Mwigulu achafua hewa bungeni na kuzua miguno

Mwigulu achafua hewa bungeni na kuzua miguno

Status
Not open for further replies.
Kupuuzwa ndio jawabu sahihi kwa watu wa aina yako.
 
damu ya watu mliouwa iringa, morogoro, singida na arusha itawatafuna mpaka siku mnaenda kaburini. hongera mwigulu kwa kuyaumbua haya manyang'au


Labda kama unataka kusema kuwa serikali imeshindwa kazi.

Kama walimkamata Lwakatare kwa video ya You tube ............... Wameshindwaje kuwakamata watuhumiwa kwenye tukio lililotokea mbele ya Askari zaidi ya 100. Halafu Naibu Katibu Mkuu wa chama Tawala anakwenda kuliomba Bunge liwakamate. Hiyo kweli ni kazi ya Bunge??

CCM kazi imewashinda .................. irudisheni serikali kwa wananchi!!
 
KIMENUKA BUNGENI,MH.MWIGULU NCHEMBA AWALIPUA MBOWE NA DR.SLAA KWA MAUAJI YA NDAGO,IRINGA,ARUSHA NA MOROGORO
9k=

ANAPIGILIA MSUMARI KWA KUSEMA "JELA NDIO WANAKOSTAHILI MBOWE NA DR.SLAA "
MBOWE AINAINAMISHA KICHWA CHINI BAADA YA MWIGULU KUMLIPUA,
chadema-mnyika1.jpg
Ni kiongozi jasiri,ni kiongozi mzalendo,nikijana shupavu,amejitolea kuipigania Tanzania ya kweli,amejitolea kupambana na wahujumu wa nchi popote pale Tanzania,Ni Mh.Mwigulu lameck Nchemba leo tena anafanya kile CHADEMA wapata maumivu yasiyonakifani,Mwigulu nchemba amewalipua kisawa sawa Vioongozi wa CHADEMA wa juu wakiongozwa na Freeman aikael Mbowe na Dr.slaa kuhusika na umwagaji damu za Watanzania wasio na hatia.Ni siku leo asubuhi kwenye kipindi cha Maswali na majibu,Mh.Mwigulu Nchemba akitoa swali la nyongeza anasema "Ndani ya miaka miwili CHADEMA wakiongozwa na Freeman Mbowe na Dr.slaa wamesababisha vifo Arusha,Ndago,Morogopro na Iringa.Kwa mauaji haya yaliyotokana na ukatili wao na kutojali maisha ya watu kwa viongozi hawa wa CHADEMA.Mbowe na Slaa wanastahili kuwa JELA na walistahili kuwa jela siku nyingi".Anasema Mbunge wa Iramba Magharibi.Baada ya kauli hiyo Ukumbi wa bunge unalindima kwa makofi mazito.Huku upande wa CHADEMA kila mmoja akiishia kukunja sura.
images


Safi sana Mwigulu Nchemba,mbona watakukoma sana hawa CHADEMA na mwaka 2015 ndio kabisa kwisha habari yao.
images

Kama wanastahili kuwa Jela, lakini wapo nje na wanapeta, Mh Mwigulu anahalalisha kauli ya Mh Mnyika aliposema "serikali hii ni legelege". Mwigulu kama top 10 wa CCM, serikali hii inafuata Dira ya CCM, Mwigulu ameshindwa nini kuisimamia serikali hii kuwasweka Jela Mbowe na Slaa? Hii habari sawa na zile hadithi za Abunuwasi "anakata tawi, wakati amelikalia kuti hilohilo"
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Goog good goog goog very goog mwigulu, watakoma
 
Kwa hili la Mwigulu na ChademAa huko BUNGENI limewafumbua Wananchi kiasi kikubwa, niko hapa Kinondoni watu wanasema Chadema haiwezi kushinda 2015 hata wafanyeje, maana ubaguzi na hila za kujilipua zinawaogopesha wananchi.

kumbe ndo uko kiofisi cha CCM hapo na magamba wenzio, yule mnene ni Tambwe Hiza! Nimepita barabarani na RAV 4 nyekundu
 
Ukijibizana na mjinga na wewe utaonekana mjinga.
Achaneni na huyo savimbi, anataka kutengeneza headlines ili watu watoke kwenye mada ya msingi.
Sasa hivi kuna katiba na mambo mengine, tu concetrate on those issues.
Ndio maana anaongelea huo ukichaaa wake bungeni tu, akijua hawezi kuitwa mahakamani!
 
Hii nchi inasikitisha sana, kama wanasiasa na viongozi na vijana kama akina Mwigulu, wanashinda kueneza siasa za chuki baina ya Watanzania na Watanzania na baathi ya watu wanachekelea ni aibu sana,
Wakati wenzetu Wakenya , Warwanda na Waganda wanaungana kwa maslahi ya nchi zao na Wakiitenga Tanzania, sisi tutabaki na nani soon Malawi hatutokua nao na Wanzambia wana plan kutubia Beira Port.
Angalizo: tuache siasa za chuki kwa maslahi ya vizazi vijazo na tuwe PROUD na nchi yetu kama Wakenya linapokuja suala la maslahi ya nchi yetu,
 
Watu wanafanya, halafu wanasema wengine. Hii dunia ni mbaya sana.
 

Attachments

  • 7 Nape na viongozi waliompokea wakiwasili kwenye kambi ya Baraza la Vijana wilaya ya Missenyi.jpg
    7 Nape na viongozi waliompokea wakiwasili kwenye kambi ya Baraza la Vijana wilaya ya Missenyi.jpg
    23.1 KB · Views: 84
Naibu katibu mkuu wa CCM bara Mwingulu Nchemba akiuliza swali la nyongeza kwa waziri ofisi ya rais utawala bora Mkuchika amesema ni kwa nini viongozi ambao wamesababisha vifo vya watu huko Singida, Arusha akiwataja viongozi wakuu wa CHADEMA; Mheshimiwa Mbowe na Slaa kuwa wafungwe ndio wamesababisha vifo hivyo.

Kama kweli huyu ndio kiongozi wa CCM basi wamekosea kumpatia hiyo nafasi kubwa na adimu ni hivi karibuni tu mahakama ya mkoa wa Singida imetoa hukumu ya kesi iliyokuwa inawakabili viongozi wa Chadema mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar Kitila Mkumbo na Mwita Waitara kuwa hawana kesi ya kujibu kutokana na huyo nchemba kushindwa kufika mahakamani.

Na pia huku Arusha tume ya haki za binadamu na utawala bora wamekwisha toa taarifa yao na kuituhumu serikali kuwa ilitumia nguvu kubwa na polisi walituhumiwa kuua.

Alianza kwa kujiita "Adam Smith of Tanzania"; mkali wa uchumi mwenye masters degree with honours; baadaye akajipachika vyeo vya DPP na DCI; likapita sasa ameongeza tena kuwa Judge, prosecutor and Jury!! hivi kweli Tanzania inahitaji such a man; a jack of all trades BUT a master of nothing!!!
 
nimeamini Mwigulu Nchemba kaanza kuchanganyikiwa kabisa, yani pamoja na kupata nafasi ya kuwa mbunge bado fikra zake ziko chini kabisa na anafikiri watu wanafungwa kwa maneno tuuu.

Kumbe ndio maana huwa wanawalazimisha watu kuwataja mbowe na Slaa.
 
Last edited by a moderator:
nimeamini Mwigulu Nchemba kaanza kuchanganyikiwa kabisa, yani pamoja na kupata nafasi ya kuwa mbunge bado fikra zake ziko chini kabisa na anafikiri watu wanafungwa kwa maneno tuuu.

Kumbe ndio maana huwa wanawalazimisha watu kuwataja mbowe na Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Hii nchi kazi kweli kweli yaani huyu ndio kiongozi mtegemewa wa ccm? Acheni masihara tuleteeni kiongozi mwingine maana kwa wenye akili wanazidi kukishangaa chama. Halafu watu wengine wanashabikia la? Hatuna dawa hospitalini, elimu ya kuunga unga walimu tatizo kila kukicha bora jana halafu anakuja na habari za kitoto namna hii? Kweli akili ndogo inaongoza akili kubwa.
 
He who goes with feaces on his buttocks must be prepared to dance with flies..
 
nawapa pole wananchi wa jimbo lake anafikiri mahakama ni kama ofisi za Lumumba naona anataka kurithi mikoba ya DPP
 
Mwigulu ni nani siyo swali.ugonjwa anaoumwa utawapeleka wapi wanaomruhusu kufanya maamuzi na kuwasemea ndiyo swali langu.mwigulu nijibu,kwa nini hutaki kwenda kliniki?huumwi kichwa/hujisikii watu hawakupendi?hujisikii kama usalama umepungua?hujifikiriii kama una akili nyingi kuliko watu wa aina yako wote?kama majibu yako ni ndiyo katika swali lolote,nakushauri uende hospitalini,elezea dalili watakusaidia uonane na daktari bingwa!kuna eneo la afya hujakaa sawasawa!mwenye kigoda wetu chichiemu tafadhali,huyu mdogo wangu anahitaji tiba!
 
kuna watu huko Igunga walimpigia kura! kweli ujinga ndio mtaji wa C.C.M
 
Siku zote nimekuwa niaamini chanzo cha umasikini na dhiki waliyonayo watanzania ni Bunge. Bunge, kama mhimili muhimu wa dola, na msimamizi na mwakilishi wa mwananchi, limepoteza mwelekeo kabisa na sasa linazamisha fikra za wananchi. Huu uzi unajadili siasa uchwara zilizoshamiri bungeni badala ya kuangalia nchi inaelekea wapi?

Leo hii Kenya, Rwanda na Uganda wanapiga matarumbera ya uzinduzi wa uboreshwaji wa bandari ya Mombasa, kwa kile wanachosema ni kukuza/kuboresha mazingira ya biashara Afrika Mashariki, bila ya uwepo wa Tanzania.

Katika hali ya kawaida, mtu alitegemea bunge, na hasa kiongozi wa juu wa chama kinachoshika madaraka kutumia fursa aliyonayo bungeni ili kuanzisha mjadala wa jinsi Tanzania itakavyojipingana kwenye zama hizi za ushindani. Lakini tunaochoona ni upuuzi huko bungeni.

Ilikuwa makosa sana kumuondoa Sitta kwenye kiti uspika. Upuuzi wa Mwigulu unalitia hasara Taifa.
 
Alichosema mhe Mcheba kuhusu waheshimiwa Slaa na Mbowe ni wauwaji na wavunjifu wa amani kwa kusababisha vifo vya watanzania kauli hii hainachembe ya ukweli? kauli hii alitamka katika kikao cha 2 mkutano wa 12 wa bunge cha tarehe 28.8.2013 alikuwa anachangia kuhusu sheria ya mwaka1995 kuwadhibiti wanasiasa kudumisha amani,kauli ya mhe Mchema kwa waheshimiwa hawa kutochukuliwa hatuwa za kisheria inadhihirisha ukweli wa serikali ya chama cha mapiduzi ni dhaifu kwa kushidwa kusimamia sheria zake,kushindwa huku kwa serikali sikwa bahati mbaya bali nikwa kubaini mvunjivu wa amani na kusababisha vifo vya wa tanzania ni serikali ya chama cha mapinduzi kwa mtazamo huu kauli ya mhe Mchema siyakweli ni ya upotoshaji kwa watanzania,serikali ya chama cha mapinduzi kwa makusudi iliwanyima watanzani elimu kwa kiasi cha kushindwa kutafakari kauli za kipuuzi kama za wakina Mhe Chemba.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom