenzi mkoani Dar es Salaam wameeleza kuwa kuna uhaba wa saruji baada ya viwanda vya Twiga na Nyati kusitisha kwa muda uzalishaji kutokana na ukarabati.

Kutokana na usitishwaji huo wa uzalishaji, kumefanya bei ya saruji kupaa kutokana Sh 13,000 hadi Sh 16,000.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema kupanda kwa bei ya saruji kumesababishwa na kusimama kwa uzalishaji katika viwanda vya saruji vya Twiga na Nyati.

Akizungumza na gazeti hili jana, Waziri Mwijage alisema sababu nyingine ni kusuasua kwa uzalishaji katika Kiwanda cha Saruji cha Mtwara cha Dangote ambacho kina matatizo ya mkataba wa kisheria.

“Twiga leo (jana), wameanza uzalishaji kidogo kidogo, Nyati nao wanapambana ili waanze kuzalisha, hawakuangalia soko la walaji wakaingia kwenye ‘Industrial Maintenance’ hivyo kufanya saruji kuadimika.

“Dangote ana matatizo ya mkataba hatujampa gesi na hatuwezi kumpa mpaka mkataba wake uwe sawa, nina imani hivi karibuni saruji itapatikana sokoni kama kawaida,” amesema Mwijage.

Mmoja wa wauzaji katika duka la CWC Hardware lililopo Kariakoo, maarufu kwa jina la Machupa amesema, “Ni wiki mbili sasa hakuna saruji, utatembea Kariakoo nzima hamna, hii ya Twiga ipo kidogo, saruji imeadimika kabisa sijui wana matatizo gani huko kiwandani.”

Chanzo: Habari leo
kuna kipindi watu walihoji tukawaambia hakuna tatizo ni mitambo tu ndo anafunga huyu dangote, kumbe twiga na walikuwawamefunga???ni viwanda vipi mnavyosema 3000+ kumbe vya kale vinatushinda, tuache usanii aisee.
wacha tusonge kuunga juhudi za mkuuu, haya mengine hayatuhusu saana japo kujenga ni siye.
 
Back
Top Bottom