Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,901
- 20,416
Sasa Mwigulu anachangia bajeti ya Makamu wa Rais Muungano. Anasema kuwa anachofanya Lissu ni jitihada zake za kuwafitinisha Wazanzibari baada ya kushindwa kuwachonganisha Watanzania Bara. Anasema kuwa wakati mwingina anaona aibu kujitambulisha kuwa anatoka Singida kutokana na matendo ya Tundu Lissu. Anasema kuwa Lissu ameongea mambo mengi ambayo hana takwimu wala hakika yake. Anawashangaa Wazanzibari kwa kufurahia hotuba ya Lissu huku wanajua kuwa anafanya jitihada za kuwagombanisha. Anasema kuwa mambo yakiharibika watakaoumia ni Wazanzibari huku Lissu akifurahia kwake Singida.