Mwigulu: Mimi ni Nyerere

Mwigulu: Mimi ni Nyerere

thehunk

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
533
Reaction score
233
Waziri wa fedha, Mwigulu Nchemba asema watu wanamfananisha na hayati baba wa taifa Julius Nyerere kwakuwa anasimamia maswala yenye maslahi kitaifa bila uoga



Nchemba-14Jan2015.jpg

Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
Ni juu ya mbio za urais
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba, ameibuka na mpya baada ya kujifananisha kwamba yeye ni sawa na Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere na aliyekuwa Waziri Mkuu, hayati Edward Sokoine, kwa madai ya kuwa na misimamo isiyoyumba katika masuala yenye maslahi kwa taifa.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, aliyasema hayo juzi wakati akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na kituo cha televisheni cha ITV, ambapo alizungumza mambo mbalimbali, likiwamo suala la uchotwaji wa zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow, iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Alisema suala la yeye kuitwa Sokoine, halijaanza leo, kwani hata alipokuwa anasoma, alikuwa akiitwa mara Nyerere au Sokoine, hasa kutokana na misimamo yake isiyoyumba, hususan katika masuala yenye maslahi kwa taifa.

"Ukicheza kama (Christian) Ronaldo ukapiga chenga kama Ronaldo, watakwita Ronaldo. Majina wanayoniita ni ya watu maarufu waliokuwa wakisimama katika haki ili kutetea haki za wanyonge," alisema.

Alisema viongozi waliopewa uongozi wana wajibu mkubwa wa kutetea haki za wanyonge, kwani wapo watu, ambao hawana fursa ya kusema na jambo hilo likiachwa kuna siku mawe yatasema na haijulikani nini kitakachotokea.

URAIS 2015
Akijibu swali lini atatangaza kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Mwigulu, ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), alisema yupo katika Chama kwa ajili ya kusimamia misingi na miiko ya Chama, hivyo hawezi kuwa miongoni mwa wanaoivunja.

"Mimi nipo kwenye Chama. Nimepewa jukumu la kusimamia miiko na misingi ya Chama. Hivyo, nisingependa niwe miongoni mwa wanaovunja miiko. Tutavuka mto. Tukishavuka, tutaangalia," alisema Mwigulu.

Kuhusu maagizo yanayotolewa na Katibu Mkuu wa CCM kwa watendaji wa serikali, alisema kwa utaratibu wa uendeshaji wa serikali ndani ya mfumo wa vyama vingi, Chama ndicho kinachoisimamia serikali.

"Sasa hivi tunakwenda kwenye uchaguzi. Watakaokwenda kuomba kura kwa wananchi ni wana-CCM siyo wataalam ama katibu mkuu wa wizara ndiyo atakwenda kufanya kampeni, hapana, ni chama," alisema Mwigulu.

WALA RUSHWA WAFILISIWE
Alisema kuna haja kwa watumishi wa serikali au viongozi wanaobainika kula rushwa wawe wanafilisiwa mali zao, kupelekwa mahakamani na wasiwe wanapewa dhamana hadi siku ya hukumu.

"Inatakiwa ijulikane mtu akila rushwa na kugundulika kwanza fedha hiyo airudishe, afilisiwe na kufikishwa mahakamani na kusiwe na dhamana mpaka siku hukumu itakapotolewa," alisema Mwigulu.
Alisema kama utaratibu huo utawekwa, watu wataogopa kuiba au kula rushwa, lakini inapokuwapo sheria na haki zaidi kumlinda mtu, ambaye anaibia wenzake, inakuwa ni tatizo.

"Siyo mtu amepoteza au amesababisha hasara ya Sh. milioni tatu halafu mnashusha nguvu mnatumia Sh. milioni moja kumshughulikia, halafu aliyefuja Sh. milioni 20 anashushwa cheo tu kwa kigezo cha utawala bora ama utawala wa sheria, hapana," alisema Mwigulu.

Alisema ni jambo la kushukuru kwa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais Jakaya Kikwete, kuanzisha taasisi kama ile ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), ambayo ina jukumu la kushughulikia vitendo vya rushwa.

Mwigulu alisema Tanzania ijayo inatakiwa ijengwe kwenye misingi ili kila mtu ajipime kama anatosha kwa uadilifu, kwani hata nchi zilizoendelea zimefanikiwa kutokana na kujiwekea misingi yake.

Alisema haiwezekani kuwa na utawala bora au haki za binadamu zinazolinda raia wanaonewa walio wengi na kulinda wanaoibia wengine.

Mwigulu alisema Watanzania lazima watambue kuwa mtu akiiba au kupoteza fedha za umma, anakuwa amesababisha watu wengine kufa kwa kukosa dawa hospitalini au akina mama wajawazito kukosa huduma.

Alisema mazingira haya yanakuwa yametengezwa na mtu, ambaye hakutimiza wajibu wake.

"Huwezi ukawa na haki ya binadamu ama utawala bora bila kuchuckua hatua. Ni lazima kuwalinda na wanaoonewa. Haiwezekani kwa mfano, mtu anapoteza Sh. bilioni 20 halafu adhabu kubwa anayopata anaondolewa cheo tu au kuhamishwa kituo cha kazi. Hii ni sawa na kumpa likizo akatumie fedha alizochukua," alisema Mwigulu.

Alisema awamu ya nne imefanikiwa kuweka uwazi katika suala la hesabu kwenye mapato na matumizi ya fedha za umma na hivyo, awamu ya tano ijayo inapaswa kuanza kuwashughulikia watu wanaofuja fedha ili kujenga nidhamu katika matumizi ya fedha za umma.

"Siyo tu kwamba, ni fedha za wahisani kwamba, ndiyo tutumie vizuri. Huko tunakokwenda fedha yoyote inatakiwa itumike kwa uadilifu ili kuwafanya walipakodi waone kodi wanayoitoa inatumika kwa malengo yaliyokusudiwa," alisema Mwigulu.

Alisema mtu akilipa kodi ya umeme aone umeme, atakuwa na moyo wa kulipa na hakutakuwa na suala la kukimbizana kuhusu kulipa kodi.

"Lakini mtu akilipa kodi akaona yeye anaendelea kuwa maskini na kuna ngazi au viongozi waliopo madarakani wananeemeka na familia zao, inavunja moyo wa kulipa kodi," alisema Mwigulu.

KASHFA YA ESCROW
Alisema Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeshawafanyia mahesabu ya kodi wanayopaswa kulipa kwa serikali wote waliopata mgawo wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow na kwamba, ni lazima italipwa na siyo jambo la mjadala.

"Lazima tajiri alipe kodi ili tuweze kusomesha maskini. Hatuwezi kusamehe kodi kubwa namna ile halafu tukakimbizana na mama mjane anayeuza mchicha," alisema Mwigulu.

Alisema katika dhamana ya utumishi, kila mmoja anabeba yake kwa sababu amesomeshwa na kodi ya serikali na kuaminiwa na taifa, hivyo haiwezekani afanye kosa halafu adhabu aibebe balozi wa CCM.

CHANZO: NIPASHE
 
Waziri wa fedha mh mwigulu nchemba asema watu wanamfananisha na hayati baba wa taifa julius nyerer kwakuwa anasimamia maswala yenye maslahi kitaifa bila uoga

weka source..
usikute unamzushia.
 
Sasa tunamtaka aanze kushugulikia matumizi makubwa ya serekali. Atangaze kuondoa ma V8 yote serekalini ayapige mnada na awake code na standard ya magari ya viongozi na serekali kwa ujumla. Hapa ndipo atakuwa amecheza Messi na sio Ronaldo tena, na uraisi tutampa bila hata kugombea.

Wenzetu Kenya na Rwanda wameweza, kwanini Tz tusiweze? Magari ya serekali na viongozi wake isizidi cc 2000 full stop.

Mwigulu if you are serious go with this utakuwa raisi hata bila kugombea, just try my advice my friend, you will see.
 
Mkuu,

Unafahamu maana ya kuendekeza?

Hiyo heading yako ni majanga.

Jaribu kuwaomba MOD's wakusaidie kuiweka vizuri.

Halafu kampeni zenu kuhusu ''kumfagilia'' Mwigulu Nchemba niza kitoto sana.

Niliwashauri kama kweli mko serious mtafute wataalam wa PR ili wawasaidie kuwashauari katika maeneo mnayoonekana mna mapungufu.

Hoja zenu kila siku ni zile zile lakini kubwa zaidi, haziwezi kujenga mazingira mazuri kwake ili apigiwe kura nyingi na wajumbe wa mkutano Mkuu wa CCM Taifa.

Unapowaambia wazee wa CCM ambao ndiyo wengi kwenye mkutano Mkuu wa CCM kuwa huyu ni mfano wa Mwl. Nyerere au Sokoine wakati hao wazee walifanya kazi pamoja na hao viongozi, kwanza watakushangaa, halafu watakudharau.

Hizi hoja zinawafaa vijana ambao hawakubahatika kumuona Mwl. Nyerere au Sokoine akifanya kazi na siyo wake walifanya kazi nao.

Ni ushauri tu.
 
mkuu haya maneno yangezungumzwa mwanzoni 2010 hadi 2013 ni sawa ila sasa 2015 yananitia shaka sana huu ni mwaka wa uchaguzi watakuja wengi wakizungumza matatizo ya wananchi ila ikifika mwaka kesho watayasahau
 
nlizima tv alipoongea haya itv juzi-toka mtoto naitwa nyerere nilikuwa na misimamo duuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu!
 
waziri wa fedha, mwigulu nchemba asema watu wanamfananisha na hayati baba wa taifa julius nyerere kwakuwa anasimamia maswala yenye maslahi kitaifa bila uoga




chanzo: nipashe

haya nyerere wa ccm ya kasi mpya
 
Nyerere hakuwa Gaidi, inashangaza Gaidi kujifananisha na mzalendo wa kweli nchi hii kuliko hata Nyerere, yaani Edward Moringe Sokoine (Mtu wa Watu)
 
ok sawa ila amefanya jitihada gani kuhakikisha audilifu kwenye chama chake?
 
asisjifanye tumeshasahau kwamba yeye ndiye amekuwa mchotaji mkuu hazina kuingiza mafisadi madarakani kwa tiketi ya CCM
 
Huyu Mwigulu huo utetezi wa wanyonge anaojivika ameanza mwaka Jana mwishoni tu, hivyo uko strategically, Wala sio tabia yake ya kuzaliwa nayo.

Nyuma ya hapo alikua mpiga vijembe tu, pamoja na kuratibu matukio mbalimbali against viongozi na mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani yanayotia Shaka.

Hata ukiangalia anachodai kutetea wanyonge ni kama amekariri tu, yaani kila siku story ni hizo hizo sijui kukimbizana na mama ntilie, wamachinga, e.t.c. na amekua akitaja tu kila mara hizi story lakini utekelezaji hakuna. Angekua ni mtekelezaji kweli tungeshaona mabadiliko.

Kingine analazimisha watu wamkubali kwa kutumia wapambe wake wamuandike kama hapa kwenye huu Uzi. Wanaomkubali ni wachache na ni watu wake, na ndio wanaolazimisha wengine tumkubali
 
Tangu lini Mwigulu kawa Waziri wa fedha? Hebu nijuzeni.
 
Juzi nilikua safarini, nilipopita pale Ruvu kuelekea Chalinze kuna daraja ambapo treni inapita juu, kuangalia juu ya ukingo wa lile daraja kuna Mpuuzi kaandika MWIGULU NDIO RAIS 2015. Nikacheka tu maana huyu jamaa ana ndoto za ajabu mno.......na huku ni kuchafua mazingira yetu, huwezi kuandika ujinga kama huu kila mahali. I hate it.
MANI zumbemkuu Chakaza tpaul na wengine huyu kijana ni mzima kweli? lusungo pale ni Vigwaza au ni Ruvu? Kumbe na wewe uliona ule upuuzi eeeh??
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom