mapambanodaima
Senior Member
- Oct 22, 2012
- 108
- 15
Wanajamvi, kale kamchezo ka Mwigulu kujiona yupo juu ya sheria na kutoa rushwa kila kona ya Iramba imemtokea puani baada ya kukamatwa na kuhojiwa na Takukuru kwa muda wa zaidi ya masaa matatu.
Wagombea wenzake walijitoa katika kinyang'anyiro tangu tarehe 25 kwa madai ya kufanyiwa rafu hizo na kutoa malalamiko yao huku wakisubiri suala hilo kushughulikiwa ndipo warejee kwenye kampeni.
===========================
Wagombea wenzake walijitoa katika kinyang'anyiro tangu tarehe 25 kwa madai ya kufanyiwa rafu hizo na kutoa malalamiko yao huku wakisubiri suala hilo kushughulikiwa ndipo warejee kwenye kampeni.
===========================
Chanzo: ITV
Ofisi ya Takukuru mkoani Singida imemuhoji kwa masaa kadhaa naibu waziri wa fedha na aliye kuwa mbunge wa Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba, kwa tuhuma za kukiuka sheria ya garama ya uchaguzi na sheria ya kuzui na kupambana na rushwa.
Akiongea na waandishi wa habari mkuu wa Takukuru mkoani Singida Bwana Joshua Msuya amesema Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amekiuka sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 katika zoezi linalo ndelea la kura za maoni ndini ya vyama vya siasa.
Katika hatua nyingine Bwana Msuya amewatahadharisha wagombea wote wa ngaza mbalimbali watakae jihushisha na kutoa rushwa iwe ya fedha au vitu,vifaa vya michezo, madawati watakuwa wamekiuka sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11/2007 na sheria ya uchaguzi cap.343 r.e 2002 na pia sheria ya garama za uchaguzi namba 6/2010.
Katika jimbo la Singida kaskazini wa tia nia saba ambao wanagombea ubunge kwa tiketi ya CCM, wametishia kujitoa katika kinyanganyiri hicho kufuatia msimamizi wa uchaguzi kumwachia mgombea mwenzao ambaye ndiye mbunge wa jimbo hilo kuto kufuata masharati ya sheria za uchaguzi jambo ambalo limekuwa kero hadi kutumia vijana wa shule kuonyesha vipeperushi vyake wakati wa mkutano wa kujinadi.
ITV haikuishi hapa ilifanya juhudi za kumwona kaimu katibu wa CCM mkoa wa Singida ambaye ndiye msimamizi mkuu wa mkoa Bwana Aluu Segamba, amekiri kuwepo kwa matatizo hayo na kuchukuwa jukumu la kumbadilisha msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo na kumweka mwingine.
Baadhi ya majimbo ya uchaguzi yenye wabunge ambao wameamua kutia nia ya kugombea tena wamekuwa wakioneka wao ni chanzo kimoja wapo kikubwa cha kuvunja mashariti ya uchaguzi na kuwasababishia wenzao kuwa na malalamiko mengi,hadi kufikia hatua ya kuiomba serekali kupeleka maafisa wa takukuru na polisi kwenye mikutano ya kujinadi kugombea ubunge.
Mwigulu aibuka na kuipongeza TAKUKURU
SIKU chache tu baada ya Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa hapa nchini (TAKUKURU )Mkoa wa Singida kumhoji aNaibu Waziri wa Fedha na Mgombea ubunge Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba, yeye ameibuka na kuipongeza taasisi hiyo kwamba imetimiza wajibu wake ipasavyo kisheria.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mwigulu alisema kitendo kilichofanywa na TAKUKURU ni sehemu ya kutimiza wajibu wao na yeye kama kiongozi wa serikali amesifu hatua hiyo.
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimekuwa mstari wa mbele katika kupambana na rushwa hapa nchini, hivyo sioni sababu ya kutoa rushwa, na sio kawaida yangu kufanya hivyo, kwani kazi yangu niliyoifanya katika Jimbo hili inaonekana na nina uhakika wa robo tatuya wananchi wananikubali , sasa nitoe rushwa ya nini. alihoji Mwigulu.
Hili ni jambo jema kwa TAKUKURU kufanya na isiwe kwa Iramba tu na maeneo mengine ambako wana mashaka kwamba kuna vitendo vya rushwa vinafanyika na nendei na huko hii ndiyo kazi ya serikali katika kuhakikisha wale wote wanaokiuka kanuni na taratibu za uchaguzi waweze kushughulikiwa ipasavyo ..alisisitiza.
Aidha alisema katika mchakato wowote wa uchaguzi ni lazima kuwepo na changamoto mbalimbali hivyo kwa haya mambo mengine ambayo wenzake wanalalamikia ni yale ambayo kimsingi walikubaliana kwenye vikao vya kamati ya siasa ya chama Julai 19 mwaka huu kabla ya kuanza mchakato huo.
Mfano tulikubaliana akwenye kikao tuwe na gari moja kila mgombea kwa ajili ya matangazo , mimi la kwangu limewazidi ni fuso lakini wao wana Canter na zina spika , sasa kama langu limewazidi hiyo siyo hoja ni mambo tuliyokubaliana wenyewe wasiwe na hofu tuendelee na mchakato, mwisho wa siku wapiga kura ndio wataamua kwani mfa maji haishi kutapatapa, hizi ni homa za uchaguzi tu.Alisema.
Katika hatua nyingine viongozi wa CCM Wilaya ya Iramba waliokuwa wakilalamikiwa na wagombea watatu Davd Jairo, Juma Killimbah na Amon Gyunda kwa madai ya kumbeba Mwigulu kwenye kinyanganyiro cha kura za maoni Wilayani humo, wameondolewa kuendelea na mchakato huo na kamati ya siasa ya Mkoa ili kuweka mambo sawasawa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Mary Maziku alisema kuwa baada ya kukaa kamati ya siasa wamekubaliana kuwa viongozi hao waondolewe katika mchakato huo ili kuondoa manunguniko hayo, baada yab kutishia kugoma kuendelea zoezi hilo.
Alitaja viongozi hao kuwa ni Katibu wa CCM Wilaya ya Iramba, Mathias Shidagisha, Katibu msaidizi Fafael Mwita, Katibu wa (UVCCM) Wilaya Abel Makala na Katibu wa Wazazi Wilaya hiyo, Halima Magolanga.
Nimefanya maamuzi kuwa katika msafara wa hawa wagombea kuwepo na magari yao matatu pia liwepo gari moja la chama na gari moja kwa ajili ya tahadhari.Alifafanua Maziku.
Aidha alisema baada ya kufanya maamuzi hayo wagombea wote wamekuwa kitu kimoja na wanaendelea na mchakato kama kawaida, hukukamati ya siasa ya Mkoa ikiwateua Khatibu Ally na Mwanaidi Kalegea kushika nyadhifa za viongozi walioondolewa na kurudishwa makao makuu wa CCM.