Mwigulu Nchemba, umelidanganya taifa?

Mwigulu Nchemba, umelidanganya taifa?

idoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2013
Posts
3,051
Reaction score
1,423
Kwanza nikupongeze kwa hotuba nzuri uloitoa kizalendo kabisa pale Dodoma, makao makuu ya serikali na chama (kama ulivyojipambanua). Ukasema pia utakapokuwa rais serikali itakuwa tayari imehamia Dodoma, wimbo ulioimbwa miaka zaidi ya 40. Mabadiliko ni Vitendo, Wakati ni Sasa!

Tuyaache hayo, turudi kwenye wasifu wako ulokuwa unasomwa kabla ya wewe kufika kwenye ukumbi wa Mwl. Nyerere. Katika moja ya sifa zako ni utashi na kipaji ulivyokuwa navyo tangu utotoni; kati ya watoto sita kwenye familia yenu, wewe ulikuwa mdogo lakini uliweza kuongoza ndugu zako kwa ustadi kabisa (kwa mujibu wa wazazi wako). Ni kipaji cha kujivunia sana, Masha'Allah! Kiongozi wa hivyo ni hazina kubwa katika taifa.

Kisha, katika wasifu huo, ikaelezwa ulipokuwa sekondari (kidato cha tatu) ulikuwa kiongozi mkuu (tuseme kaka mkuu, au rais wa serikali ya wanafunzi). Bila shaka shule inayosemwa hapa ni Iliboru (kwa mujibu wa wasifu-kazi wako). Ulipata nafasi hiyo baada ya aliyekuwa kaka mkuu kuachia ngazi miezi miwili tu baada ya kuchaguliwa na kupelekea waalimu kukuchagua wewe kuongoza shule. Uliongoza kwa ustadi wa juu sana, ukapendwa pia na wakubwa zako hasa wa kidato cha tano na sita, na baadaye ukatunukiwa cheti cha uongozi bora. Hongera sana!

Ikaelezwa pia ulipohitimu shahada ya kwanza ya Uchumi (BA Economics) ya chuo kikuu cha Dar es Salaam uliongoza kwa kupata alama ya juu kabisa (highest GPA) na kupelekea kupata udhamini wa masomo ya shahada ya uzamili (masters) kutoka BoT. Inafaamika kwamba unapofaulu kwa kiwango cha juu kabisa pale UDSM utapatiwa udhamini wa kuendelea na masomo kutoka BoT, Chuo, au mashirika mengine (nina uzoefu na Idara ya Uchumi). Na ukimaliza 'masters' uhakika wa kazi ni 300%; eidha BoT wakuchukue, kwa kuwa wamekusomesha (hawawezi wakapoteza pesa kukudhamini, halafu umalize ukose ajira), au Wizara ya Fedha, au Chuo (kupitia idara husika) kikuajiri kuwa mkufunzi na baadaye mhadhiri kabisa.

Sasa ndugu yangu Mwigulu Nchemba, kwenye hotuba yako ukasema unajua tatizo la ajira kwa kuwa una uzoefu nalo, eti ulipomaliza 'degree' ya pili ulienda kubeba zege! kheeee, were you serious? au ndiyo kufanya mzaha na vijana wasio na ajira? Eti mkeo akawa mama lishe na wewe ukawa mbeba zege! BoT walikusomesha ya nini? Kwenye wasifu-kazi wako inaonesha mwaka 2006 ulipomaliza 'masters' ulienda BoT na kuwa Mchumi I mpaka 2010 ulipoamua kugombea ubunge. Sasa, hilo suala la kubeba zege limetoka wapi? umewadanganya watazania? Kama ndivyo, uombe radhi basi! Au ufafanue!
 
Of course nyinyi mliokulia ktk familia za kifisadi hamuwezi kumwelewa Mwigulu uzoefu aliouzungumzia,ila wale waliokulia ktk familia za kikabwela ndiyo waliomwelewa zaidi.Mwigulu was talking to ordinary Tanzanians, his world view about Tanzanian economic development resonates well with ordinary/middle class tanzanians views.
 
swali ni je, amebebe zege? na inaonekana alipomaliza 'masaters' aliajiriwa BoT moja-kwa-moja!
 
Sio ukimaliza masomo unaajiriwa papo hapo utakaa kidogo mtaani aidha kusubiri matokeo au taratibu zingine na wakati huo mfadhili hatakuwa anakupa chochote maana tayari umemaliza masomo mfano vyuo vingi humaliza mihula mwezi wa 6 matokeo hutoka mwezi 9 na graduation hufanyika mwezi wa 11 ili angalau mtu apate cheti aweze kuajiriwa hivyo tangu kumaliza mitihani mpaka graduation ni miezi 4 mpaka 5 kwa mtu mwenye familia lazima uchakarike ili mambo yaende sawa.
 
Kawaida unapolipiwa ada iwe Bodi Ya Mikopo au mashirika Ya umma haiwi ni lazima watakuajiri mara tu baada ya masomo yako. Lazima uonje msoto.

Labda kama ulikuwa kazini ukaomba ruhusa ya kwenda masomoni hapo ndio utaenda kuripoti tu.

Kwa tunaomfshamu MWIGULU ni kwamba alipo maliza masomo Ridhwani ndiye alimtoa. Alimkuta anateseka akamwahidi kumtafutia chansi ya kuonana na Baba Ridhwani JK alipomkubalia akamweka kwanza katika chama akisubiri nafasi BOT
 
Mkuu. Kumbuka mtu muongo huwa hana kumbukumbu ya kile alichodanganya hata kama ingekuwa ndani ya dakika 10 lazima asahau alichokisema maana ni uongo. Hiyo ni sifa mojawapo ya mtu muongo.

Mwigulu ni tapeli la kisiasa. Amesahau kuwa tunajua alifeli darasa la saba na badala yake akanunua jina la mtu aliyekuwa amefaulu aitwaye Mwigulu.
 
swali ni je, amebebe zege? na inaonekana alipomaliza 'masaters' aliajiriwa BoT moja-kwa-moja!
Wewe ndo unatakiwa ueleze kama alifanya nini baada ya kumaliza 'Masters'...

Yeye kaeleza anachokiona ni ukweli sasa wewe kama unaona ni uongo ueleze ukweli ukoje....

Sina uhakika kama wewe(kama unafanya kazi) mara tu baada ya kumaliza masomo yako moja kwa moja ulianza kazi pasipo kusubiri mtaani...
 
kiukweli baada ya kumsikiliza jana huyu jamaa kwa makini,lazima niseme yuko vizuri na hii nafasi ya jana ni platform ya 2025,mimi kura yangu utaipata bila shida
 
Of course nyinyi mliokulia ktk familia za kifisadi hamuwezi kumwelewa Mwigulu uzoefu aliouzungumzia,ila wale waliokulia ktk familia za kikabwela ndiyo waliomwelewa zaidi.Mwigulu was talking to ordinary Tanzanians, his world view about Tanzanian economic development resonates well with ordinary/middle class tanzanians views.

.........Samahani, naomba tafsiri ya hayo maneno hapo kwenye red maana dictionary yangu imegoma.
 
Mkuu. Kumbuka mtu muongo huwa hana kumbukumbu ya kile alichodanganya hata kama ingekuwa ndani ya dakika 10 lazima asahau alichokisema maana ni uongo. Hiyo ni sifa mojawapo ya mtu muongo.

Mwigulu ni tapeli la kisiasa. Amesahau kuwa tunajua alifeli darasa la saba na badala yake akanunua jina la mtu aliyekuwa amefaulu aitwaye Mwigulu.

Mhhh!!!! mm sijui!
 
Mkuu mbona unatuchanganya? Hasa hasa unachotaka kueleza wana JF ni nini, hapa naona unauma na kupuliza - hivi Lameck as person una bifu nae au?
 
atakuwa amejirekodi atajicheka sana aibu yake
 
kwa umbaali kajamaa kanafaa kuliko LOWASSA na MEMBE
alibeba / hakubeba hiyo sio sifa ya urais
au wewe utampigia kura ukijua kuwa alipasua mawe na kubeba zege???
 
Back
Top Bottom