Mwigulu Nchemba afanikisha harambee Milion.19, Aivaa CHADEMA

Mwigulu Nchemba afanikisha harambee Milion.19, Aivaa CHADEMA

Taswira

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
1,198
Reaction score
452
Naibu katibu mkuu wa CCM na mbunge wa jimbo la Iramba magharibi ameshiriki kikamilifu kwenye harambee ya ujenzi wa kanisa wilaya ya singida Vijijini,kata ya Kijota Usharika wa Mijuhu jimbo la Mashariki Dayosisi ya kati KKKT.
Mbunge huyo amefanikisha upatikanaji wa Tsh.Milioni 19 na laki tisa na themanini.Pia amefakisha upatikanaji wa viti 500 vya plastic kama hatua ya awali katika kufanikisha ujenzi wa kanisa hilo.

Ikumbukwe Mbunge huyo anayevuma kwenye medani za siasa yawezekana kuliko mbunge yeyote kwa sasa hapa nchini,yupo jimboni kwake kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.Jana alianza kwa kufanya vikao vya ndani na madiwani na viongozi mbalimbali wa chama na serikali.

Pia siku ya jana alitumia kuhamasisha michezo jimboni kwake na wilaya mpya ya Mkalama ambapo Mbunge huyo alishiriki kucheza mechi ya mpira wa miguu akiwa upande wa madiwani.

Kwenye harambee ya leo mbunge huyo Mh.Mwigulu Lameck nchemba madelu alitumia nafasi kuongea na washarika na wananchi wa kata ya kijota,kijiji cha Ikuwi kuwaomba kuachana na tabia ya kulishwa maneno na wanasiasa na viongozi mbalimbali kuhusu serikali yao eti haifanyi kazi.

Amesisitiza kuwa endapo wananchi na viongozi wa vyama vya siasa wangemrudia mungu,wangejikita kusaidia ujenzi wa nyumba za ibada,kushiriki kwenye huduma za kiroho leo hii Tanzania tusingekuwa na aina hii ya viongozi wa vyama vya siasa hasa upinzani wenye uroho wa madaraka,wanaomwaga damu za watanzania ili tu wapate madaraka ndani ya nchi hii.

Mh.Mwigulu nchemba amekwenda mbali zaidi kwa kulaani vikali kauli ya kiongozi wa CHADEMA Dr.slaa yakuwambia viongozi wa dini waache kuombea amani ya nchi.Amesema viongozi kama hao ni wakupuuzwa kabisa kabisa,na niwazi Dr.slaa na chama chake hana nia njema kwa nchi yetu.Ni kwasababu aliachana na misingi ya dini na kiroho ndio maana uwezo wake wa kufikiri kuhusu amani ya nchi ni hafifu kupita kiasi.

KESHO Mh.Mwigulu Nchemba ataendelea na kazi ya kuzungukia miradi ya maendeleo hususani barabara ndani ya jimbo lake.

ASANTE.
 
"Biti 500 ni nini!"

Amani ni tunda la haki.Utaombeaje amani nje ya mantiki?
Hueleweki mkuu jipange upya.Soma habari kwanza,unahama kwenye topic ya Mh.
MSALIMIE josephine Mshumbusi shemeji yako.
 
Hivi huyu chizi naye nani atamsikiliza?Ndio maana idadi ya watu wasio na inaongezeka Tanzania kwasababu wanapoteza imani na viongozi wao wa dini.Hawa watu walipaswa kutengwa na kanisa na baadaye walazimishwe kutubu kwa kuwaomba msamaha Watanzani kutokana na mambo maovu waliyowafanyia lakini ndio kwanza wanapewa heshima ya zulia jekundu.Pesa imewageuza viongozi wetu wa dini kuwa majukwaa ya wanasiasa waovu kwenda kujisafisha kisha wanaendelea na maovu kawaida wakijuwa fika kuwa kesho wataenda kujiosha tena katika macho ya waumini.Kwanini tunaruhusu hizi imani zinajisiwe na wanasiasa wachafu kama hawa?
 
Huko Kanisani alienda kuombea amani kweli? Hivi amani iliyokuwepo huko nyuma ilitokana na maombi hayo? Unajua kama kuna upuuzi duniani ambao mtu anaweza kuufanya ni kutokutumia akili. Hivi polisi akiamrishwa ampige risasi raia ambaye hana chochote mkononi mwake, utamwambia mtu huyo aende kanisani akaombe amani?

Serikali inalo jukumu la ulinzi wa raia wake, lakini inaposhindwa kufanya kazi hiyo inawaambia watu waende makanisani na misikitini eti kwamba amani iweze kupatikana. Ni nadharia gani inazungumzia upatikanaji wa amani wa namna hiyo?
 
Piga kazi mkuu. Bavicha wanachonga sana humu JF we fanya mavitu huko jimboni.
 
"Biti 500 ni nini!"

Amani ni tunda la haki.Utaombeaje amani nje ya mantiki?

-Ha!ha!ha!ha!ha! Mwzee wa sumu ya panya you know, kumbe hawa mburulaz bina majangaz wa ukwe bado wapi. Walahi kama vipi Masali kiboko. Nilidhania sumu ya panya iliwaua enzi zile

-Imean, super sana CCM bado ni Imara, ila hawa mabaki ya CDM hatuwataki. Ben Saanane inabidi ufanye kazi nzuri kuwaangamiza hawa panya wa Prezo you know, kama vipi huyu mbebs ajipange sana arudi kwaho Bavicha
 
mungu hadhihakiwi chochote apandacho mtu ndicho atakachovuna.ukiwa mnafiki utavuna unafiki muda ukifika.
 
kuna haja ya jumuia kama cct na jumuiya nyingne za kislam kuliangalia hili suala la siasa kwenye nyumba za ibada. La si hivyo ndio kwa style hii aman inatoweka kidogokidogo. Chuki inaanzia hapa.
 
Ujinga mtupu.Ni aibu kuleta upuuzi huu hapa jamvini.
 
Mwaka huu makanisa na misikiti itapata wafadhili wengi sana. Lakini mbele ya safari wakirudi kwa ajili ya kampeni wasizuiliwe. Wakati wa shida wanasiasa wamatumika kuchangia ujenzi wa makanisa na misikiti, viongozi wa kanisa wasiwasahau wakati wa uchaguzi.

Hiyo hatari iliyopo makanisani na misikitini ni kubwa kuliko ufisadi wenyewe. Viongozi wa kanisa naomba niwaulize swali, hivi hayo makanisa mkishindwa kuyajenga kwa michango ya waumini wenu mtakwenda jehanamu? Mtatoa wapi ujasiri wa kuwakemea mafisadi kama fedha zao mnazijengea makanisa?
 
kuna haja ya jumuia kama cct na jumuiya nyingne za kislam kuliangalia hili suala la siasa kwenye nyumba za ibada. La si hivyo ndio kwa style hii aman inatoweka kidogokidogo. Chuki inaanzia hapa.

Kweli anajulikana sana kwa siasa za maji taka

Hata hao waliomkaribisha kwa harambee hawana hofu ya Mungu, yaani Mwigulu amchangie Mungu sadaka? Muuaji, mkubwa huyu, sadaka yakw haina tofauti na ile ya Kaini,
 
Back
Top Bottom