Kada mahiri wa CCM na kipenzi cha Watanzania Mwigulu Nchemba yupo kwenye mikakati mizito ya kuisambaratisha CHADEMA na Kuirudisha Heshima ya Chama Kubwa CCM katika medani za siasa Tanzania. Akiwa katika mapumziko mazito amesema sasa umefika muda muafaka wa kuwajulisha Watanzania nini kipo nyuma ya Chadema amesema watanzania wakae mkao wa kushangilia ushindi.
Aidha amesema ana mpango wa kuwapumzisha vijana wawili ambao wanaonekana ni mamluki kutoka CHADEMA kwani hawakubaliki katika siasa za majukwani na wapenzi wengi wa ccm hasa vijana wa Green guard wanawachukia sana. amesema atakuja na kikosi kipya kilicholelewa na kukulia ndani ya ccm kupitia chipukizi za CCM. amesema vijana hao wawili waliokuwa wanachama na viongozi wa Bavicha ni mzigo kwa chama kwani kila wanapopita huzomewa na hawana uwezo wa kufanya siasa za majukwani.
Mwigulu amesema baada ya mapumziko anayokaribia kuyamaliza atafanya mkutano mkubwa wa hadhara katika mikoa ya kanda ya ziwa na kusini.