Mwigulu, billion 10 za Mishahara ya walimu zipo wapi?

Mwigulu, billion 10 za Mishahara ya walimu zipo wapi?

mwinukai

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2011
Posts
1,447
Reaction score
630
Mh. Mwigulu akilulizwa swali na Mbunge wa Tabora mjini siku ya tarehe 4/6/2015 kuhusiana na walimu wapya ambao hawajapata mishahara yao.

Mh. alijibu kuwa amewaagiza hazina na wao wameshatuma billioni kumi kwa ajili ya mishahara, lakini cha ajabu mpaka sasa walimu walioanza kuripoti tarehe 1/5/2015, hawajapata mishahara yao, hawajalipwa stahili zao ikiwamo nauli na fedha za kujikimu, ukingatia wako maeneo ya ugenini kwa hapa Serikali inategemea wataishije ?

Je ile ahadi yako Mh. Mwigulu imeishia wapi ukizingatia tulijiaminisha kuwa wewe ni mtetezi wa wanyonge?
 
Mh. Mwigulu akilulizwa swali na Mbunge wa Tabora mjini siku ya tarehe 4/6/2015 kuhusiana na walimu wapya ambao hawajapata mishahara yao Mh. alijibu kuwa amewaagiza hazina na wao wameshatuma billioni kumi kwa ajili ya mishahara, lakini cha ajabu mpaka sasa walimu walioanza kuripoti tarehe 1/5/2015 wengi wao, hawajapata mishahara yao, hawajalipwa stahili zao ikiwamo nauli na fedha za kujikimu, ukingatia wako maeneo ya ugenini kwa hapa Serikali inategemea wataishije ? Je ile ahadi yako Mh. Mwigulu imeishia wapi ukizingatia tulijiaminisha kuwa wewe ni mtetezi wa wanyonge?
 
Hana jibu maana ni mnyama asiye na meno..!! Mkuya ndio aulizwe!
 
Yuko busy na kutafuta urais. Nyie shauri yenu. Ndipo mjue kama ndani ya Ccm hamna msema kweli hata mmoja.
 
Sijawahi ona wamefanya jambo kwa mafanikio!
 
Hata mkiwapa miaka mingine mia, vinyo ni ileile!
 
Shida nimeshuhudia walimu wakipiga lampard.... Hawajapata hata ya kujikimu
 
Hii kauli imejaa utata, hazina alimuagiza nani? Huyu naye anataka kuwa Rais wakati wizara ya fedha nanga inapaa!

Mh. Mwigulu akilulizwa swali na Mbunge wa Tabora mjini siku ya tarehe 4/6/2015 kuhusiana na walimu wapya ambao hawajapata mishahara yao Mh. alijibu kuwa amewaagiza hazina na wao wameshatuma billioni kumi kwa ajili ya mishahara, lakini cha ajabu mpaka sasa walimu walioanza kuripoti tarehe 1/5/2015 wengi wao, hawajapata mishahara yao, hawajalipwa stahili zao ikiwamo nauli na fedha za kujikimu, ukingatia wako maeneo ya ugenini kwa hapa Serikali inategemea wataishije ? Je ile ahadi yako Mh. Mwigulu imeishia wapi ukizingatia tulijiaminisha kuwa wewe ni mtetezi wa wanyonge?
 
Hii kauli imejaa utata, hazina alimuagiza nani? Huyu naye anataka kuwa Rais wakati wizara ya fedha nanga inapaa!

Hata hivyo, si alijiuzuru nafasi ya unaibu waziri? ama ilikuwa ni lugha ya kutafuta kura za urais?
 
Sio Walimu tu, kuna wfanyakazi wa miaka mingi wa idara na Taasisi za serikali hawana mishahara tangu mwezi December 2014.

Mwigulu alianzisha mfumo wa kulipa wafanyakazi wa serikali kupitia HAZINA NA UTUMISHI ambapo mishahara ya wafanyakazi inakwenda moja kwa moja katika account zao.

Wakati wa kuigiza wafanyakazi katika mfumo huo wa LAWSON kuna baadhi ya wafanyakazi hawakuingizwa. Aidha kuna baadhi ya wafanyakazi mishahara yao ilikosewa kwa kuingizwa kidogo.

Tangu wakati huo kuna wafanyakazi ambao hawajapata mishahara na Mwigulu aliyekuwa champion wa mfumo huo wa lawson ameshindwa kulipatia ufumbuzi tatizo hilo.

Aidha kuna wafanyakazi tangia wakati huo wanapata mishahara pungufu tofauti na sitahiki yao. Mwigulu analifahamu tatizo hili kwasababu ameafanya mazungumzo mara nyingi na vyama vya wafanyakazi na waajiri wa idara na Taasisi za serikali kuhusu kasoro hizo. Lakini jibu lake limekuwa lile lile kwamba mwezi huu kasoro hizo zitatuliwa lakini leo ni miezi 6 na bado kasoro hizo hazijatatuliwa na wafanyakazi wanaendelea kuteseka.
 
Back
Top Bottom