Mwigulu Nchemba achomoza urais 2015

Mwigulu Nchemba achomoza urais 2015

5556a4c0-ad2e-11e4-a106-450870834ba2_Ashley-Graham-Sports-Illustrated.jpg
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge Jaku Ayoub amesema Mwigulu muda si mrefu utakuwa mkuu wa Nchi.

Jaku Ayoub ni Mbunge kutoka baraza la wawakilishi, ameyasema leo kipindi cha maswali na majibu Bungeni baada ya Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kujibu swali lake la msingi.

My take: CCM kuweni makini na huyu Kijana.

Huyu Mbunge ana historia yoyote ya utabiri hapo kabla? Otherwise atakua anaropoka tu!!
 
Huyo mbunge hajielewi kama Jungu Kuu(JK) maana Jungu Kuu lipolipo tu,kazi yake ni kukumbatia viporo,vitu vichafu na vilivyooza ambavyo sio salama kwa afya ya binadamu
 
huku mtaani wanasema mwigulu ni kikwete wa pili
 
Hata mm ukinipa laki5 namtamka kumtabiria mtu ubunge au Urais
 
KUTOKA KILIMANJARO HOTEL(KEMPISK)Dr Wilbrod Slaa amwagia Sifa Mwigulu Nchemba mbele ya Rais wa Ujerumani

Katika hali ya kustaajabisha na isiyotarajiwa kutokana na historia ya nyuma, leo Dr Slaa amemwagia sifa Naibu Waziri wa Fedha Ndg Mwigulu Nchemba akianza kwa kusema kwa kingereza kama ilivyotafsiriwa, Namshukuru mungu nimekuona uso kwa uso leo, " CHADEMA tulikuwa tunakuchukia, na mimi binafsi nilikuwa nakuchukia sana, tulidhani unatushambulia, kumbe wewe ni mkweli, ni jasiri na ni mzalendo wa kweli wa Taifa hili ambaye huogopi kukosoa uovu, nimefuta msimamo wangu juu yako wa jinsi nilivyokuwa nakuchukulia, wewe ni hazina kubwa ya Taifa leo.
Dr.Slaa ameyasema hayo mapema hii leo wakati wa Mkutano wa Viongozi wa vyama vya siasa na Rais wa Ujeruman ambaye tangu jana yupo Nchi kwa Ziara ya kikazi.Katibu Mkuu huyo wa Chadema aliendelea kusisitiza kuwa "Sasa watanzania wanakupenda na hata sisi CHADEMA tunakupenda na tunakutegemea kwa maslahi ya Taifa. Msimamo uliouweka kwenye sakata la ESCROW, katiba, wakwepa kodi matajiri, wenye matumizi mabaya ya fedha na kuayakemea mafisadi bila kujali yapo CCM umekutambulisha kuwa wewe ni nani, waliokuita jina la SOKOINE WA PILI hawakukosea, kwanini wewe ni Naibu Waziri tu lakini tunaiona ladha ya Sokoine na kivuli cha Sokoine, naamini ungekuwa Waziri mkuu kama alivyokuwa Sokoine tungemwona Sokoine Mweneyewe. Tunajua mafisadi watakuchukia ila songa mbele Taifa liko nyuma yako. Sisi hatuna sababu ya kupingana au kumchukia mtu mzalendo."Alisisitiza Slaa.

Kwa upande wake Prof Lipumba ambaye siku za karibuni amekumbana na kashikashi za Jeshi la polisi amesema "mimi ni Mwalimu wa uchumi, Mwigulu ni First Class Economist kweli amefuzu kwa kuelewa, tatizo watu kama hawa huwa ngumu kueleweka na mawazo yao kutumika. Mimi nimeshauri sana, sidhani kama huwa nasikilizwa, wewe umeonesha tofauti kubwa sana katika muda mfupi.
Nadhani watanzania wasiangalie muda uliokaa Wizaran bali waangalie ulichokifanya, wataona kuna mambo unayo na wewe ni hazina kwa Taifa kama alivyosema Dr Slaa. Nanimesikia nia yako ya kuutaka Urais, tunakutakia kila la kheri kwa maslahi mapana ya Taifa.
Alipofika mgeni wao Mhe Joachim Goakh Rais wa Ujeruman, Mwigulu Nchemba ndiye aliyekuwa wa kwanza kuongea, katika maelezo yake Mwigulu alielezea umhimu wa watanzania kujiandikisha watumie vizuri muda uliopo ili kujiandisha na kupigia kura katiba kwani wasipoipigia fedha zote zilizotumika zitakuwa zimepotea na mambo mazuri yalioko kwenye katiba yatakuwa yamepotea. Mwigulu alibainisha changamoto za zoezi hilo na kusema Serikali imechukua hatua na Serikali inauhakika mambo yatakwenda vizuri.
Ndipo Dr Slaa alipopewa nafasi ya kuongea, alimwangia sifa Mwigulu mbele ya Rais wa Ujeruman kuwa nampongeza Mwigulu kwa kazi nzuri anazozifanya na kwa uzalendo wake kwa Taifa hili. Huyu ni kijana mkweli, mzalendo na jasiri, huku Prof Lipumba akimtambulisha kwa Rais huyo kuwa ni Mgombea wa CCM katika uchaguzi ujao. Dr Slaa akamalizia kwa kusema tunakutakia kila la kheri ila utatusumbua (Kicheko). Katika maelezo yake Dr Slaa alishambulia Serikali kuwa inang'ang'ania zoezi la katiba mpya huku tume haina uwezo wa kuandikisha, huku wapinzani hawana imani na tume huku wapinzani hawana imani na katiba iliyokiuka maoni ya wananchi. Kwa upande wake Prof Lipumba alilaani kitendo cha Serikali kutumia Polisi kuwapiga wapinzani na kuwafungulia kesi.
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge Jaku Ayoub amesema Mwigulu muda si mrefu utakuwa mkuu wa Nchi.

Jaku Ayoub ni Mbunge kutoka baraza la wawakilishi, ameyasema leo kipindi cha maswali na majibu Bungeni baada ya Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kujibu swali lake la msingi.

My take: CCM kuweni makini na huyu Kijana.


Huyo mbunge muulize ila kesi yake ya meli iliyo wazamisha watu imemalizika?
 
Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge Jaku Ayoub amesema Mwigulu muda si mrefu utakuwa mkuu wa Nchi.

Jaku Ayoub ni Mbunge kutoka baraza la wawakilishi, ameyasema leo kipindi cha maswali na majibu Bungeni baada ya Naibu waziri wa fedha Mwigulu Nchemba kujibu swali lake la msingi.

My take: CCM kuweni makini na huyu Kijana.
Utabiri kama huu hata mtoto wa darala LA pili anaweza kutabiri.
 
this is the season we will witness most politicians indulging in some playacting.I reward this man a B plus...
 
Back
Top Bottom