Mwigulu Nchemba Kuropoka Unamuharibia Rais

Ni dhahiri Mh. Rais hakukosea kumtoa Mwigulu nchemba kwenye barraza la mawaziri. Waziri wa mambo ya nje na wengine wanapambana kutumia lugha ya diplomasia kuomba tusaidiwe, mwigulu nchemba yeye anatukana world bank bila kusahau bado yuko serikalini na kwenye chama tawala na alikuwa Waziri mwandamizi.

Ndugu yangu mwigulu, hapa umebugi stepu. Umeharibu, kama ni utetezi au kutaka kurudi kwenye baraza, haiwezekani. Pole sana kwa matusi yako kwa world Bank. Usisahau hawa watu wanafadhili miradi mingi na ndio mshirika pekee wa maendeleo alobakia. Use common sense bro. Naona huko kwenye ile kundi la wanaomhujumu Rais kijanja

View attachment 1338276
Wewe mjinga tu,kwani hili sakata limeanza leo?si limeanza ukiwa bado kwenye baraza la mawaziri?Sasa ulishindwaje kushauri kwenye baraza la mawaziri kwamba waziri wa fedha awaandikie barua hayo unayo yatapika sasa.Watu wengine mmshukuru Mungu kwa watanzania kuwa masikini na kukosa ufahamu otherwise mmeshachezea kiberiti na petrol
 
Kwa nini uwezo WA kutungwa/ kupata mimba usisubiri mpaka Mtoto amalize shule?.
Arudi school after how long?, Mtoto wake alee Nani?.
Akirudi shule analindwa tena na sheria ya kutokula tunda la mwanafunzi?.

Tukiwaambia hawarudi wakawa wanatoa Tu wanapata matatizo hata vifo.. baadaye tuwape vijana wetu wake waliotoa mimba ishirini kisa shule, Bora azae tumjue mapema tumdelete kwenye possible wachumba.

Ni wangapi ambao wakishapata mimba wako willing kabisa kabisa kurudi shule?, Ni kweli wanahitaji shule au tunawalaaimisha?. Vipi kuhusu uwezo wao?. He huko private nako huwa wanakata?. Government imekataza shule binafsi kuandikisha waliowahi kuzaa?.
Je sio fursa MTU kuanzisha shule ya wanafunzi WA namna hiyo?.

Huu ni mjadala mrefu,tusiuangalie kisiasa au Imani za kidini. Tuongee ukweli
 
Imagine mtu impatient kama huyo na asiekuwa na persuasive language ndio angekuwa waziri wa fedha si balaa huko kwenye kutafuta fedha za nje.

Halafu sasa udhani kama ata kasoma sababu hadi kupayuka ovyo. Walichosema WB ni mmoja wa decision maker kaomba zoezi liwe postponed baada ya kujitokeza viherehere dizaini ya kina Zitto.

Hila as far as they’re concerned kwa wao hakuna tatizo kutokana na ushauri wa mwakilishi wao wa region.

Halafu sasa kwenye international arena barua za wapuuzi zinapofika kwenye international media zinaibua hisia za international pressure groups and activists wa maswala husika.

Kukwepa lawama ya kuwa WB ina support serikari zenye sera kandamizi its logical for WB kuweza kuona umuhimu wa kulitolea ufafanuzi hilo swala na jinsi hela itakavyotumika hili kulinda reputation yao.

Whatever the reason sio muda wa povu kwa mtu makini, huyu Mwigulu lazima kavurugwa sehemu sio bure.
Tanzania utafikiri tumelaaniwa ...Inaelekea zile statics za Yeriko kuhusu werevu na Wajinga zina ukweli ndani yake.

Bunge letu limejaa wajanja wajanja tu ndiyo maana hata Rais akifukuza Waziri anapata shida kuteua mwingine wa maana kuzidi aliyemuondoa. Kwa ufupi tu ni kwaba Tanzania haina Leadership materials wa kutosha. Bungeni wengi ni Design za Msukuma, Kibabjaji .... wanachopishana ni VYETI tu. Wengine wana vyeti wengine hawana ....!!
 
Wazungu ni watu wema sana kuliko viongozi wa kiafrika!Wanatusaidia pmj na MiPhd yetu kutoka jalalani kwamba mtoto aliyechini ya miaka 18 hana uhuru wa kutosha katika kufanya maamuzi ni peer thinking hivyo anahitaji kusaidiwa akipata ujauzito lakini pia sio wote wanapata ujauzito kutokana na viherehere vyao lahasha wengine wanabakwa au kushawishiwa kutokana na mazingira duni ya kiuchumi,wengi wamepata ujauzito kwa kupewa msosi tu,hvyo tuwapinge akina Mwigulu na wengine wenye mawazo finyu kuhusu haki ya mtoto wa kike kupata elimu.Ebu tutumie common sense tu hvi mzungu ananufaika ninini katika hili?je mabinti hawa ni makenikia mpaka tuambiwe tunaowasupport sio wazalendo (unpatriotic) kama asemavyo Mwigulu na Phd yake?Sijui miafrika tukoje ndio inferiority complex.
Well actually personal I am not a supporter wa kumnyima mtu yeyote haki ya kupata elimu.

Dunia ya leo msemo wa kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha sio theory tena bali ni fact. Wameenda mbele zaidi elimu ni afya pia, kwa sababu inamsaidia mwanadamu kuweza kuchukua hatua za kujikinga kwa kuelewa wa madhara.

Nakubaliana na mtazamo wako wa ‘poor’ thinking kwa watoto ni sababu ya msingi; mabeberu jambo hilo wameliweka kama vulnerability.

Ya kwamba ni rahisi sana kumlaghai mwanafunzi kwa zege kuliko mtu mzima na ni rahisi sana mtoto kubakwa na kunyamazishwa iwapo familia itaamua kufumbia macho.

Kwa ivyo central to the problem sio mtoto kwa mtazamo wao bali society; ndio maana linapokuja swala la kutembea kimapenzi na mtoto wazazi nao wanafungwa kama walijua hawaku report.

Kama ni mashuleni iwapo walimu walijua kuna mwenzao anatabia hizo si ajabu na wao wakaenda jela au kufukuzwa pamoja kama awakutoa taarifa na mwalimu mkuu nae akaenda.

Ndio maana ulaya mwalimu akijulikana tu ana mahusiano na mwanafunzi wa sekondari chances utasikia kakimbia na nchi, vinginevyo siyo tu jela, ukitoka unakuwa kwenye sex offenders list na kwa wenzetu ukienda kuomba kazi criminal record lazima utaje na zingine upeleke CRB (kama vile uhakiki wa polisi) basically umeshaharibu maisha yako yote.

Kutokana na mziki wenyewe watu wazima ata wakiona mtoto paja, mgongo na chuchu zimenona sio kwamba awatamani lakini wakifikiria jinsi maisha yao yanavyoweza haribiwa wengi hawathubutu.

Sio sisi pamoja na hukumu kali bado ni rahisi kukwepa mikono ya sheria achilia mbali kutembea na watoto bali ata wanapopewa mimba, ukizingatia na shida za zilio wengi it makes it even easier to get away with.

Sasa badala ya serikari kupambana na wanafunzi inabidi iione jamii ndio tatizo zaidi. Na kutaka kuona more accountability kutoka huko kwenye service level.

In short ni vita ambavyo wanasiasa inabidi wapigane kuona more is done in terms of detering those acts, haki inapatikana na watoto wanapewa elimu sio lazima shule za kawaida.

Lakini aina maana kuandika barua ya kuzuia serikari ikose hela kabisa hapo hao hakina Zitto wamekosea lazima uangalie picha kubwa inapokosekana hiyo hela hakina nani nao wanaoathirika na kwanini waadhibiwe kwa maamuzi yasiyo yao.
 
Kwa hiyo kupata mimba ndo mwisho wa Elimu,,,?mtoto akipata mimba uwezo wake unaishia hapo,?fikiria Mara mbilimbili bro,,kupata mimba Ni kosa,,,ila Hilo kosa ila hukumu yake isiwe kunyima Elimu,,,,maisha yanaendelea daily,,,,,
kuna mambo mengine yanakera hasa kwa mtu mwenye uchungu na nchi yake kama Mwigullu. Hata mimi nasema wanaotetea ujinga huu wa watoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni ni wapumbavu, Tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne , Mwanafunzi alikuwa akpata ujauzito ni nyumbani moja kwa moja, kwanini leo ionekane ni kuwaonea? Nani anaweza kutoa ushahidi katika awamu ya JKN, MWINYI, MKAPA na JAKAYA mwanafunzi fulani alipata ujauzito akaenda kujifungua akarudi shule ya Serikali. Kasomeni Sheria na kanuni za Wizara ya Elimu kuhusiana na sheria za shule za Serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa wasipotoa kabisa atafaidika nini?, badala ya kutetea tupewe huo msaada anaungana na Zitto kabwe
Bora wakajengee shule binafsi za wanafunzi waliobeba mimba wakiwa shule, serikali hitawazuia.
Tukikubali kupangiwa mambo yetu ya ndani na ya kitamaduni na desturi tutaishia pabaya.

Juzi tu humu kuna mwana JF amekuja kulalamika familia yake inasambaratika kisa mdogo wa mkewe amezaa mtoto huku bado anataka kusoma huku analazim isha mtoto wa mwezi mmoja amuachie mke wa jamaa.

Kama angesubiri atimize malengo yake ya kieleimu kusingekuwa na kuvuruga ndoa ya dada yake.
Pili kusingekuwa na kumnyima mtoto mchanga wa mwezi mmoja kupata haki yake ya msingi ya kulelewa na mama mzazi, pia haki yake ya kunyonya maziwa ya mama hadi miezi sita kama inavyotakiwa kitabibu au kisayansi.

Mnalilia haki za hawa wasichana huku wanataka kukandamiza au kuzuwia haki za watoto wachanga kulelewa na mama zao hadi umri muafaka.

hili likikubaliwa lina athari kubwa sana kwenye malezi, tutakuja kupata taifa la watu wa ajabu wenye matatizo ya akili na malezi mazuri.
 
kuna mambo mengine yanakera hasa kwa mtu mwenye uchungu na nchi yake kama Mwigullu. Hata mimi nasema wanaotetea ujinga huu wa watoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni ni wapumbavu, Tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne , Mwanafunzi alikuwa akpata ujauzito ni nyumbani moja kwa moja, kwanini leo ionekane ni kuwaonea? Nani anaweza kutoa ushahidi katika awamu ya JKN, MWINYI, MKAPA na JAKAYA mwanafunzi fulani alipata ujauzito akaenda kujifungua akarudi shule ya Serikali. Kasomeni Sheria na kanuni za Wizara ya Elimu kuhusiana na sheria za shule za Serikali.
Kasome kwanza Education and Training Policy 2014 Tanzania(Sera ya Elimu na Mafunzo 2014) Ndani yake kuna Re-entry policy inayoruhusu watoto wa kike wanaopata mimba kurudi kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Sera hii ilisainiwa na Rais wa wakati huo Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.
Mpaka sasa sera hiyo haijafutwa, isipokuwa pamekuwa na matamko ya kejeli tu na vitisho vya kumnyima haki yaliyotolewa na viongozi wetu akiwamo Jiwe. Mara hatutaki kusomesha wazazi......mara wachague moja.
 
Attachments

JMK aliwaasa waache kiherehere. Nasikia nchi yetu ni mojawapo zinazoongoza kwa mimba za utotoni. Mimba za kiherehere hizo.
Watetezi wa "VIHEREHERE" ni WASALITI aina ingine. Imagine wasingekua viherehere wakahitimu masomo yao, badala ya hilo.
 
Hata kama ila walikuwa hawafukuzwi shule na siku ya mtihani wa mwisho anakuja na mimba yake au mtoto wake.
Hakuna kifungu kinachoonyesha mwanafunzi akishika mimba afukuzwe.
kuna mambo mengine yanakera hasa kwa mtu mwenye uchungu na nchi yake kama Mwigullu. Hata mimi nasema wanaotetea ujinga huu wa watoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni ni wapumbavu, Tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne , Mwanafunzi alikuwa akpata ujauzito ni nyumbani moja kwa moja, kwanini leo ionekane ni kuwaonea? Nani anaweza kutoa ushahidi katika awamu ya JKN, MWINYI, MKAPA na JAKAYA mwanafunzi fulani alipata ujauzito akaenda kujifungua akarudi shule ya Serikali. Kasomeni Sheria na kanuni za Wizara ya Elimu kuhusiana na sheria za shule za Serikali.
 
Kasome kwanza Education and Training Policy 2014 Tanzania(Sera ya Elimu na Mafunzo 2014) Ndani yake kuna Re-entry policy inayoruhusu watoto wa kike wanaopata mimba kurudi kuendelea na masomo baada ya kujifungua. Sera hii ilisainiwa na Rais wa wakati huo Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.
Mpaka sasa sera hiyo haijafutwa, isipokuwa pamekuwa na matamko ya kejeli tu na vitisho vya kumnyima haki yaliyotolewa na viongozi wetu akiwamo Jiwe. Mara hatutaki kusomesha wazazi......mara wachague moja.
Asante kwa kuleta hii, maana watu wasahaulifu au hawajui ila wako tu kuunga kila atakachosema Jiwe alimradi awaone awape uteuzi.
 
Hata kama ila walikuwa hawafukuzwi shule na siku ya mtihani wa mwisho anakuja na mimba yake au mtoto wake.
Hakuna kifungu kinachoonyesha mwanafunzi akishika mimba afukuzwe.
Kifungu kipo shuleni ni kosa lisilikuwa na marudi ni kufukuzwa tu ,nimeshuhudia watoto wengi wakifukuzwa shule wakati nasoma

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Akisajiliwa hafukuzwi na hoja yenu haina mashiko kwa sababu Rais kazuia kwa hyo inaonyesha zamani walikuwa wanaenda. Bila ya hivyo raid asingekataza
Kifungu kipo shuleni ni kosa lisilikuwa na marudi ni kufukuzwa tu ,nimeshuhudia watoto wengi wakifukuzwa shule wakati nasoma

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora wakajengee shule binafsi za wanafunzi waliobeba mimba wakiwa shule, serikali hitawazuia.
Tukikubali kupangiwa mambo yetu ya ndani na ya kitamaduni na desturi tutaishia pabaya.

Juzi tu humu kuna mwana JF amekuja kulalamika familia yake inasambaratika kisa mdogo wa mkewe amezaa mtoto huku bado anataka kusoma huku analazim isha mtoto wa mwezi mmoja amuachie mke wa jamaa.

Kama angesubiri atimize malengo yake ya kieleimu kusingekuwa na kuvuruga ndoa ya dada yake.
Pili kusingekuwa na kumnyima mtoto mchanga wa mwezi mmoja kupata haki yake ya msingi ya kulelewa na mama mzazi, pia haki yake ya kunyonya maziwa ya mama hadi miezi sita kama inavyotakiwa kitabibu au kisayansi.

Mnalilia haki za hawa wasichana huku wanataka kukandamiza au kuzuwia haki za watoto wachanga kulelewa na mama zao hadi umri muafaka.

hili likikubaliwa lina athari kubwa sana kwenye malezi, tutakuja kupata taifa la watu wa ajabu wenye matatizo ya akili na malezi mazuri.
mkichwa tope tu...najua mnaenda na beats za bwana mkubwa akibadilisha mtabadilisha mawazo.Huu ni ukenge uliiopitiliza,narudia tena mifumo mibovu ya kiuchumi kwa jamii ndio chanzo cha mimba kwa mabinti achilia mbali kubakwa.Nakuuliza hvi mzungu ananufaikaje na hili suala la kuwatetea watoto waliopata mimba?
 
kuna mambo mengine yanakera hasa kwa mtu mwenye uchungu na nchi yake kama Mwigullu. Hata mimi nasema wanaotetea ujinga huu wa watoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni ni wapumbavu, Tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne , Mwanafunzi alikuwa akpata ujauzito ni nyumbani moja kwa moja, kwanini leo ionekane ni kuwaonea? Nani anaweza kutoa ushahidi katika awamu ya JKN, MWINYI, MKAPA na JAKAYA mwanafunzi fulani alipata ujauzito akaenda kujifungua akarudi shule ya Serikali. Kasomeni Sheria na kanuni za Wizara ya Elimu kuhusiana na sheria za shule za Serikali.
Acha ujima wewe,tuko karne ya 21.jkn,mwinyi,mkapa ata kikwete sio marais.usiishi kwa kukalili
 
mkichwa tope tu...najua mnaenda na beats za bwana mkubwa akibadilisha mtabadilisha mawazo.Huu ni ukenge uliiopitiliza,narudia tena mifumo mibovu ya kiuchumi kwa jamii ndio chanzo cha mimba kwa mabinti achilia mbali kubakwa.Nakuuliza hvi mzungu ananufaikaje na hili suala la kuwatetea watoto waliopata mimba?
Umemaliza kutukana?
Ongeza matusi ukiridhika yametosha njoo tujadili hoja sio matusi.
 
kuna mambo mengine yanakera hasa kwa mtu mwenye uchungu na nchi yake kama Mwigullu. Hata mimi nasema wanaotetea ujinga huu wa watoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni ni wapumbavu, Tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne , Mwanafunzi alikuwa akpata ujauzito ni nyumbani moja kwa moja, kwanini leo ionekane ni kuwaonea? Nani anaweza kutoa ushahidi katika awamu ya JKN, MWINYI, MKAPA na JAKAYA mwanafunzi fulani alipata ujauzito akaenda kujifungua akarudi shule ya Serikali. Kasomeni Sheria na kanuni za Wizara ya Elimu kuhusiana na sheria za shule za Serikali.

Ni aibu sana kujiita TataMadiba halafu unatoa mawazo ya namna hii. Watu kama ninyi ni kwa sababu hamna wahanga wa mimba za utotoni.

Kweli unaweza kulinganisha mila na desturi au matendo ya zamani na leo au miaka 15 ijayo?? Hivi ukisikia “kuendelea” nini tafsiri yako?? Dunia ya na hata serikali yako inajihusisha na maswala ya dunia. Hivi unafahamu WID, WAD au WAG? Unajua habari za Gender Equality au Gender Equity? Ninaona sasa hujui elimu ni haki ya binadamu (bado uko kwenye malazi, mavazi na chakula)!! - hiyo historia unayoizungumzia.

Sifurahii kunyimwa mkopo huu kwa sababu najua ungeleta mabadiliko katika sehemu husika. Lakini kama maana yake ni kutetea mtoto wa kike - acha na iwe hivi. Tumieni pesa zenu wenyewe kufanya taratibu zenu - msitake pesa za mashirika ya kimataifa yanayofuata mambo mapya ya dunia kutekeleza mambo yenu ya awamu ya kwanza!!

Now that is fairness!!
 
kuna mambo mengine yanakera hasa kwa mtu mwenye uchungu na nchi yake kama Mwigullu. Hata mimi nasema wanaotetea ujinga huu wa watoto wa kike kupata mimba na kurudi shuleni ni wapumbavu, Tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza hadi ya nne , Mwanafunzi alikuwa akpata ujauzito ni nyumbani moja kwa moja, kwanini leo ionekane ni kuwaonea? Nani anaweza kutoa ushahidi katika awamu ya JKN, MWINYI, MKAPA na JAKAYA mwanafunzi fulani alipata ujauzito akaenda kujifungua akarudi shule ya Serikali. Kasomeni Sheria na kanuni za Wizara ya Elimu kuhusiana na sheria za shule za Serikali.
Unajua watanzania sijui tuna reasoning gani?? Kwanini msijenge mifumo itakayoepusha wanafunzi kubebeshwa mimba?? Mfano mkaweka shule za mabweni nchi nzima n.k unadhani mimba zitaongezeka?? Ila nyie mnaona kutimua ndio solution ?

Hivo hao watoto maelfu wakiacha shule kila mwaka tutakuwa na taifa gani la kesho?? Elimu ni haki ya kila mtu awe mvuta bangi au malaya. Mara 10 muweke fine au ban ya kuajiriwa serikalini ila sio ashindwe kusoma na kuandika eti kisa alifanya kosa!!!

Ni adhabu kubwa mnoo
 
Ni dhahiri Mh. Rais hakukosea kumtoa Mwigulu nchemba kwenye barraza la mawaziri. Waziri wa mambo ya nje na wengine wanapambana kutumia lugha ya diplomasia kuomba tusaidiwe, mwigulu nchemba yeye anatukana world bank bila kusahau bado yuko serikalini na kwenye chama tawala na alikuwa Waziri mwandamizi.

Ndugu yangu mwigulu, hapa umebugi stepu. Umeharibu, kama ni utetezi au kutaka kurudi kwenye baraza, haiwezekani. Pole sana kwa matusi yako kwa world Bank. Usisahau hawa watu wanafadhili miradi mingi na ndio mshirika pekee wa maendeleo alobakia. Use common sense bro. Naona huko kwenye ile kundi la wanaomhujumu Rais kijanja

View attachment 1338276
Hilo jina anavyoanza na DK ni kasoma soma au??? Kama ni la kusomea walah taifa linatatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom