Nimeamini Watanganyika ni Vichwa maji kweli kweli. Unamtetea Mwigulu Nchemba na kumkandia Dr. Slaa? Sawa, Dr. alisema nchi haitatawalika. lakini je! Mwangosi ni Dr. alimtenda vile? Mauaji ya Mwaka juzi Arusha, ni Dr. Slaa? Waliotekwa, kuteswa, kung'olewa kucha, macho na meno, ni Dr. Slaa? Dr. alichomaanisha ni kwamba, atafanya kazi kuhakikisha watanzania wanatambua haki zao, na kuzidai. Haki zenyewe ni zipi? Meremeta, EPA, Kiwira, Symbioni, Fedha za Uswis n.k. (na alishalitolea ufafanuzi suala hilo, ila CCM mnalificha suala hilo kwa makusudi). Mauaji na vurugu zinazotokea nchini kwa sasa, hazisababishwi na Dr. Slaa, wala CHADEMA. Bali ni CCM kupitia kwa serikali yake, kupitia kwa Polisi wake. Hivi Dr. Slaa au CHADEMA wajilipue kwa bomu, inawezekana? Wawaue watanzania ili iweje? Nguvu ambayo CCM wanaitumia kuinyamazisha chadema, ni kubwa kuliko kawaida. Na hiyo ni kielelezo cha Utawala uliochoka kimfumo na kifikra na kimaono. Mwaka Juzi, serikali jeshi la polisi liliua kule arusha, likizuia maandamano ya CHADEMA. Siku ya kuaga miili ile, CHADEMA waliorganize ibada zile bila uwepo wa polisi, na hakuna kilichoharibika. Iweje watuambie kuwa mkusanyiko wa Jumamosi ungeharibu upelelezi? CCM, POLICE, SERIKALI, mnatakiwa mtuambie kinagaubaga, kuhusu sababu ya haya yanayotokea, na si kuilaumu CHADEMA. Tumesikia kwenye chaguzi ndogo za jumapili, jinsi vijana wa CCM walivyoteka watu wa chadema kule Arusha makuyuni, sengerema n.k. halafu leo mnakuja kutuambia kuwa VURUGU NA MAUAJI YA TANZANIA CHADEMA WANAHUSIKA?