Mwigulu Nchemba: CCM imejenga shule za kata, CHADEMA mbona hawajajenga hata chumba?

Wewe humshangai Mwigulu bado?!Hujashtuka tu?!
Kwanza anasema CCM imejenga shule za kata halafu hapo hapo anailaumu CHADEMA (LISSU) kwa kuwakataza wananchi "KUJENGA" shule...Shule zipi tena?!
Kuhusu suala la ofisi; ni ujinga kuilinganisha CHADEMA na SERIKALI!CHADEMA haikusanyi kodi hivyo haiwajibiki BUNGENI katika kujenga au kutojenga ofisi! Serikali chini ya CCM inakusanya kodi kwa wana CHADEMA, CCM.TLP.CUF,JAHAZI ASILIA na wale wasio na vyama..! Kama kweli CCM inajenga shule,basi wana CCM pekee ndiyo wanaopaswa kutoa michango/kujenga ili wajisifu vyema!
Mwisho,ili tujue kwamba kujenga ofisi za vyama ni jambo rahisi NI BORA tuambiwe tangia mwaka1992,CCM imeweza kujenga ofisi ngapi za chama!
 
Back
Top Bottom