Mwigamba: Kukamatwa kumenipa mafanikio ma3, siogopi jela | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwigamba: Kukamatwa kumenipa mafanikio ma3, siogopi jela

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mwangaza, Dec 22, 2011.

 1. Mwangaza

  Mwangaza Senior Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 198
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33

  COPIED FROM FB, by Mtanzania Halisi:

  Nukuu ya Samson Mwigamba: -

  “ Kwa sasa napenda kuwaambia wasomaji wangu kwamba safari yangu ya siku 8 iliyoanzia chumba cha mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kuishia Gereza la Mahabusu la Keko ilikuwa ya mafanikio makubwa.

  Fanikio la kwanza ni kwamba safari hiyo IMESABABISHA MAKALA ILE ISOMWE NA ASKARI WENGI ZAIDI NA RAIA WENGI ZAIDI. Wakati naandika makala ile nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine askari wengi wa nchi hii hawasomi makala kama hizi kutokana na asili ya kazi yao. Lakini nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine hata raia wa kawaida ni wachache watakaosoma na hivyo ujumbe wangu kuwa umewafikia watu wachache.

  Fanikio la pili la safari yangu hiyo ni kwamba imeniwezesha kuishi japo kwa siku kadhaa maisha ya nusu jehanamu iitwayo mahabusu hapa Tanzania. SASA SIOGOPI TENA KWENDA HUKO WALA SIOGOPI TENA KUFUNGWA. “  Na fanikio la tatu, nimefanikiwa kujua yale ambayo sikuyajua. Yako mengi yaliyonipeleka huko na ambayo ndiyo niliyoyataka na nitayaandikia ripoti kamili na kuifikisha kunakohusika. Lakini najua wengi mnataka kujua ilikuwaje huko hivyo nitawasimulia kwa kifupi ilikuwaje.

  SOURCE: Wameniweka kizuizini lakini mawazo yangu yako huru

  MyTake: Kama ilivyodesturi ya Polisi kutekeleza maagizo bila kutathimini madhala yake, Kumshitaki Samson Mwigala ni sawa na "Kumpiga chura teke"
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  nachelea kuamini katika hili polisi wametumia utashi wao bali msukumo kutoka "mahala" pengine as almost have been katika masuala yenye maslahi kisiasa.
   
 3. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Pole sana mwigamba kwa yaliyokupata. Yote yanamwisho.
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Nasubiri ripoti Mwigamc kwa hamu. Kujua kilichn upande wa pili wa pazia ni vizuri.

  Makala Mwigamba ambayo Polisi wameíta ya kichochezi na ya wiki hii "WAMENIWEKA KIZUIZINI LAKINI MAWAZO YANGU YAKO HURU" na ile ya Mwanakijiji " Je, hii ni makala ya kichochezi?" vinazidi kufunua akili yangu juu ya ubovu, usiseme udhaifu, wa POLISI Tanzania.
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kilichonifurahisha baada ya mwigamba kufika keko na wafungwa kugundua kuwa ni mwenyekiti wa chadema wa mkoa wa Arusha,alichotewa maji ya kuoga,alipewa godoro la kulalia,na hakuwa na zamu yoyote ile maana jamaa walijua kuwa ni mkombozi wa wanyonge.
   
 6. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Wameniweka kizuizini lakini mawazo yangu yako huru
  [​IMG]

  Samson Mwigamba ​
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] [TABLE]
  [TR]
  [TD] "WAMENIWEKA kizuizini kwa zaidi ya wiki moja lakini mawazo yangu hayakuzuiliwa hata kwa dakika moja, wameulaza mwili wangu katika mazingira magumu kwa zaidi ya wiki moja lakini ubongo wangu haukuathirika hata chembe, kwa zaidi ya wiki moja walifanya kazi ya kuudhoofisha mwili lakini roho ya ujasiri iliyo ndani yangu imeimarika maradufu".
  Haya ni maneno niliyoyatamka kwa watu wa kwanza niliokutana nao baada ya kuachiwa kwa dhamana mahakamani Kisutu siku ya Alhamisi Desemba 15, 2011 na kesho yake Ijumaa Desemba 16, 2011 nikayaweka kwenye ukurasa wangu wa Facebook.
  Sitaingia undani wa kesi yangu iliyo mahakamani ndugu wasomaji ambapo ninashtakiwa kwa uchochezi na imeelezwa na waendesha mashtaka wa serikali kwamba nimewashawishi askari wa majeshi yote kukataa kutii amri ya serikali halali iliyoko madarakani. Makala husika wengi mmeshaisoma na kama kweli ni ya uchochezi Mahakama ya Kisutu itaamua.
  Kwa sasa napenda kuwaambia wasomaji wangu kwamba safari yangu ya siku 8 iliyoanzia chumba cha mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kuishia Gereza la Mahabusu la Keko ilikuwa ya mafanikio makubwa.
  Fanikio la kwanza ni kwamba safari hiyo imesababisha makala ile isomwe na askari wengi zaidi na raia wengi zaidi. Wakati naandika makala ile nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine askari wengi wa nchi hii hawasomi makala kama hizi kutokana na asili ya kazi yao. Lakini nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine hata raia wa kawaida ni wachache watakaosoma na hivyo ujumbe wangu kuwa umewafikia watu wachache.
  Lakini hatua ya Polisi kuniweka rumande na hatimaye kunifikisha mahakamani, kumewafanya askari na raia wa kawaida wengi sana kuitafuta makala hiyo na kuisoma wengine mara mbili na wengine mara tatu na hata mara nne.
  Wazo la msingi la makala ile ilikuwa kuwataka askari kufanya kazi kwa kutumia akili zao kwa kutafakari. Kama askari wanatakiwa kutii amri bila kutumia akili yao kwa nini wale walioamriwa wakawakamate na kisha kuwapeleka msitu wa Pande na kuwaua wafanyabiashara wa Mahenge hatimaye walifikishwa Mahakama ya Kisutu na serikali ya JK huyo huyo na IGP huyo huyo, DCI huyo huyo na hata DPP huyo huyo?
  Lakini swali jingine, kama askari anatakiwa kufanya kazi ya kutii amri halali na haramu bila kutumia akili yake, kwa nini rais huyu huyu alilihutubia taifa kupitia kwa wazee wa Dar es salaam na kuwaasa wafanyakazi na umma kwa ujumla kwamba busara ya kawaida inatakiwa kufanya kazi kama mbayuwayu? Kwamba akili ya kuambiwa changanya na yako? Si angesema pale kwamba mfano huo hauwahusu polisi?
  Nakumbuka maandamano ya kanda kwa kanda ya CHADEMA yalipoanza kule Mwanza, Rais Jakaya Kikwete mara moja akakimbia kwenye kulihutubia taifa na kudai eti serikali yake imechaguliwa kihalali kwa hiyo lazima CHADEMA wasubiri 2015 kuitoa madarakani. Nimeandika makala simple sana ya kuunga mkono kauli ya rais na kuwashauri askari wetu kwamba kama wafanyakazi wengine na wao "akili ya kuambiwa wachanganye na ya kwao", walinda serikali wananikamata kwamba nawaasa askari wasitii amri ya serikali halali iliyoko madarakani.
  Huu wimbo wa ‘serikali halali iliyoko madarakani' unamaanisha nini? Je, hii si dalili kwamba CCM iliingia kwamba safari hii iliingia madarakani kwa kuchakachua na hivyo ikiona hata ‘nyasi' inadhani ni ‘nyoka'
  Mbona wakati ule walipopata ushindi wa asilimia 80.2 hatukuusikia huu wimbo? Kwa nini miaka hii? Na kwa nini Februari 5 mwaka huu Rais Kikwete akiwahutubia wana CCM wenzake kule Dodoma aliwaambia "wapinzani wametusumbua sana na hivyo huko tuendako inabidi tugangamare sana"? Je, kugangamara alikomaanisha ni kwamba aliingia madarakani isivyo halali na hivyo inabidi wagangamare ili kusalia kwenye madaraka kwa miaka 5?
  Na je, kugangamara kwenyewe ndo huku kutumia Polisi DCI kunyamazisha uhuru wa maoni? Kama ndivyo napenda nirejee maneno ya mwandishi Angela Kiwia kwenye Dira la Jumatatu wiki hii kwamba wamekosea sana maana hiyo ni sawa na kuzuia mvua isinyeshe.
  Fanikio la pili la safari yangu hiyo ni kwamba imeniwezesha kuishi japo kwa siku kadhaa maisha ya nusu jehanamu iitwayo mahabusu hapa Tanzania. Sasa siogopi tena kwenda huko wala siogopi tena kufungwa.
  Na fanikio la tatu, nimefanikiwa kujua yale ambayo sikuyajua. Yako mengi yaliyonipeleka huko na ambayo ndiyo niliyoyataka na nitayaandikia ripoti kamili na kuifikisha kunakohusika. Lakini najua wengi mnataka kujua ilikuwaje huko hivyo nitawasimulia kwa kifupi ilikuwaje.
  Nilipigiwa simu na SSP Hiza wa ofisi ya DCI makao makuu ya Jeshi la Polisi Jumatatu Desemba 5. Nikaitika wito na kuripoti ofisini kwake Jumanne kesho yake ambapo nilihojiwa na Inspekta Msaidizi Nicholaus Stanslaus juu ya makala niliyoitaja hapo juu nikituhumiwa kama nilivyoeleza.
  Baada ya kuandika maelezo yangu nilitakiwa kuripoti tena polisi kesho yake Jumatano na nikafanya hivyo na ndipo nilipokamatwa siku hiyo hiyo na kuswekwa rumande ya Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
  Nililala humo mpaka asubuhi wakaja kunichukua na kunirejesha makao makuu ya jeshi kabla ya asubuhi hiyo hiyo ya Alhamisi Desemba 8 kupelekwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa shtaka hilo la uchochezi.
  Walikuwepo madiwani wawili waliokuwa tayari kunidhamini lakini kwa maombi ya upande wa mashtaka nilitakiwa kuwa na wadhamini wawili na mmoja lazima awe na hati ya nyumba.
  Na kwa sababu hakuna aliyelitarajia sharti hilo hakuna aliyekuwa nayo pale mahakamani na hivyo nikaambiwa sikutimiza masharti ya dhamana na ndipo nikapelekwa kwenye Gereza la Mahabusu la Keko. Niliingia gerezani Keko nikiwa nimevalia vazi la kombati, kitu kilichowafanya mahabusu zaidi ya 1,000 walioko mle na wafungwa takriban 100 pamoja na askari magereza wote kunitambua kirahisi kwamba ni mtu wa CHADEMA.
  Kama kuna kitu nawashukuru wapelelezi wa DCI Manumba na Usalama wa Taifa ambao tuligundua kwamba walikuwa wakifanya kazi kwa karibu sana katika suala hili, ni kule kutouambia uongozi wa Gereza la Keko kunitenga na mahabusu wa kawaida. Kwa hiyo nilipofika nilichanganywa nao ugali na maharage, nikalala nao ‘mchongoma', mpaka nikapata fursa ya kutembelea chumba cha ‘gereza ndani ya gereza'.
  Ugali unatolewa mara moja kwa saa 24 na mchana wa kati ya saa 6 na saa 9. Ni ugali uliopikwa kwa unga ambao kimsingi hata mbwa anayefugwa nyumbani kwa waziri anaweza asiule kwa maharage yaliyochemshwa (si kupikwa).
  Baada ya kula saa 10 alasiri kengele inapigwa na wote mnalazimishwa kwenda kulala. Selo namba 5 na 6 za bwalo namba IV ambazo nililala (namba 5 siku moja na namba 6 siku 6), zote zina eneo la futi za eneo 450. Kwa kipimo cha siku hizi ni chumba cha kama mita 9 kwa tano hivi. Mpaka leo kwenye milango kibao kimebandikwa kwamba wanatakiwa kulala watu 15 kila selo lakini namba 5 tulilala 66 na namba 6 hadi naondoka tulikuwa tukilala watu 64.
  Siku ile ya kwanza nilipelekwa mnadani (mahali ambapo mahabusu wageni hujikusanya na manyapara wa kila selo kuja kuchagua idadi ya kuongeza kwenye selo zao kama wanunuzi wachaguavyo ng'ombe mnadani) na nikachukuliwa kwenda namba 5. Kule tulilala mchongoma. Mchongoma ni aina ya kulala kwa kujibananisha kupita kiasi ili watoshee watu zaidi ya 60 kwenye selo waliyopaswa kulala watu 15.
  Kwanza mnajinyoosha kama maiti inyooshwavyo kisha mnalalia ubavu ambapo wa kwanza akilala kwa kuelekeza kichwa ukutani anayefuata ataelekeza miguu, anayefuata kichwa, anayefuata miguu, mpaka mwisho. Hakuna kujigeuza kwa kuwa hakuna nafasi na utakuwa unawasumbua wenzako lakini kutokana na kuchoka inabidi kila baada ya masaa mawili nyapara apige makofi na hapo ndipo mnageuka wote na kulalia ubavu mwingine.
  Hayo ni machache kati ya mengi sana niliyoyagundua kule. Kama nilivyosema mwanzo, yaliyo mazito nitayafikisha kunakohusika. Lakini naomba niwashukuru sana mahabusu wa Keko kwa jinsi walivyonipokea na ushirikiano walionipa tangu waliponipokea.
  Kwa kuwa niliingia nikiwa sina ndoo ya kuchotea maji nilitakiwa nisioge mpaka siku ninapokwenda mahakamani kwa mujibu wa sheria za selo kama nilivyopewa orientation na mabwana afya wa selo zote za 5 na 6.
  Lakini siku ya kwanza nilipolala namba 5 ratiba ilikatizwa na mahabusu wote wakatangaziwa kwamba wamwachie kiongozi aoge kwanza. Nikaenda kuoga na asubuhi nilioga pia wakati ni wale wanaomiliki ndoo tu ndio wanaoruhusiwa kuoga mara mbili kwa siku.
  Kesho yake kijana kutoka Arusha alinitambua na kuniuliza. Nilipomhakikishia kwamba mimi ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha, alisikitika sana. Amekaa ndani ya gereza lile tangu 2008 na kesi yake haijaanza kusikilizwa.
  Yeye alinipeleka kwa askari wa selo namba 6 ambaye amekaa humo gerezani tangu 2010 Julai akiwa ni zao la siasa chafu za CCM kwa kuwa alikuwa anagombea udiwani kwenye kata moja.
  Yeye alinipangia mahali pa kulala kwenye kigodoro changu peke yangu, akisema kiongozi huwezi kulala mchongoma. Nilioga mara mbili kwa siku kwa ridhaa ya mahabusu wote na siku ya zamu yangu ya kuchota maji, tuliokuwa nao zamu walikataa katakata nisichote maji. Hata kombati ilipochafuka nikataka kufua, vijana walininyang'anya na kuifua wao.
  Siku naondoka mle kwa pamoja waliniomba kwa niaba ya mahabusu wote wa Tanzania niwe msemaji wao. Nilikubali wajibu huo na nitautekeleza kwa uwezo wangu wote kwa namna tuliyokubaliana nao. Nachukua fursa hii kuwapa pole mahabusu wote Tanzania kwa jinsi ambavyo wanatendewa kinyume cha Katiba ya nchi ibara ya 13 (6) (b) ambayo inasema: "Ni marufuku kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo".
  Lakini ndugu hawa wamefungwa tayari bila mahakama kuthibitisha kama wana hatia. Wakati naingia nilikuta katoka siku chache tu zilizopita mahabusu ambaye aliishi ndani ya gereza hilo kwa miaka 11 halafu baadaye mahakama ikamwachia huru kwamba hakutenda kosa hilo.
  Mahabusu tunaowaona ndani ya mabasi na makarandika ya polisi ni asilimia chini ya 20 ambao wametenda makosa kweli. Wengi ni wale ambao wanakamatwa na askari wakifika kituoni na baadaye kubambikiziwa kesi nyingine.
  Vivyo hivyo kwa kesi za mauaji. Matokeo yake vijana wa watu waliokamatwa kwa uzururaji wanajikuta wanafikishwa mahakamani kwa mauaji na hawatakiwi kujibu lolote kwa kuwa mahakama waliyofikishwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na wanakwenda kukaa jela miaka mitano, sita, nane, kumi ama hata 11 bila hatia.
  Wanaacha kazi zao ama biashara zao, familia zao zinayumba, wanaliongezea taifa mzigo wa kuwalisha bila kufanya kazi kwa miaka yote hiyo kwa kubambikiwa kesi au aidha kwa chuki binafsi ama kwa sababu wameshindwa kutoa rushwa.
  Mahabusu hawa hawaruhusiwi kupiga kura wala kuchangia mchakato wa katiba mpya. Hawana mawasiliano na yeyote na simu ndani ya gereza ni kosa la jinai ambalo litakupeleka gerezani ndani ya gereza.
  Nilikwenda kuwasalimia wale waliokuwa ndani ya gereza gerezani. Ni watu wenye makosa ya kukutwa na simu, ama sigara ama wakapigana na wenzao. Hawa huwekwa kwenye selo maalumu namba 6 kwenye bwalo namba 6. Ndani ya selo hiyo watakaa siku 14 mchana na usiku bila kutoka nje ya selo.
  Nikataka kujua hizo simu zinaingizwaje gerezani. Kwa sababu siku tunaingia tulivuliwa nguo zote na kusachiwa kwa kupitishiwa scanner ya kutambua kama tumeficha kitu chochote mwilini. Na hilo hufanyika kwa kila mahabusu ama mfungwa anayeingia kutoka nje ya mlango wa gereza bila kujali kama atatoka na kuingia mara ngapi kwa siku hiyo.
  Nikaambiwa kwamba askari wenyewe wanachukua rushwa kwa mahabusu na kuwaletea simu halafu kisha tena wanakuja kuzikamata na kupewa rushwa na wakikosa wanakupeleka kwenye selo ya adhabu.
  Ndugu zangu ukurasa huu hautatosha kueleza yote. Nawasihi tu tubadili mtazamo na kuanza kupigania haki za hawa watu pia. Ni Watanzania wenzetu wanaoonewa sana bila mtetezi kwa kuwa tulio nje tunadhani ni majambazi wote, ni wauaji wote, ni wezi wote, ni wachochezi wote, na kila aina ya makosa, kumbe sivyo. Jaribu kutafakari lakini kujua vizuri ni mpaka ufike kule. Kama una ubavu andika makala ya uchochezi upelekwe.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 7. F

  Froida JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  Wameniweka kizuizini lakini mawazo yangu yako huru
  [​IMG]

  Samson Mwigamba

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]
  “WAMENIWEKA kizuizini kwa zaidi ya wiki moja lakini mawazo yangu hayakuzuiliwa hata kwa dakika moja, wameulaza mwili wangu katika mazingira magumu kwa zaidi ya wiki moja lakini ubongo wangu haukuathirika hata chembe, kwa zaidi ya wiki moja walifanya kazi ya kuudhoofisha mwili lakini roho ya ujasiri iliyo ndani yangu imeimarika maradufu”.
  Haya ni maneno niliyoyatamka kwa watu wa kwanza niliokutana nao baada ya kuachiwa kwa dhamana mahakamani Kisutu siku ya Alhamisi Desemba 15, 2011 na kesho yake Ijumaa Desemba 16, 2011 nikayaweka kwenye ukurasa wangu wa Facebook.

  Sitaingia undani wa kesi yangu iliyo mahakamani ndugu wasomaji ambapo ninashtakiwa kwa uchochezi na imeelezwa na waendesha mashtaka wa serikali kwamba nimewashawishi askari wa majeshi yote kukataa kutii amri ya serikali halali iliyoko madarakani. Makala husika wengi mmeshaisoma na kama kweli ni ya uchochezi Mahakama ya Kisutu itaamua.
  Kwa sasa napenda kuwaambia wasomaji wangu kwamba safari yangu ya siku 8 iliyoanzia chumba cha mahabusu cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na kuishia Gereza la Mahabusu la Keko ilikuwa ya mafanikio makubwa.

  Fanikio la kwanza ni kwamba safari hiyo imesababisha makala ile isomwe na askari wengi zaidi na raia wengi zaidi. Wakati naandika makala ile nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine askari wengi wa nchi hii hawasomi makala kama hizi kutokana na asili ya kazi yao. Lakini nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine hata raia wa kawaida ni wachache watakaosoma na hivyo ujumbe wangu kuwa umewafikia watu wachache.
  Lakini hatua ya Polisi kuniweka rumande na hatimaye kunifikisha mahakamani, kumewafanya askari na raia wa kawaida wengi sana kuitafuta makala hiyo na kuisoma wengine mara mbili na wengine mara tatu na hata mara nne.

  Wazo la msingi la makala ile ilikuwa kuwataka askari kufanya kazi kwa kutumia akili zao kwa kutafakari. Kama askari wanatakiwa kutii amri bila kutumia akili yao kwa nini wale walioamriwa wakawakamate na kisha kuwapeleka msitu wa Pande na kuwaua wafanyabiashara wa Mahenge hatimaye walifikishwa Mahakama ya Kisutu na serikali ya JK huyo huyo na IGP huyo huyo, DCI huyo huyo na hata DPP huyo huyo?

  Lakini swali jingine, kama askari anatakiwa kufanya kazi ya kutii amri halali na haramu bila kutumia akili yake, kwa nini rais huyu huyu alilihutubia taifa kupitia kwa wazee wa Dar es salaam na kuwaasa wafanyakazi na umma kwa ujumla kwamba busara ya kawaida inatakiwa kufanya kazi kama mbayuwayu? Kwamba akili ya kuambiwa changanya na yako? Si angesema pale kwamba mfano huo hauwahusu polisi?

  Nakumbuka maandamano ya kanda kwa kanda ya CHADEMA yalipoanza kule Mwanza, Rais Jakaya Kikwete mara moja akakimbia kwenye kulihutubia taifa na kudai eti serikali yake imechaguliwa kihalali kwa hiyo lazima CHADEMA wasubiri 2015 kuitoa madarakani. Nimeandika makala simple sana ya kuunga mkono kauli ya rais na kuwashauri askari wetu kwamba kama wafanyakazi wengine na wao “akili ya kuambiwa wachanganye na ya kwao”, walinda serikali wananikamata kwamba nawaasa askari wasitii amri ya serikali halali iliyoko madarakani.

  Huu wimbo wa ‘serikali halali iliyoko madarakani’ unamaanisha nini? Je, hii si dalili kwamba CCM iliingia kwamba safari hii iliingia madarakani kwa kuchakachua na hivyo ikiona hata ‘nyasi’ inadhani ni ‘nyoka’
  Mbona wakati ule walipopata ushindi wa asilimia 80.2 hatukuusikia huu wimbo? Kwa nini miaka hii? Na kwa nini Februari 5 mwaka huu Rais Kikwete akiwahutubia wana CCM wenzake kule Dodoma aliwaambia “wapinzani wametusumbua sana na hivyo huko tuendako inabidi tugangamare sana”? Je, kugangamara alikomaanisha ni kwamba aliingia madarakani isivyo halali na hivyo inabidi wagangamare ili kusalia kwenye madaraka kwa miaka 5?
  Na je, kugangamara kwenyewe ndo huku kutumia Polisi DCI kunyamazisha uhuru wa maoni? Kama ndivyo napenda nirejee maneno ya mwandishi Angela Kiwia kwenye Dira la Jumatatu wiki hii kwamba wamekosea sana maana hiyo ni sawa na kuzuia mvua isinyeshe.

  Fanikio la pili la safari yangu hiyo ni kwamba imeniwezesha kuishi japo kwa siku kadhaa maisha ya nusu jehanamu iitwayo mahabusu hapa Tanzania. Sasa siogopi tena kwenda huko wala siogopi tena kufungwa.
  Na fanikio la tatu, nimefanikiwa kujua yale ambayo sikuyajua. Yako mengi yaliyonipeleka huko na ambayo ndiyo niliyoyataka na nitayaandikia ripoti kamili na kuifikisha kunakohusika. Lakini najua wengi mnataka kujua ilikuwaje huko hivyo nitawasimulia kwa kifupi ilikuwaje.
  Nilipigiwa simu na SSP Hiza wa ofisi ya DCI makao makuu ya Jeshi la Polisi Jumatatu Desemba 5. Nikaitika wito na kuripoti ofisini kwake Jumanne kesho yake ambapo nilihojiwa na Inspekta Msaidizi Nicholaus Stanslaus juu ya makala niliyoitaja hapo juu nikituhumiwa kama nilivyoeleza.

  Baada ya kuandika maelezo yangu nilitakiwa kuripoti tena polisi kesho yake Jumatano na nikafanya hivyo na ndipo nilipokamatwa siku hiyo hiyo na kuswekwa rumande ya Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
  Nililala humo mpaka asubuhi wakaja kunichukua na kunirejesha makao makuu ya jeshi kabla ya asubuhi hiyo hiyo ya Alhamisi Desemba 8 kupelekwa Mahakama ya Kisutu na kusomewa shtaka hilo la uchochezi.

  Walikuwepo madiwani wawili waliokuwa tayari kunidhamini lakini kwa maombi ya upande wa mashtaka nilitakiwa kuwa na wadhamini wawili na mmoja lazima awe na hati ya nyumba.
  Na kwa sababu hakuna aliyelitarajia sharti hilo hakuna aliyekuwa nayo pale mahakamani na hivyo nikaambiwa sikutimiza masharti ya dhamana na ndipo nikapelekwa kwenye Gereza la Mahabusu la Keko. Niliingia gerezani Keko nikiwa nimevalia vazi la kombati, kitu kilichowafanya mahabusu zaidi ya 1,000 walioko mle na wafungwa takriban 100 pamoja na askari magereza wote kunitambua kirahisi kwamba ni mtu wa CHADEMA.

  Kama kuna kitu nawashukuru wapelelezi wa DCI Manumba na Usalama wa Taifa ambao tuligundua kwamba walikuwa wakifanya kazi kwa karibu sana katika suala hili, ni kule kutouambia uongozi wa Gereza la Keko kunitenga na mahabusu wa kawaida. Kwa hiyo nilipofika nilichanganywa nao ugali na maharage, nikalala nao ‘mchongoma’, mpaka nikapata fursa ya kutembelea chumba cha ‘gereza ndani ya gereza’.

  Ugali unatolewa mara moja kwa saa 24 na mchana wa kati ya saa 6 na saa 9. Ni ugali uliopikwa kwa unga ambao kimsingi hata mbwa anayefugwa nyumbani kwa waziri anaweza asiule kwa maharage yaliyochemshwa (si kupikwa).

  Baada ya kula saa 10 alasiri kengele inapigwa na wote mnalazimishwa kwenda kulala. Selo namba 5 na 6 za bwalo namba IV ambazo nililala (namba 5 siku moja na namba 6 siku 6), zote zina eneo la futi za eneo 450. Kwa kipimo cha siku hizi ni chumba cha kama mita 9 kwa tano hivi. Mpaka leo kwenye milango kibao kimebandikwa kwamba wanatakiwa kulala watu 15 kila selo lakini namba 5 tulilala 66 na namba 6 hadi naondoka tulikuwa tukilala watu 64.
  Siku ile ya kwanza nilipelekwa mnadani (mahali ambapo mahabusu wageni hujikusanya na manyapara wa kila selo kuja kuchagua idadi ya kuongeza kwenye selo zao kama wanunuzi wachaguavyo ng’ombe mnadani) na nikachukuliwa kwenda namba 5. Kule tulilala mchongoma. Mchongoma ni aina ya kulala kwa kujibananisha kupita kiasi ili watoshee watu zaidi ya 60 kwenye selo waliyopaswa kulala watu 15.

  Kwanza mnajinyoosha kama maiti inyooshwavyo kisha mnalalia ubavu ambapo wa kwanza akilala kwa kuelekeza kichwa ukutani anayefuata ataelekeza miguu, anayefuata kichwa, anayefuata miguu, mpaka mwisho. Hakuna kujigeuza kwa kuwa hakuna nafasi na utakuwa unawasumbua wenzako lakini kutokana na kuchoka inabidi kila baada ya masaa mawili nyapara apige makofi na hapo ndipo mnageuka wote na kulalia ubavu mwingine.
  Hayo ni machache kati ya mengi sana niliyoyagundua kule. Kama nilivyosema mwanzo, yaliyo mazito nitayafikisha kunakohusika. Lakini naomba niwashukuru sana mahabusu wa Keko kwa jinsi walivyonipokea na ushirikiano walionipa tangu waliponipokea.

  Kwa kuwa niliingia nikiwa sina ndoo ya kuchotea maji nilitakiwa nisioge mpaka siku ninapokwenda mahakamani kwa mujibu wa sheria za selo kama nilivyopewa orientation na mabwana afya wa selo zote za 5 na 6.
  Lakini siku ya kwanza nilipolala namba 5 ratiba ilikatizwa na mahabusu wote wakatangaziwa kwamba wamwachie kiongozi aoge kwanza. Nikaenda kuoga na asubuhi nilioga pia wakati ni wale wanaomiliki ndoo tu ndio wanaoruhusiwa kuoga mara mbili kwa siku.
  Kesho yake kijana kutoka Arusha alinitambua na kuniuliza. Nilipomhakikishia kwamba mimi ndiye Mwenyekiti wa CHADEMA wa Mkoa wa Arusha, alisikitika sana. Amekaa ndani ya gereza lile tangu 2008 na kesi yake haijaanza kusikilizwa.

  Yeye alinipeleka kwa askari wa selo namba 6 ambaye amekaa humo gerezani tangu 2010 Julai akiwa ni zao la siasa chafu za CCM kwa kuwa alikuwa anagombea udiwani kwenye kata moja.
  Yeye alinipangia mahali pa kulala kwenye kigodoro changu peke yangu, akisema kiongozi huwezi kulala mchongoma. Nilioga mara mbili kwa siku kwa ridhaa ya mahabusu wote na siku ya zamu yangu ya kuchota maji, tuliokuwa nao zamu walikataa katakata nisichote maji. Hata kombati ilipochafuka nikataka kufua, vijana walininyang’anya na kuifua wao.
  Siku naondoka mle kwa pamoja waliniomba kwa niaba ya mahabusu wote wa Tanzania niwe msemaji wao. Nilikubali wajibu huo na nitautekeleza kwa uwezo wangu wote kwa namna tuliyokubaliana nao. Nachukua fursa hii kuwapa pole mahabusu wote Tanzania kwa jinsi ambavyo wanatendewa kinyume cha Katiba ya nchi ibara ya 13 (6) (b) ambayo inasema: “Ni marufuku kwa mtu aliyeshitakiwa kwa kosa la jinai kutendewa kama mtu mwenye kosa hilo mpaka itakapothibitika kuwa anayo hatia ya kutenda kosa hilo”.

  Lakini ndugu hawa wamefungwa tayari bila mahakama kuthibitisha kama wana hatia. Wakati naingia nilikuta katoka siku chache tu zilizopita mahabusu ambaye aliishi ndani ya gereza hilo kwa miaka 11 halafu baadaye mahakama ikamwachia huru kwamba hakutenda kosa hilo.
  Mahabusu tunaowaona ndani ya mabasi na makarandika ya polisi ni asilimia chini ya 20 ambao wametenda makosa kweli. Wengi ni wale ambao wanakamatwa na askari wakifika kituoni na baadaye kubambikiziwa kesi nyingine.

  Vivyo hivyo kwa kesi za mauaji. Matokeo yake vijana wa watu waliokamatwa kwa uzururaji wanajikuta wanafikishwa mahakamani kwa mauaji na hawatakiwi kujibu lolote kwa kuwa mahakama waliyofikishwa haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na wanakwenda kukaa jela miaka mitano, sita, nane, kumi ama hata 11 bila hatia.

  Wanaacha kazi zao ama biashara zao, familia zao zinayumba, wanaliongezea taifa mzigo wa kuwalisha bila kufanya kazi kwa miaka yote hiyo kwa kubambikiwa kesi au aidha kwa chuki binafsi ama kwa sababu wameshindwa kutoa rushwa.
  Mahabusu hawa hawaruhusiwi kupiga kura wala kuchangia mchakato wa katiba mpya. Hawana mawasiliano na yeyote na simu ndani ya gereza ni kosa la jinai ambalo litakupeleka gerezani ndani ya gereza.

  Nilikwenda kuwasalimia wale waliokuwa ndani ya gereza gerezani. Ni watu wenye makosa ya kukutwa na simu, ama sigara ama wakapigana na wenzao. Hawa huwekwa kwenye selo maalumu namba 6 kwenye bwalo namba 6. Ndani ya selo hiyo watakaa siku 14 mchana na usiku bila kutoka nje ya selo.
  Nikataka kujua hizo simu zinaingizwaje gerezani. Kwa sababu siku tunaingia tulivuliwa nguo zote na kusachiwa kwa kupitishiwa scanner ya kutambua kama tumeficha kitu chochote mwilini. Na hilo hufanyika kwa kila mahabusu ama mfungwa anayeingia kutoka nje ya mlango wa gereza bila kujali kama atatoka na kuingia mara ngapi kwa siku hiyo.

  Nikaambiwa kwamba askari wenyewe wanachukua rushwa kwa mahabusu na kuwaletea simu halafu kisha tena wanakuja kuzikamata na kupewa rushwa na wakikosa wanakupeleka kwenye selo ya adhabu.Ndugu zangu ukurasa huu hautatosha kueleza yote. Nawasihi tu tubadili mtazamo na kuanza kupigania haki za hawa watu pia. Ni Watanzania wenzetu wanaoonewa sana bila mtetezi kwa kuwa tulio nje tunadhani ni majambazi wote, ni wauaji wote, ni wezi wote, ni wachochezi wote, na kila aina ya makosa, kumbe sivyo. Jaribu kutafakari lakini kujua vizuri ni mpaka ufike kule. Kama una ubavu andika makala ya uchochezi upelekwe.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Pamoja na hiyo makala inayodaiwa ni ya uchochezi, nafikiri uchadema wa Mwigamba umechangia kwa kiasi kikubwa kumkamata na kumshtaki. Kwa kuwa suala hili liko mahakamani, lets hope kwamba mahakama itatoa uamuzi wa haki!!!!

  Tiba
   
 9. F

  Froida JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli Safari ya Ukombozi inahitajika yaani usalama wa Taifa na Polisi wameanzisha genge la kutisha watu
  Hivi Usalama wa Taifa na Polisi wanaweza kutupa ushuhuda ni lini vyombo vya dola vilishinda Haki,Haki inacheleweshwa lakini haiwezi kunyang'anywa Kamwe ,Pole Samsom huu ni mwanzo tuu wa mateso wengi watateseke kuelekea kwenye ukombozi wa Kweli
   
 10. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hongera sana Mwigamba ndio uanamageuzi huo... tupo pamoja
   
 11. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2011
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Nimesoma makala hiyo hapo juu, hakika imenitia uchungu sana. Mungu ibariki tanzania. Mwigamba naomba nikutie moyo; mungu muumbaji yuko nawe kwani wewe umetangulia lkn wengi sana watakuja. Kumbuka kutafuta kitabu hiki kwenye signature yangu na kukisoma, kwani itakufariji sana kukufahamisha kwamba yupo mwombezi wetu yesu kristo katika patakatifu pa mbinguni na mlango wa rehema bado uko wazi. Na ubarikiwe.
   
 12. k

  kalikenya New Member

  #12
  Dec 22, 2011
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekua nikitoa machozi kila mstali niliousoma hivi Tanzania tumefikia hapo. Mwigamba Tanzania wanaofanya kazi ni waandishi wa habaritu na Mungu analijua Atakupiogania na utashinda tu serikari dhalimu haidumu hata
   
 13. Losomich

  Losomich JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Pole sana kiongozi! Mambo haya kama wanayatenda kwa watu wasiyo na hatia je kwa wenye hatia itakuwaje? Mungu akutie nguvu ili moyo wako wa ushujaa usitetereke mpaka mwisho wa yote! Just to mind you, ''No struggle no freedom at all.'' VIVA Mwigamba VIVA Chadema!!!
   
 14. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  well Mwigamba tembea kifua mbele tena umekuwa zaidi ya shujaa 2011, makala hilo naomba itafsiriwe kwa lugha ya kiingereza imekuwa na mvua bara zima la afrika walipo madikteta chini ya Asikari mbumbubu... HONGERA SANA SHUJAAA
   
Loading...