Mwigulu: Polisi kamateni wanaokejeli

Mwigulu: Polisi kamateni wanaokejeli

Huko kunako kwendwa kwa nchi yetu yani kuna haja kusoma na kuifahamu sheria sana yan sana.Ili kujipatia pesa kwa mambo kama haya.Akija kichwa na nguvu zake na huna kosa basi unapiga bingo yap!
 
waanze na yeye.

swissme
Ha ha ha haaa,ameenda kujua changamoto zinazowakabili,mimi tu mwananchi wa kawaida nazijua changamoto za polisi na magereza tangu nasoma primary na hata sikuwauliza nazijua kwa kuwatazama tu,au kupita kwenye makazi yao wanayoishi.Hii ni kuwakejeli kwakweli
 
Waanze na yeye aliyesema atatoa ushaidi duniani mpaka mbinguni
 
aliyasema hayo maneno akiwa bungeni ! naona picha kama alikuwa bungeni vile
 
Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamikia makazi ya polisi kuwa hayaridhishi,mara kadhaa mawaziri wa mambo ya ndani wamekuwa wakikiri kuwa polisi wanaish kwenye mazingira magumu .................mi niliskia kwao ingawa nimeshaona hiyo hali miaka kwa miaka
Hiyo ni kejeli. Kwanini usinyamaze uwaache na u****a wao??. Mil 7 sio mchezo.
 
Mara kadhaa wabunge wamekuwa wakilalamikia makazi ya polisi kuwa hayaridhishi,mara kadhaa mawaziri wa mambo ya ndani wamekuwa wakikiri kuwa polisi wanaish kwenye mazingira magumu .................mi niliskia kwao ingawa nimeshaona hiyo hali miaka kwa miaka

Maisha magumu kwao? Kivipi,vwakati ukisema wamakufungulia mashtaka??. Waache na u##%&$ wao sisi tufanye yetu.
 
Hivi yale maagizo ya siku saba, wiki mbili, ziara za kushtukiza mara tu baada ya kuteuliwa kwa mawaziri wetu kuliishia wapi? Kuna aliyefuatilia maagizo hayo na kumalizika kwa muda wake, yapo yaliyotekelezwa? Ikiwa itakuwa utendaji wetu ni kukamata watu kila siku, basi hii siyoTanzania kama nchi, bali Shule ya Sekondari Tanzania. Tufanye kazi za msingi, itakuwa ni Tanzania pekee duniani ambayo raia hawana haki ya kukosoa watendaji wake, na ni katika kukubali kukosolewa, watawala hupata mrejesho na kurekebisha mambo.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokejeli vyombo vya ulinzi na usalama nchini.


Nchemba aliyasema hayo jana wakati akizungumza na askari polisi, askari magereza na askari wa idara ya uhamiaji mkoani hapa ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.


“Watu wanaoongoza kwa uzalendo ni walioko katika vyombo vya usalama kwa sababu vinamlinda mtu aliyelala na mali zake.


“Lakini pia, ikitokea askari kavamiwa na majambazi kauawa au wameuawa, eti unakuta mtu anakejeli na kusema wangekufa ishirini ndio ingekuwa bomba.


“Kejeli kama hizo si za kuvumilika na mtu atakayefanya hivyo katika mitandao ya kijamii au mahali popote, anatakiwa kukamatwa na kuchukuliwa kama sehemu ya wahalifu wanaofanya makosa na si kwa mujibu wa sheria za mitandao.


“Anayeshangilia alichofanya adui na yeye ni sehemu ya adui, wakamatwe wafundishwe, lazima askari wapate heshima inayostahili,” alisema Nchemba.


Pamoja na hayo, waziri huyo alivitaka vyombo vya usalama vinapopambana na wahalifu, viwe vinatumia nguvu ili viweze kufanikiwa.


“Mnapopambana na wahalifu tumieni nguvu na nawaambia siungi mkono askari anayejihusisha na matukio ya uhalifu.


“Nawaomba pia mfanye kazi kwa kutenda haki ili wananchi wasiendelee kulalamikia vyombo vya dola kwamba vinaupendeleo na vinawaonea baadhi ya watu,” alionya.


Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Dk. Kato Rugainunura, alisema Gereza la Mahabusu Morogoro na magereza ya wilaya za Ulanga na Kilosa, yanakabiliwa na msongamano wa mahabusu.


Naye Ofisa wa Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Morogoro, Safina Muhindi, alisema idara hiyo inakabiliwa na tatizo la uwepo wa wafungwa wa nje ya nchi wanaomaliza muda wa vifungo vyao nchini kwa kuwa hawana bajeti ya kuwasafirisha kurudi kwao.
chanzo:mtanzania
 
1475166310809.jpg
 
Back
Top Bottom