Mwigulu Nchemba afanikisha harambee Milion.19, Aivaa CHADEMA

Mwigulu Nchemba afanikisha harambee Milion.19, Aivaa CHADEMA

Kuna makanisa machache sana yenye misimamo na yenye kufuata taratibu za Kimungu, mengine yamebaki kuganga njaa tu. Viongozi wanayatumia kutekeleza malengo yao. Ni aibu kanisa kugeuzwa sehemu ya kampeni, madhabahu ya Mungu yamekuwa kama majukwaa ya kawaida tu yeyote anaweza panda na kuongea anachojisikia. Makinisa yako kwenye ushindani wa majengo ya kifahali na wingi wa matoleo badala ya kumtafuta Mungu.
 
Tangu jopo jipya la safu ya viongozi wa ccm kuingia madarakani mwigulu akiwemo chadema hata pakushika hawana wamebaki kutukana.
 
Waovu mtawajua kwa matendo yao..
Hupenda kukaa viti vya mbele katika ibada na kutumia muda wao mwingi kujitapa na kuwatukana wengine.
Hupenda kutoa fedha zao nyingi za damu ili wasifiwe na watu
Hupenda kujitangaza kuwa ni wema machoni pa watu ktk masoko na nyumba za ibada.
Hujiona wao ni wema na waadilifu zaidi ya wengine.
Amin nawaambia thawabu yao ni moto mkali uwakao milele.huko ndiko kuna kilio na kusaga meno.
 
Huko Kanisani alienda kuombea amani kweli? Hivi amani iliyokuwepo huko nyuma ilitokana na maombi hayo? Unajua kama kuna upuuzi duniani ambao mtu anaweza kuufanya ni kutokutumia akili. Hivi polisi akiamrishwa ampige risasi raia ambaye hana chochote mkononi mwake, utamwambia mtu huyo aende kanisani akaombe amani?

Serikali inalo jukumu la ulinzi wa raia wake, lakini inaposhindwa kufanya kazi hiyo inawaambia watu waende makanisani na misikitini eti kwamba amani iweze kupatikana. Ni nadharia gani inazungumzia upatikanaji wa amani wa namna hiyo?

nadharia ya chama dola hiyo mkuu.
 
So haki ni nini?
Wewe na degree zako za India na maswala ya diplomasia ulipaswa ufahamu HAKI ni nini na AMANI ni nini?.

Nenda kapate kwanza mwanga kuhusu Deontological ethics and Concept of justice upate kuweza kuliweka neno HAKI sehemu ambayo linapaswa liwe, kwa wakati gani na madhumuni gani.

Nani kakwambia kila amani ni tunda la haki na kwenye haki kuna amani.
 
CHADEMA wamekariri "amani ni tunda la haki" bila hata kuelewa maana ya haki katika jamii.

Ukiwauliza haki ni nini hawana hata majibu wakati kila siku wanasema walianza na Mungu na watamaliza na Mungu.

Wanaosema amani ni tunda la haki, they can't even talk the talk and walk the walk.

PEACE is earned or given?If you want peace then You have to work for it and to beg for it.Guarantee people jobs,medical care,education,good housing and people will have a peace of mind because they have nothing now to worry and eventually have the real peace(physical peace).With the regard to the situation we are in today,We will have to fight for our rights to maintain peace.
 
-Ha!ha!ha!ha!ha! Mwzee wa sumu ya panya you know, kumbe hawa mburulaz bina majangaz wa ukwe bado wapi. Walahi kama vipi Masali kiboko. Nilidhania sumu ya panya iliwaua enzi zile

-Imean, super sana CCM bado ni Imara, ila hawa mabaki ya CDM hatuwataki. Ben Saanane inabidi ufanye kazi nzuri kuwaangamiza hawa panya wa Prezo you know, kama vipi huyu mbebs ajipange sana arudi kwaho Bavicha

umeandika nini hiki?
 
nenda kuzimu.hujawahi kukose hata herifi moja wapumbavu kama ww na kidigr cha india unajifanya unajua kila kitu .nyambafu.

teja vipi? Umekolea na kitu cha pakistan? Naona lugha kali watumia.
 
Wewe na degree zako za India na maswala ya diplomasia ulipaswa ufahamu HAKI ni nini na AMANI ni nini?.

Nenda kapate kwanza mwanga kuhusu Deontological ethics and Concept of justice upate kuweza kuliweka neno HAKI sehemu ambayo linapaswa liwe, kwa wakati gani na madhumuni gani.

Nani kakwambia kila amani ni tunda la haki na kwenye haki kuna amani.

Unaweza kuilinganisha Degree ya India na ya Bongo?Usiishi kwa kukariri mkuu.
 
Naibu katibu mkuu wa CCM na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi ameshiriki kikamilifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa wilaya ya singida Vijijini,kata ya Kijota Usharika wa Mijuhu jimbo la Mashariki Dayosisi ya kati KKKT.
Mbunge huyo amefanikisha upatikanaji wa Tsh.Milioni 19 na laki tisa na themanini.Pia amefakisha upatikanaji wa viti 500 vya plastic kama hatua ya awali katika kufanikisha ujenzi wa kanisa hilo.

Ikumbukwe Mbunge huyo anayevuma kwenye medani za siasa yawezekana kuliko mbunge yeyote kwa sasa hapa nchini,yupo jimboni kwake kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.Jana alianza kwa kufanya vikao vya ndani na madiwani na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.
Pia siku ya jana alitumia kuhamasisha michezo jimboni kwake na wilaya mpya ya Mkalama ambapo Mbunge huyo alishiriki kucheza mechi ya mpira wa miguu akiwa upande wa madiwani.

Kwenye harambee ya leo mbunge huyo Mh.Mwigulu Lameck nchemba madelu alitumia nafasi kuongea na washarika na wananchi wa kata ya kijota,kijiji cha Ikuwi kuwaomba kuachana na tabia ya kulishwa maneno na wanasiasa na viongozi mbalimbali kuhusu serikali yao eti haifanyi kazi.
Amesisitiza kuwa endapo wananchi na viongozi wa vyama vya siasa wangemrudia mungu,wangejikita kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada,kushiriki kwenye huduma za kiroho leo hii Tanzania tusingekuwa na aina hii ya viongozi wa vyama vya siasa hasa upinzani wenye uroho wa madaraka,wanaomwaga damu za watanzania ili tu wapate madaraka ndani ya nchi hii.
Mh.Mwigulu nchemba amekwenda mbali zaidi kwa kulaani vikali kauli ya kiongozi wa CHADEMA Dr.slaa yakuwambia viongozi wa dini waache kuombea amani ya nchi.Amesema viongozi kama hao ni wakupuuzwa kabisa kabisa,na niwazi Dr.slaa na chama chake hana nia njema kwa nchi yetu.Ni kwasababu aliachana na misingi ya dini na kiroho ndio maana uwezo wake wa kufikiri kuhusu amani ya nchi ni hafifu kupita kiasi.
KESHO Mh.Mwigulu Nchemba ataendelea na kazi ya kuzungukia miradi ya maendeleo hususani barabara ndani ya jimbo lake.
ASANTE.

Naomba tujiulize mimi na wewe mleta mada,hivi katika vitu vya maendeleo katika jimbo hilo ni ujenzi wa kanisa? Vipi shule zina madawati,je shule zina vitabu vya kutosha? Unapokwenda kutoa hotuba makanisani na kutoa tuhuma dhidi ya chama kingine je kuyazungumza hayo kanisani ni sehemu yake je kwa hili tunamtofautisha Mwigulu na mambo aliyoyafanya Lipumba?
 
.......nasikia jimbo liko wazi!!!!
Mtaendelea sana kusubiri mkono uanguke mithili ya fisi.

CCM tunaendelea kutekeleza ilani yetu ya uchaguzi 2010 na kila tunapojikwaa hatuanguki bali tunaendelea na safari ya kisiasa kama ilivyo toka 1995.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom