Mwigulu: Polisi kamateni wanaokejeli

Mwigulu: Polisi kamateni wanaokejeli

Mr Hero

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2015
Posts
5,540
Reaction score
7,464
MWIGULU: POLISI WAKAMATENI WANAOWAKEJELI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokejeli vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akizungumza na askari polisi, askari magereza na askari wa idara ya uhamiaji mkoani hapa ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.

“Watu wanaoongoza kwa uzalendo ni walioko katika vyombo vya usalama kwa sababu vinamlinda mtu aliyelala na mali zake.

“Lakini pia, ikitokea askari kavamiwa na majambazi kauawa au wameuawa, eti unakuta mtu anakejeli na kusema wangekufa ishirini ndio ingekuwa bomba.

“Kejeli kama hizo si za kuvumilika na mtu atakayefanya hivyo katika mitandao ya kijamii au mahali popote, anatakiwa kukamatwa na kuchukuliwa kama sehemu ya wahalifu wanaofanya makosa na si kwa mujibu wa sheria za mitandao.

“Anayeshangilia alichofanya adui na yeye ni sehemu ya adui, wakamatwe wafundishwe, lazima askari wapate heshima inayostahili,” alisema Nchemba.

Pamoja na hayo, waziri huyo alivitaka vyombo vya usalama vinapopambana na wahalifu, viwe vinatumia nguvu ili viweze kufanikiwa.

“Mnapopambana na wahalifu tumieni nguvu na nawaambia siungi mkono askari anayejihusisha na matukio ya uhalifu.

“Nawaomba pia mfanye kazi kwa kutenda haki ili wananchi wasiendelee kulalamikia vyombo vya dola kwamba vinaupendeleo na vinawaonea baadhi ya watu,” alionya.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Morogoro, Dk. Kato Rugainunura, alisema Gereza la Mahabusu Morogoro na magereza ya wilaya za Ulanga na Kilosa, yanakabiliwa na msongamano wa mahabusu.

Naye Ofisa wa Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Morogoro, Safina Muhindi, alisema idara hiyo inakabiliwa na tatizo la uwepo wa wafungwa wa nje ya nchi wanaomaliza muda wa vifungo vyao nchini kwa kuwa hawana bajeti ya kuwasafirisha kurudi kwao.

Chanzo: Mtanzania
 
MWIGULU: POLISI WAKAMATENI WANAOWAKEJELI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokejeli vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akizungumza na askari polisi, askari magereza na askari wa idara ya uhamiaji mkoani hapa ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.
Mwigulu: Polisi wakamateni wanaowakejeli

Nawashauri waanze na raia wanovaa sare za askari wetu wapendwa.
 
MWIGULU: POLISI WAKAMATENI WANAOWAKEJELI

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, ameliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata watu wanaokejeli vyombo vya ulinzi na usalama nchini.

Nchemba aliyasema hayo jana wakati akizungumza na askari polisi, askari magereza na askari wa idara ya uhamiaji mkoani hapa ili kujua changamoto wanazokabiliana nazo.
Mwigulu: Polisi wakamateni wanaowakejeli

Hivi chemba na nape Ni ndugu? Hawatumiagi vichwa vyao vizuri
 
Kejeli nayo imekuwa kosa la kuweza kumfanya mtu akamatwe?

Hawa watu bana!
Nyani, let us be professional, let us define Kukejeli first so that we have a common base for presenting our arguments. Kama hatujakubaliana definition ya "kejeli" hatuwezi kuwa na jawabu linalokubalika kwa wote ie is kukejeli a crime according to our book of laws! Is it provided for in the penal code!
 
Nyani, let us be professional, let us define Kukejeli first so that we have a common base for presenting our arguments. Kama hatujakubaliana definition ya "kejeli" hatuwezi kuwa na jawabu linalokubalika kwa wote ie is kukejeli a crime according to our book of laws! Is it provided in the penal code!

But is it a crime, though?

If it is, what category does it fall under?

Infraction? Misdemeanor? Felony?
 
Putin--129319.jpg

Vladimir-Putin-Carrying-Viktor-Yanukovych--123578.jpg

Vladimir-Putin-Drops-HIs-Pants-For-Obama--112336.jpg

Jaribu ufanye kwetu uone cha moto.
 
Kukera, Kuudhi, Kukasirisha au hata Kukosoa in their book haya yote ni makosa, inabidi kufanya mapitio ya sheria zetu kidogo ili ziweze kuendana fikra za viongozi wetu vinginevyo watakuwa wanapoteza muda kufungua kesi mahakamani
 
Back
Top Bottom