Hongera sana mtoa taarifa, Hii taarifa imepokelewa. Na achana nao wote baadhi ya matahila wanaokubeza.
Tena kwa kauli nyepesi katika jambo zito kama hili. Nadiliki kuwaita matahila kwa hoja zao zao dharimu na dhaifu. licha ya kwamba wameona hadi ushahidi wa picha.
Mfano: mtu anaposema eti kila siku unawatuhumu polisi wetu, huyu akili yake iko timamu au ni uji mtupu? Kwani hoja hii ameona ikilipotiwa katika mtiririko upi hadi kujenga hoja ya kila siku? Nonses.
Si hilo tu. bali juha mwingine, anaetumia lugha eti acha upuuzi wa kulituhumu jeshi polisi angali mtoa maada ameonyesha hadi taarifa za masikitiko makubwa kuwa kupitia ajali hiyo tumepoteza askari. Harafu unaita kuwa hiyo ni taarifa ya kipuuzi?
Huna hoja ya kuchangia kaa kimya.
Hizi zama sio za blabla ama ubabaishaji wa kurahisisha mambo hasa unapokuja katika maisha ya watu.
Ni wakati wa kuheshimu sheria bila kujali ukubwa ama udogo wa sheria hiyo husika.
Kuanzia kwa raia hadi mamlaka mbalimbali za umma ni wajibu na haki yetu, kuhakikisha kwamba sote tupo chini na si juu ya sheria.
Pia hii izangatiwe kuwa hii ni taarifa, na si hukumu kwa jeshi la polisi.
Kwani tunatambua sote umhimu wa jeshi la polisi na ugumu wa majukumu, hususani wale wote waadirifu na Wazalendo wa taifa lao, Pamoja na wanaotekeleza majukumu yao kwa mjibu wa tarabu na sheria za nchi.
.........,.............