Mwigulu adai wananchi ndio walioshauri tuweke tozo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
120,811
226,656
Waziri wa Fedha Mh Mwigulu akizungumza na Waandishi wa habari amesema kwamba Wananchi wenyewe ndio walioshauri serikali iweke Tozo ili kupanua wigo wa mapato , na kwamba ilichofanya serikali ni kuufanyia kazi ushauri wa Wananchi.
---

1718988746858.jpeg
Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema wananchi ndio walioshauri Serikali ipanue wigo wa tozo za miamala kwa kujumuisha miamala yote ya kielektroniki, ili wananchi wote wachangie maendeleo. Ameeleza kuwa awali miamala iliyokuwa ikitozwa ni iliyokuwa ikifanyika kwa simu pekee.

Chanzo: SwahiliTimes
 
Waziri wa Fedha Mh Mwigulu akizungumza na Waandishi wa habari amesema kwamba Wananchi wenyewe ndio walioshauri serikali iweke Tozo ili kupanua wigo wa mapato , na kwamba ilichofanya serikali ni kuufanyia kazi ushauri wa Wananchi .

Chanzo : SwahiliTimes
Wananchi tunaiahauri serikali kuacha kuibeba CCM ktk chaguzi kuu, naomba na hili lishughulikiwe kwa sababu serikali sikivu inawasikiliza wananchi

Huyu waziri anafaa kwenye comedy zaidi
 
jInga sn, kama walishauri mbona wanalalamika sasa?
Kweli sisi wananchi wajinga kama alivyosema kiongozi wa upinzani yaani tumependekeza tozo wenyewe


Halafu tuje tulalamike huu ni ujinga kwekikweli!

Waziri atuambie wananchi wangapi walipendekeza Kati ya wangapi unaweza kuta wananchi wenyewe ni mawaziri na wafuasi tu.

Mambo ya wote tuwe wote, tozo iliyopendekezwa bungeni ni za simu wa siyo za kibenki
sawa lakini hii nchi tumechelewa sana kimaendeleo sasa sijui kulinganisha na nani
 
Hayo maoni ya wananchi waliyakusanya lini na kwa njia gani?

Aache uongo, hizo tozo zimepitishwa na lile bunge la CCM lisiloweza kuihoji chochote serikali kisha Rais akaweka saini.
Shirika LA TWAWEZA ndo lilifanya research
 
Back
Top Bottom