Mwigulu Nchemba: CHADEMA itakufa 2015

Huyu ni zaidi wa tahira na
mwenda wazimu, Nchemba ni vibaraka wanao tumika na mafisadi au walanguzi wa ccm kuipotosha jamii zetu, sasa ajue cc vijana wa kitanzania hatuangalii cha Dr Slaa wa viongozi wa Chadema tunachotaka na kudhamiria ni kuiona ccm inaondoka madarakani kwa mbinu zote,jukumu la kizazi chetu ni kuiondoa ccm madarakani kama lilivyo jukumu la wakina nyerere kumuondoa mkoloni kwa kuipatia Tanganyika huru,
HUYU MHUNI mkuu Nchemba tuna kuhakikishia labda ufe kabla ya muda ila wajinga wenzako walionunuliwa akili ndani ya ccm mtashuhudia, tunajua lengo lenu sio kumshambulia Slaa ila ni kuiua wimbi la mabadiliko kwa kizazi cha sasa cha watz,mtawa nunua wengi, mtawa katisha tamaa wengi na mtawadhuru wengi ila hadi kieleweke mana hii ni kazi ya mungu lazima yatimia kwamba watz tutaondoka mikononi mwa ccm.
Wewe Na Nape endeleeni ila mtakuwa mashahidi kwa kila jambo mlofanya na kupanga kufanya ktk kuhujumu tumaini jipya la Watz.
Wapeni salamu zangu fisadi lowassa, na mzee dhaifu bila kusahau mchawi mropokaji Makamba sr.
 
Mwigulu tumeshamzoezea kwa uropokaji wake. CDM haiwezi kufa kwa utabiri feki wa Mwigulu. Kwa hiyo Mwigulu siku hizi amegeeuka kuwa sheikhe Yahaya. Hivi hawezi kujifunza kwa huyo sheikhe aliyetabiri kuwa Dr. Slaa atakufa na matokeo yake akafa yeye? Mwigulu awe makini asije akajikuta anakufa yeye na CDM inaendelea kupeta. CDM imo mioyoni mwa Watanzania kwa hiyo hata siku moja haiwezi kufa kwa kuwa hakuna mbadala zaidi ya CDM katika safari ya kulikomboa taifa hili kutoka katika mikono ya mafisadi na wezi ambao ni CCM aka magamba
 
Wewe ndo umepita na wakati kweli. Mbona u mvivu wa kujisomea na kufikiri. Umesahau kuwa rais kibaki ameingia madarakani akiwa na miaka 72? Jisomee acha uvivu wa kufikiri. Je umesahau kuwa Michael Sata wa Zanzibar aka Super Cobra ameingia madarakani akiwa na umri wa miaka 76? Tatizo lenu watu wa CCM aka magamba ni wavivu wa kufikiri na kujisomea ndo maana mnasaini mikataba bila hata ya kujua kilichomo.
Umri umemtupa mkono Dr Slaa, Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 Dr. Slaa atakuwa na umri wa miaka 70.
 
Keep talking b....!


Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 

Ama kweli CCM ya sasa ni vituko tupu
 
aka mkosa chama tatizo la Watz tunashabikia tusilolijua kwani hamjua vita iliyopo cdm? kama hamjui hicho chama cha wachaga mtadanganyika mpaka lini fuatilieni mtaona au ni chama cha mzee Mtei

nakubaliana na wewe kilaza, tofauti chademai ni cha wachaga kama unavyolazimisha wewe na ccm ni ya mafisadi, Unafahamu kwamba binadamu akibanwa haja ni lazima aende kunakotakikana, hivyo umezidiwa haja ndo maana unasema cdm ni cha wachaga, tujadili suala la msingi nini maoni yako kuhusu mfumo wa sheria ukizingatia ufisadi ktkt serikali ya tz inayo ongozwa na ccm?
 
natoa wito kwa makamanda wote cdm kuwa makini na fedha chafu wanazo tumia wenzetu kujaribu kutuvuruga.tukatae ushawishi wa aina yeyote ile.chama chetu ni imara na sisi tuwe imara kama ni dhiki tumepata vyakutosha tusidanganywe na walafi wachache tukaiacha ikazidi kunajisiwa na hawa ccm .waliotugeuka tuachane nao ila mungu yuko upande wa wanyonge siku zote.Laana itakayo wakuta wasaliti wetu itawagarimu vizazi vinne.Tusonge mbele bila woga hakika ipo siku mama zetu watajifungua salama na shule zetu za kata zitakuwa na maabara za kisasa.maji safi na salama kwetu sote nawsilisha
 
Mbona kifo cha CHADEMA kinazidi kuahiliswa?tuliambiwa itakufa 2012,ikavuka salama,sasa tunaambiwa 2015!kulikoni?????????????

Kwa sasa CCM sijui kama kuna mtu ana uwezo wa kukaa chini na kuja na mikakati............. ndiyo maana wamemrudisha Mangula ambaye sidhani kama anaweza. Kwa sasa ni mwendo wa kuropoka tu kwenda mbele. We hushangai akina Nape mpaka wanazungumza mambo yao binafsi wakati wanahojiwa mambo muhimu ya kitaifa. Eti Board imemkumbusha hivi kariburni kulipa mkopo wake.......... hivi jina lake haliko kwenye ile website au hawakulitoa gazetini walipotishia kuwapeleka mahakamani??

!995 Nyerere aliwaambia wasihangaike na Mrema......... tishio ni CDM wao hawakusikia kwa vile hawana strategy wanafuata upepo. Sasa upepo wa siku hizi ni tofauti na zamani..... suku hizi unakuja kwa kindisho kama cha Harrycane....!!!
 
Chadema na viongozi wake wanaitesa ccm ile mbaya. Kiongzi wa ccm ili aonekane anafanya kazi lazima aseme kitu kibaya kuhusu chadema. Bahati mbaya hawajui in so doing watu wenye akili wanajua chadema ni hatari kwa ccm.

Ccm endeleeni kuifagilia chadema.
 
Mimi naomba kuuliza wana Jf, Mwigulu ni kwamba hana akili timamu, kichaa, bange au ni njaa ndiyo inamsumbua?
 
Sijaona mtu mpumbavu kama Mwigulu. Atakufa yeye Chadema ataiacha.
 
Mwigulu.......,Hopeless guy.
Utakufa wewe,CHADEMA HAIWEZI KUFA.
Dr Slaa KIBOKO YENU,lakini hata bila yeye itabaki imara tu.
Mwigulu wewe na chama chako,CCM..Wananchi wameishawachoka,ila mmeziba masikio.
JK na Viongozi wa juu wa CCM sera yenu kuu ni UFISADI.
RUSHWA KILA SEHEMU;-Mahakamani,Police,Huduma za Afya,TRA,Ardhi,Halmashauri,Utalii,nk..
Kuwa CCM lazima uwe FISADI na UPENDE RUSHWA.
MNATAFUTA WACHAWI,...WACHAWI NI NINYI WENYEWE,
WANANCHI WAMEWACHOKA KWA MATENDO YENU.
WANANCHI mmeishawachosha na Blah Blah zenu kuhusu rasilimali zao,kwani wao hawajui kuwa
gesi ni ya Wa-tanzania wote?
Lakini rasilimali hizo zinawanufaisha wachache,akina Kinana,EL,Mzee wa Vij......nk
CHADEMA INA NGUVU YA UMMA,WEWE ENDELEA KUPIGA DEBE NA HUYO HAYATI(CCM) UTAJIKUTA
UMEBAKI PEKE YAKO.
 
Kweli inaingia akilini kwa mtu mzima kubashiri kifo cha mpinzani wake? Kweli unaweza kumbashiria kifo mshindani wako wa biashara? Mwigulu na Nape ni mbumbumbu wa siasa za kistaarabu, I hope mwisho wao JK akimwaga manyanga.
 
Samahani mwigulu alimaanisha ccm itakufa 2015, ni bahati mbaya mdomo uliteleza tuu maana anaigwaya sana cdm, ndo maana akaitamka. Kiukweli alimaanisha ccm
 

1948-2015 ni miaka 67.

Je hivi vizee/vibabu vya CCM vinavyo ng'ang'ana kugombea Urahisi kwa tiketi ya Chama Twawala 2015 vitakuwa na umri gani????
  1. Steven Masato Wassira born: 1945-2015..............70 years
  2. Edward Ngoyay Lowassa born: 1950-2015.............65 years
  3. Samwel Sitta born: 1942-2015............................73 years
  4. Benard Membe born: 1952-2015........................... 63 years
  5. Kingunge Ngombale Mwiru born:192x-2015..............9x years!

Nelson Mandela alianza kuingoza South Africa akiwa na miaka 76( Born 191😎 mnamo mwaka 1994. Kwa hiyo swala la uzee kwa umri kwa uzee halina mashiko. CCM ndo kwanza kumejaa vijeba kuliko hata CHADEMA!
 
Hivi huyu jamaa ndio amekua msemaji wa magamba nn! Hajui majukumu yake kabisa.
 
Kauli aliyotoa Mwigulu kuhusu Chadema ni ileile aliyoitoa Wasira,ndo hapo ujue wanaelekezwa hata kufikiria,Wasira alikopeshwa mawazo kuwa CDM itakufa 2013 baada ya utabiri huo kushindwa amekopeshwa Mwigulu mawazo hayohayo CDM itakufa 2015.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…