Chama cha Mapinduzi Mwaka huu kitamteua
Kada mmoja Mwenye sifa zinazojitosheleza
kuwakilisha Chama hicho kwenye Uchaguzi
Mkuu mwaka huu October, Ili kupambana na
Vyama vingine vya Siasa.
Katika hali ya vuguvugu la kujitangaza Lowassa
na Pinda wameonyesha nia, mmoja katangaza
hadharani kimya kimya na mwingine anafanya
maandalizi ya hali mali kwa kazi hiyo tu.
Chama cha Mapinduzi hakiwezi kuwapa ridhaa
watu hawa wawili kwasababu nyingi zifuatazo:
1. Historia ya Uteuzi ndani ya CCM
inawahukumu. Hakuna Waziri Mkuu au
aliyepata kuwa na cheo hicho amepata kuwa
Rais, isipokuwa Mwl. Nyerere enzi za Uhuru
miaka ya 1960. Waliojaribu siku zote
wameshindwa, Rejea Chaguzi za Mwaka
1985,1995,2005, Malicela,Warioba,Salim,Msuya
na Sumaye. Hawa wote historia za utendaji wao
ziliwatupa nje, haya ni sawa kwa Lowassa na
Pinda.
2. Wote wameingia kwenye Kashfa za Utendaji,
Lowassa alijiuzuru kwa aibu juu ya Sakata la
Richmond Mwaka 2008 ambalo anahusishwa
moja kwa moja na sakata hilo.
Pinda kahusishwa na sakata la Escrow na
Sukari fake na kufoji vibali vya uingizaji wa
sukari kuua Viwanda vya Ndani na kukwepa
kodi. Haya ni MADOA sugu yasiyofutika, CCM
itapata wakati mugumu kuwanadi mmoja Kati
yao.
3. Lowassa kahusishwa kwenye skendo za
ufisadi tangu enzi za Mwinyi,Mkapa na Kikwete,
kuhujumu uchumi wa Chama cha Mapinduzi
kupitia hisa za Vodacom, Sukita na Viwanja,
amejilimbikizia Mali zenye utata, na mwaka
2008 na 2009 alitajwa kuwa ni miongoni mwa
Mafisadi 10 wanaolihujumu Taifa, Pia ana
historia mbaya ya kukataliwa na Nyerere na
amenyooshewa kidole mara kadhaa na Baba wa
Taifa na hili halijapata kufutika kwenye
kumbukumbu.
Pinda kaingia kwenye kashfa ya Utendaji
mbovu, Wananchi na Watalaam wa Mambo ya
Utawala wanamuweka Pinda kwenye Orodha ya
Mawaziri Wakuu Wabovu tangu Uhuru wa Nchi
hii akifuatiwa na Sumaye. Hana uwezo wa
kuitumikia nafasi hiyo kwa maarifa na maamuzi,
madudu mengi yamefanyika chini yake hasa
TAMISEMI, Wizara nyeti za Serikali
zinahujumiwa kwa RUSHWA ya wazi yeye
hachukui hatua. Doa kubwa lisilosahaulika ni
Operation TOKOMEZA ambalo alipaswa
kuwajibika na mpaka Sasa Wananchi
waliothirika hawajalipwa fidia yeye yupo tu.
4. Lowassa anatumia Fedha nyingi kuwanunua
wafanya maamuzi ndani ya Chama chake hasa
Wajumbe wa NEC na sasa ameamua kuanza
kuwalipa Mishahara kabisa kila mwezi ili
amalizane nao kabisa kukwepa TAKUKURU
watakapo kutana Dodoma Mei Mwaka huu,
haya ni sawa na Pinda kupitia mpambe wake
Masaburi wanagawa Dola za Kimarekani ili
kupunguza wingi wa Noti kwa nia ya
kujitengenezea Mazingira ya kukubalika.
Matendo haya ya Lowassa na Pinda
yamekidhalilisha Chama cha Mapinduzi hasa
kipindi hiki ambacho chuki ya Wananchi iko juu
dhidi ya Matendo ya Rushwa,Wizi wa Mali za
Umma na Ufisadi.
CCM itakuwa na wakati mugumu kumnadi
yeyote Kati ya wawili hawa kwa Wananchi.
5. Lowassa na Pinda ni mfano wa kuigwa wa
Viongozi wala Rushwa na wanaotokana na
Rushwa na Wananuka Rushwa kwa Matendo na
Maneno yao. Lowassa akiulizwa swali "Katika
Malengo yako una mpango gani wa kupambana
na Rushwa na Ufisadi?" Hawezi kujibu swali hili
kwani nafsi yake na Historia yake ni zao la
Matendo hayo, yeye Mkubwa wa wala Rushwa.
Pinda kajidhalilisha kwenye Sakata la Escrow
kwa kutetea wahujumu waziwazi, amediliki
kukubali kuwa pesa zote ni za IPTL bila kujali
kodi ya Umma, Recalculation na Mapendekezo
ya Bunge. Mgawo ulivyokuwa wa kutupatupa
haiwezekani Pinda asijue wala kupewa kwenye
mfuko.Majina yaliyoko Stanibic na lake limo.
CCM kumteua mmoja kati ya hawa ni
kuutangazia Umma na Dunia kuwa Tanzania ni
wala Rushwa na CCM ni Chama Cha Mafisadi
na Mfano Mzuri ni Mgombea wao 2015.
6. Pinda na Lowassa hawawezi kushindana na
Ukawa, hawajui kujenga hoja wala kujitetea,
hawana historia ya kufanya siasa za Ushindani
hasa na Mtu kama Dr.Slaa,Lipumba na Zitto.
CCM lazima ipate Kada mwenye uwezo wa
Kujenga hoja, mwenye ushawishi na mzoefu
kwenye majukwaa ushindani na siasa.
7. CCM inahitaji Mgombea ambaye ni kiungo
imara ambaye anaweza kuitetea CCM upande
wa Zanzibar (Pinda SIFA hii Hana) na
anayeweza kuunganisha makundi ya kisiasa na
kidini (Lowassa sifa hii hana,rejea Matamko ya
Viongozi wa dini na leo Jumuiya za Kisilaam).
8. Lowassa ni mtu wa Visasi na amekuwa
kwenye mivutano na Kundi kubwa la Wana CCM
hivyo hawezi kuwa Mwenyekiti wa Chama na
Chama kikasimama ili kuisimamia Serikali,
Pinda kwa udhaifu wake hawezi kuwa
Mwenyekiti wa CCM Chama kitakuwa legelege
na kitakufa, Mifumo ya Chama itasinzia na
kukosa ubunifu.
CCM haiwezi kuwakabidhi Chama watu hawa
wawili
9. Wote wako kundi la Mawaziri Wakuu hivyo
uwepo wa mmoja ni kiama kwa mwingine,
haiwezekani wote wakapendekezwa kwenye
kundi moja, hivyo Pinda na Lowassa ni Fungu la
kukosa.
Maoni ya Wananchi na Wana CCM wanatoa
nafasi kubwa kwa Makada wengine hasa
MWIGULU NCHEMBA
wanajadiliwa kuwa Viongozi wasionuka Ufisadi,
hawana Makundi ndani ya CCM.Mungu ibariki Tanzania.