Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

Mwigulu Nchemba wadanganye wasiokujua

"Dyu-silu", Du! Umenikumbusha mbali sana, niliwatega sana hao ndege kule kwetu. Wana kawaida ya kutengeneza viota kwa kuchimba chini, wanaweka vinyasi na kutaga mayai.

ndo jina tulilokuwa tunamtania wafuasi wake kipindi cha kampeni Iramba
 
vema kwa kuweka kumbukumbu sawa, kama anabisha na aweke vyeti vyake halisi hapa, si vya kuchonga;
Hata hivyo uongo wa nini? upper second mbona ni pass nzuri tu! anatakiwa ku-deliver tu na si kujisifia kwa vyeti ambavyo kumbe ni uongo....
 
Hebu nawe tuletee CV za wazazi wako tuzitafakari na kujua nini kilitokea kabla ya kukuzaa, maana unakera kwa kuleta hoja isiyokuwa mezani kila mara

Hivi wazazi wake ni wanasiasa wanaotaka kuongoza nchi usiwe mjinga kiasi hicho
 
Unajua alieweka hii thread alipo au unakurupuka tu?Leroy asante kwa kutuhabarisha kaka.Mwambieni Mwigulu aache kelele uongo hauishi muda mrefu kabla hujaumbuka
Hapo unaposema alikuwa tawi la Arusha umedanganya sana.......intelijensia ya Chadema imefeli hata habari za ufaulu huna data kwani umshndwa kutuambia point alizopata, punguza kuishi na hasira moyoni utakufa na kihoro.......Mnyika alikiri kudisko mwaka wa 2........au unabisha?
 
Mkiliman Mkuu soma andiko lake anasema hata degree ya pili hana 1st class..any body can say that, mimi sina information znazohusu elimu ya mwigulu, ninachotaka ni anishawishi ndio maana nikademand vielelezo kuhusu degree ya pili.

Wanasema mwigulu kadanganya, kama kweli kadanganya alete cv ambayo mwigulu kaiweka on public domain tuone alipodanganya. Cv ni document iletwe.
 
Last edited by a moderator:
Hapo unaposema alikuwa tawi la Arusha umedanganya sana.......intelijensia ya Chadema imefeli hata habari za ufaulu huna data kwani umshndwa kutuambia point alizopata, punguza kuishi na hasira moyoni utakufa na kihoro.......Mnyika alikiri kudisko mwaka wa 2........au unabisha?

Kama hakuwahi Kuwa Arusha si useme alikua wapi? unagongwa nn? sisi wengine hatupendi kuchangia sababu ya watu kama wewe, mbavu zako!
 
Tatizo ni kuwa viongozi wengi serikalini wamedanganya elimu zao. Na vilevile hakuna sheria inayowabana wala kuchukuliwa adhabu pindi wanapobainika. Na hill limrchangia sana.kwenye utekelezaji mbovu serikalini. Vilevile hawana uchungu na elimu.
 
Chuki zisipumbaze akili yako. Hoja hapa ni Mh. Mwigulu na ikiwa ni baada ya yeye kujitapa elimu yake, wapi ulimskia Mh. Lema na Mh. Mbowe wakifanya hvyo. Jikite kwenye hoja mkuu, na utailinda heshma yako.
ona maajabu hayo, halafu eti huyo mageti sita ni mbunge anayewakilisha wananchi kupitia chama cha upinzani.
 
Umenipa jibu la swali nililokuwaga najiuliza, ilikuwaje "toto jinga aliyefeli STD VII akatumia jina la msukuma mmoja akaenda kupata Degree 1st class! Pia msomi gani mwenye akili akawa anapanga mbinu chafu na mauaji kwa wapinzani wa chama chake? Ubarikiwe kwa kunipa jibu.
 
maelezo kuhusu degree ya pili kuwa hakuPata 1st class hayajajitosheleza, rudi katafute evidence uje upya. Pia ilete CV iliyopo kwenye tofuti ya bunge uweke hapa tuone wapi unaposema kadanganya.. Ulete pia CV ya mbowe na lema

Secretary upo makini sana kumtetea boss wako
 
jamani mwigulu ni kopo tu kiuchumi,nchi ya viongozi legelege huzaa serikali legelege ya akina mwigulu.hata kama ni kweli kitendo cha kujitapa kinaonesha udhaifu mkubwa kwa kiongozi.
 
CCM YAZIDIWA MADENI

Mbali na madeni makubwa, chama hicho kikongwe kimeshindwa kuwasilisha makato ya wafanyakazi wake; madeni kutoka taasisi za fedha yamelundikana hadi kufikia zaidi ya Sh. 1.3 Bilioni huku nikielezwa kuwa Akaunti zake zimefilisika. Mabilioni haya ya fedha yametafanwa na wakubwa wakiongozwa na Mwigulu Nchemba.

Soma kiambatanisho hiki hapa chini kilichotoka kwa Mwigulu Nchemba kwenda kwa Zakia Meghi. Ni wakati Nchemba alipokuwa akikabidhi madaraka ya Katibu wa Uchumi na Fedha kwa Zakia Meghji. MAKABIDHIANO YA IDARA YA UCHUMI NA FEDHA
KATI YA MHE. MWIGULU L. NCHEMBA (MB)(MNEC)
NA MHE. ZAKIA H. MEGHJI (MB) KATIBU
WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA
WA UCHUMI NA FEDHA
2. IDARA YA UCHUMI NA FEDHA
Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana mjini Dar es Salaam tarehe 27 – 29 Januari, 2004 pamoja na mambo mengine ilipitisha muundo mpya wa Idara ya Uchumi na Fedha. Awali Idara hii ilijulikana kama Idara ya Fedha na Mali za Chama. Badiliko hili la muundo linazingatia mambo yafuatayo:-
.
(a) Kwa mujibu wa Mwelekeo wa Sera za CCM katika miaka ya 2010 – 2020 na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 Chama kinatakiwa kusimamia kwa nguvu mpya Sera zake za Uchumi hususan modenaizesheni ya Uchumi na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
(b) Aidha suala la Vitega Uchumi na Uwekezaji katika Chama linatakiwa kupewa umuhimu na msukumo mkubwa ili kukiimarisha Chama kimapato na hatimaye kiweze kujitegemea. HESABU ZA CHAMA NA KAMATI YA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA (a) HESABU ZA CHAMA
Hesabu za Chama zimekaguliwa na wakaguzi wa nje TAC-Associates kwa mwaka wa Fedha 2009/2010 na 2010/2011. Hesabu hizo zimeshawasilishwa kwa Mwenyekiti kwa ajili ya kuwekwa saini na baadaye kuwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali. Zoezi la kuziwasilisha kwenye vikao vya Chama litafuata baadaye. Kwa mujibu wa hesabu hizo, Chama kina mali zenye thamani ya Shs. 49.2bn/= hadi tarehe 30.06.2011. Thamani ya mali inashuka kila mwaka kutokana na Chama kutofanya uthamini wa mali zake. Mara ya mwisho uthamini ulifanyika mwaka 1992. Kwa hiyo Wakaguzi wameshauri kuwa Chama kifanye upya zoezi la uthamini. Kutokana na ukubwa na upana wa kazi hii, zoezi hili linahitaji wataalam wengi, kwa sababu hiyo Chama huwa kinawatumia Chuo cha Ardhi kwa kuwa wao wanawatumia wanafunzi wao katika kuifanya kazi hii na hivyo kuharakisha zoezi hilo.
(b) KAMATI YA KUHAKIKI MALI ZA CHAMA
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa iliyokutana Aprili, 2007 mjini Dar es Salaam iliunda Kamati ya Wataalam kwa ajili ya uhakiki mali za Chama. Majina ya Wataalam hao ni:-
(1) Ndg. Peter Machunde – Fedha na Vitega Uchumi
(2) Ndg. George Fumbuka – Fedha na Vitega Uchumi
(3) Ndg. Sam Mapande – Mwanasheria
(4) Ndg. Kanyoni Salum Kanyoni – Mhandisi
(5) Ndg. Jacquiline Noni – Mfanyabiashara
(6) Ndg. Simon Mapolu – Mchumi
(7) Ndg. Janeth Mbene – Mchumi
(8) Ndg. Ussi Faki – Mkaguzi
Katibu wa Kamati hiyo alikuwa Ndugu L.L. Burugi – Meneja Miliki wa Chama.
Kamati ilianza kazi tarehe 19/6/2007 na kukamilisha tarehe 28/10/2007. Kazi ya Kamati hii ililenga mali za Kudumu za Chama zilizopo Makao Makuu, Mikoani na katika Wilaya zilizopo kwenye Makao Makuu ya Mikoa. Aidha, zoezi hili lilihusisha pia mali za Jumuiya za Chama katika maeneo hayo pamoja na kufanya tathmini ya mwenendo wa Makampuni ya Chama. 12. BAADHI YA MADENI AMBAYO CHAMA KINADAIWA
(1) MADENI YA BENKI NA TAASISI ZA FEDHA
NBC Ltd. – 143,763,404.00
NSSF – 831,822,961.50
Ukaguzi wa Hesabu – 72,240,000.00
1,107,826,365.50
Deni la NBC ni la tangu mwaka 1994 kupitia Kampuni ya Chama TANTI kwa kuweka rehani nyumba 10 za CCM zilizoko Area ‘C’ – Dodoma. Mkopo wa NSSF unahusu Jengo la CCM Shinyanga. NSSF walimalizia kujenga Jengo. Mazungumzo yalifanyika kati ya CCM/NSSF na kufikia makubaliano ya Chama kununua Jengo hilo kwa shs. 1,109,097,282/= kiasi cha 25% kimelipwa. Deni la ukaguzi linatokana na ukaguzi wa hesabu za mwaka 2009/2010 na 2010/2011. (2) MADENI YA VYOMBO VYA HABARI 1. Clouds Entertainment Media Group 13,080,000.00
2.Radio Tumaini 424,800.00
3. ITV 3,778,360.00
4. Sahara Media Group Ltd 44,244,000.00
5. Sports Dream Co. Ltd 810,000.00
6. KIUTA 9,430,350.00
7. Colour Print 22,619,792.00
8. Business Times Ltd (Majira) 4,988,945.00
9. Habari Corporation 6,850,000.00
10. Mwananchi Communication Ltd 9,620,000.00
11. TSN 8,271,160.00
12. Guardian Ltd 11,702,160.00
13. TBC 7,687,360.00
14. Uhuru Publication Ltd 55,049,040.00
15. WAPO Radio 1,000,000.00
16. Zanzibar Leo 4,500,000.00
17. Raia Mwema 1,129,000.00
18. FTV Production 1,980,000.00
Jumla Tshs. 201,866,807.00
 
Huyu mtu hata kamaa alizipata hizo hana uwezo wa kuongozaa hata familia yake tunajua CCM ni dhaaifu huyo kwao ni kichwa
 
Katiba ya sasa inasemaje?Je Mwigulu hana sifa ya kuwa waziri au mwanasiasa?Watanzania tunapotoka sana hasa linapokuja suala la viongozi kupewa nafasi za juu,tujiulize Kawawa alikuwa na elimu ya kiwango gani wakati anaachiwa nchi na Mwalimu Nyerere?
Tunaweza kuweka maprofesa na madaktari na kada nyingine zote za elimu katika nafasi za uongozi lakini bado tusipate maendeleo kwani uongozi ni hekima na busara mengine hayo ni nyongeza tu na mbwembwe nyingi za vyeti visivyokuwa na faida kwa taifa.


Kwani uliwai kumusikia kawawa anajitangazia elimi take?? Hapa hoja ni kweli mwigulu ni mchumi WA daraja la Kwanzaa!!
 
Back
Top Bottom