Mwigulu Nchemba: CCM imejenga shule za kata, CHADEMA mbona hawajajenga hata chumba?

sokoinei

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,832
566
Leo akichangia hotuba ya Wizara ya elimu,kama kawaida yake mh Mwigulu aliacha kuchangia mambo ya msingi ktk hotuba iliyokua mezani ya Mh Mulugo waziri wa Elimu na badala yake akaanza kutoa Vijembe kama kawaida yake kwa CHADEMA kwamba anashangaa kama na wao (CHADEMA) wanalalamika kwa matokeo ya kidato cha nne 2012 huku akijua kua wao CHADEMA kufeli kwa wanafunzi hao ni Furaha yao na ndicho walichokua wanakitaka.

Alisema iweje CHADEMA wajidai wana uchungu na wanafunzi kufeli na kushuka kwa elimu huku wao (CHADEMA) wakiwahamasisha wananchi wasijenge shule!
Aliwaomba Watanzania kuwaogopa Wasanii na Waigizaji wanaojidai wana uchungu na nchi hii huku wakiikosoa Serikali kwa kisingizio cha kuwa wanaikosoa CCM. alisema hakuna nchi inaitwa CHADEMA bali kuna nchi inaitwa Tanzania ya Watanzania. Hivyo yeyote anaepinga Serikali haipingi CCM bali anawapinga Watanzania.

Akimalizia alisema kuwa anawashangaa CHADEMA kukosoa Shule za kata zilizojengwa na CCM huku wao wenyewe (CHADEMA) hawajawahi hata kujenga chumba kimoja zaidi ya kishia kupanga Viofisi vya Chama.

Akichangia hotuba hiyo Mbunge wa Mbulu mh Mustapha Akunay alisema kua Watanzania wasipotoshwe kwani Shule za Kata zimejengwa kwa nguvu za Wananchi wakishirikiana na Serikali. Na kwamba hakuna hata Shule moja iliyojengwa na CCM kwani shule hazijengwi na vyama vya Siasa.
Nawakilisha.
 
Duh huyu mheshimiwa Lameck naona kama wananchi wa jimbo lake walimchagua ili aende kuwaponda CHADEMA huko mjengoni. Huyu msomi wa first class kwa ufupi ukiangalia mambo yake anayoyafanya i.e. Maneno, na matendo kama mavazi yenye nembo, marangi rangi atakuwa manic. Madaktari tusaidieni.
 
Muonggooooooooooooo shule za kata hazijajengwa na CCM ni wazazi walichanga ela tena kwa kulazimishwa na wenyeviti wa vijiji,

mf kwetu Rombo kila kaya walichangia sio chini ya elfu 20,

wajinga wataiamini kauli yake.
 
Hivi akili za binadamu wote hukaa kichwani kweli?mie nakataa!kuna wengine hukaa sehemu nyingine za mwili!hapo hapo anasema shule hazijengwi na CCM chama cha siasa bali serikali na wananchi halafu hapo hapo anataka Chadema wajenge shule kwani Chadema ni wizara ya elimu au pia chama cha siasa?huyu mbunge wenu amechoshwa sana akili na hili dude Chadema please,mpumzisheni tu 2015!
 
Uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana tangu lini vyama vya siasa vikajenga shule?na kama anajivunia hayo majengo ya ccm hivi hajui kwamba majengo yote yalijengwa wakati wa chama kimoja ikimaanishwa kwamba vilijengwa kwa fedha za wananchi wote?Ilipaswa kurudisha majengo yote serikalini pale tulipoanzisha vyama vingi na iko siku tutadai majengo yote yarudi serikalini kama wataweza hapa kupangisha chumba
 
Kwani Chadema ndio wenye serikali? amesahau kuwa hata hizo ofisi anazofikiri ni za CCM kuwa zilijengwa kupitia nguvu za wananchi wakati ulipokuwepo mfumo wa Chama kimoja na zilipaswa zimilikiwe na Serikali wala sio Chama? nafikiri huyu jamaa huwa anavuta bangi kabla ya kuingia bungeni
 
Eti Lameck Mkumbo ndiyo THINK TANK YA CCM, first Class economist! CCM wanajenga SHULE? Kumbe CCM siku hizi inakusanya kodi? Nitaacha kulipa kodi kama kodi yangu inakwenda CCM.

Give me a break Lameck Madelu Mkumbo ALIAS Mwingulu Nchemba
 
Uwezo wake wa kufikiri ni mdogo sana tangu lini vyama vya siasa vikajenga shule?na kama anajivunia hayo majengo ya ccm hivi hajui kwamba majengo yote yalijengwa wakati wa chama kimoja ikimaanishwa kwamba vilijengwa kwa fedha za wananchi wote?Ilipaswa kurudisha majengo yote serikalini pale tulipoanzisha vyama vingi na iko siku tutadai majengo yote yarudi serikalini kama wataweza hapa kupangisha chumba

Mkuu,mi viwanja vya mpira ndo navimind,eti ccm kirumba! mafi ya mende.
 
Nimefuatilia uwezo wake mdogo sana very poor arguments....!! Huko Iramba wana hasara...ngoja katiba mpya....!! Mbivu na mbichi.
 
Nchema, Mtela, Shonza akili zao wameamua kujifanya vichaa wakati wanafahamu kinachoendelea. Lakini ni ujinga wa aina nyingine kudhani kwamba wananchi ni wajinga kiasi hicho na eti kwamba wanasubiria wao tu ndio wawafute ujinga.
Wanadanganyana na
kufarijiana utadhania
wanatumia mrijuana
vipi hawa Watanzania?
 
Nimefuatilia uwezo wake mdogo sana very poor arguments....!! Huko Iramba wana hasara...ngoja katiba mpya....!! Mbivu na mbichi.

If you do not want to spoil your day ukiona Nchemba amepewa nafasi ya kuchangia hoja bungeni ni bora ukaondoka. This guy is never serious in anything apart from kuzungumza siasa hata bungeni.
 
Tatizo lake huyu gambamwitu anafikiria kwa kutumia tumbo.... Hashughulishi ubongo wake kabisa
Naanza kupata mashaka huenda elimu yake ya chuo kikuu ilipatikana kwa njia za ULIBERALI...
 
Back
Top Bottom