Mwigulu Nchemba ulimkosea nini Mheshimiwa Rais!?

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Habari za siku nyingi kaka!

Mara ya mwisho tulikutuna Lumumba na ukanidokeza kuhusu safari yako ya Mkoani Kigoma na 'ulinitonya' kuhusu safari yako ya Nigeria kwa TB J.


Tulipiga soga zihusuzo 'jembe' Magu hasa kuhusu anavyowafanya msilale 'Mawaziri' hiyo yote ni kwa sababu ya u busy usiokoma!Tulicheka,tulifurahi na mwisho ukaniaga na ulielekea katika ofisi ya KM.


Ajabu baada ya siku mbili mbele nikasikia tetesi kuwa mda wowote utatumbuliwa,nilihamaki!


Nilikutafuta kwenye simu yako na hukupatikana. Lakini asubuhi yake nikaelezwa kwamba ulikesha safari Kigoma na tayari ulifika asubuhi mapema.Nilikumbuka kuhusu hiyo safari kwa sababu ulinijuza.


Siku hiyo hiyo mchana nikapata habari kwamba umetumbuliwa!Hakika tetesi za janaye jioni zikawa za kweli.Nilijiuliza pasina kuelewa sababu.



Sikuelewa hali uliyokuwa nayo na hasa kwasababu hata wewe hukufahamu na ulishtukizwa na maamuzi yale ya bwana mkubwa.


Sasa leo na kwa uwazi nataka nifahamu ulifanya/ulimkosea nini bwana mkubwa!?
 
Andiko lako halina mantiki!

Kwa nini hukumtafuta tena ili muongee naye kama mlivyokuwa mnaongea kabla hajatumbuliwa?

Sasa unaleta hapa Jamiiforums ili tukusaidie nini wakati unayemuuliza huwa unaongea naye?

Kumbuka kutunga story ili ionekane niya kweli inataka mtu mwenye fikra pana na uelewa mkubwa!
 
Yaani sultan aliambiwa na wale nyoka wadogo wadogo kuwa huyu nchemba anataka kugombea urais kwa hiyo jiandae kung'oka basi jamaa mara nyingi anasubiri ukosee kidogo tu anakata jina kweli Mungu sio halima sakata la kibiti likaja jamaa akakatwaa mazima ,si unakumbuka hili la huyu makamba jr yaani alipoona ,jr atachukua umaarufu basi jamaa akamkata pembe kwa kifupi sultan hataki uwe juu yake,lakini amesahau Mzee Mkapa alimwacha yeye aongee kama mzaramo kila mahali yeye tu leo amesahau
 
Ukitaka kuwajua wale waliosherehekea kuanguka kwako; tizama comments zao. Mh Mwingulu, huyu naye ni mmoja wao. Mkumbuke alivyokuwa anachekacheka hovyo siku aliyoitaja mwenyewe. Hasidi hana dogo. Weye ulishayasahau hayo machungu, muulize; alikusikia wapi ukilalamika?
 
Kiukweli kabisa Nchemba alifitinishwa na Rais na KP ambae nae juzi kati kapigwa za uso kwa fedheha
 
Habari ya likizo ndugu?
Andiko lako halina mantiki!

Kwa nini hukumtafuta tena ili muongee naye kama mlivyokuwa mnaongea kabla hajatumbuliwa?

Sasa unaleta hapa Jamiiforums ili tukusaidie nini wakati unayemuuliza huwa unaongea naye?

Kumbuka kutunga story ili ionekane niya kweli inataka mtu mwenye fikra pana na uelewa mkubwa!
 
Back
Top Bottom