MWIGULU tena SUMBAWANGA Mjini

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Kipenga kimelia jimbo la Sumbawanga Mjini. Ni baada ya Mahakama ya Rufani Tanzania kutupilia mbali rufaa ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kwa tiketi ya CCM,Hilary Aeshi. Kwa mujibu wa Sheria za Uchaguzi,ndani ya siku 90,uchaguzi mdogo utafanyika. Mahakama ya Rufani ndiyo Mahakama ya mwisho.Jana,jimbo la Sumbawanga Mjini limekuwa wazi rasmi.

Baada tu ya uamuzi huo wa Mahakama ya Rufani, wazito wa CCM waliitana Ofisi Ndogo za CCM-Dar es Salaam kwa kikao cha dharura. Kikao kilianza saa 2.00 usiku na kuisha saa 6.30 usiku. Kilikuwa na vigogo wa juu wa CCM wakiwemo baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM. Ajenda ilikuwa ni Uchaguzi wa Sumbawanga Mjini.

Katika kikao hicho ambacho nami shushushu huru nilikuwemo,timu ya Kampeni ilipangwa kabisa. Itaoongozwa na Mwigulu Lameck Nchemba,Mbunge wa Iramba Mashariki-CCM. Mwigulu atasaidiwa na timu inayoundwa na vijana wengi wa Sumbawanga Mjini waliobatizwa jina la 'Watoto wa Nyumbani'. Watia nguvu watakuwa akina Wassira,Firikunjombe na Lusinde. Fomu zitaanza kutolewa mwezi huu mwishoni.

Hatahivyo, UVCCM wametakiwa kukaa mbali na uchaguzi huo kwakuwa kwasasa hawana picha nzuri kwa jamii kutokana na kile kinachoendelea katika chaguzi zao. Ningweza kuandika mengi.Lakini nina 'hang-over' ya mkutano wa Lumumba.Kumekucha!
 
CCM wangekuwa wanafunzi wangepata zero. Mwigulu ni disaster, kaleta balaa Igunga akaleta kushindwa Arumeru Mashariki, leo wanataka wampeleke tena na S'wanga mjini!!
 
Mh!wakajipange upya naona kikosi chao hakijakaa vizuri.Huyu Lusinde itakuwa uchocho wa chadema kwa sababu beki huyu huwa ni mvivu kukaba!!
 
Unadhani watampeleka nani zaidi ya huyo mharibifu?Wanajiandalia anguko lao.
 
Kama kuna siku ccm wamelamba garasha, ni kumtanguliza Mwigulu kwenye mapambano. Lusinde, je Sumbawanga ni mashabiki wa matusi?Wassira, je Sumbawanga wanajali vitisho?CCM, sikio la kufa.
 
Kwasababu atakuwepo Lusinde, nyumbani kwangu ni marufuku kwa watoto walio chini ya miaka 18 kusikiliza Redio au kuangalia TV yanayojiri Sumbawanga
 
chadema mtumeni vicent nyerere huko sumbawanga, maana hicho kikosi chao nyinyiemu vicent nyerere anakimudu vizuri sana na wanamuogopa vibaya sana, mtumeni mwita mwikabe kapige baseline study na kupanga mashambulizi wapi yataanzia wapi yataishia na gharama stahiki watu tuko tayari kuchangia tu.... nyinyiemu kwisha kabisa hawana timu nyingine kabisa ... MUNGU ASANTE.
 
Jamani mbona rahaaa, mambo yameshaiva sumbawanga, wakazi wa sumbawanga mjiandae kupewa kanga, fedha, tshirt, na hata pombe za bure. Vilevile mjiandae kupata maigizo ya bure toka kwa lusinde, mwigulu na wengineo! Matusi bila kukosa! Bado igunga tunasubiri.....
 
political strategy ya ccm kwasasa ni kutumia kampenzi za majitaka na kudhuru wanaowapinga hivyobasi timu nzuri kwa kutimiza hilo ni kuwatumia kina mwigulu, lusinde, wasira et al
 
Cdm jimbo letu hilo huyo mzizi tuna jua mbinu zake zote!na safari hii lazima avae kufuli kichwani!
 
CCM wangekuwa wanafunzi wangepata zero. Mwigulu ni disaster, kaleta balaa Igunga akaleta kushindwa Arumeru Mashariki, leo wanataka wampeleke tena na S'wanga mjini!!
kwa mawazo yako wampeleke nani?kila mtu kachafuka kwa kashifa za rushwa hakuna mwenye afadhali mkuu
 
Spendi kurudia walichochangia wadau wengi humu, nilicho kipenda hapa ni hiki; Hivi magamba wanajua kuwa sasa hivi hawapendwi sio tu na wananchi bali hata ndani yao pia kuna wazalendo wanaopenda nchi yao kuliko chama chao? kwani huu uzi umefikaje hapa, someni alama za nyakati, ni kweli ccm imekufa!
 
Back
Top Bottom