Mwezi wa tisa nahamia rasmi Dar

Shida na raha

JF-Expert Member
Aug 8, 2014
3,774
3,460
Habari za majukumu wakubwa na wadogo..

Kama mada inavojieleza hapo juu.
Kama kawaida ukiwa umeolewa na serikali shuruti urushwe rushwe kama kama mpira wa mdako...

Kwa mara ya kwanza nilianza kufanyia kazi

Kigoma...Dodoma...Kigoma...Zanzibar... Na sasa hivi nakuja Dar rasmi. Nawaomba watu Dar mnipe ushirikiano wenu wa hali na mali.. Makaazi yangu yatakua Kigamboni..

Watu Kigamboni tutakua tunaonana na kupiga swaga mbili tatu.. Ila kwa wale vibaka mkae mbali na mimi sitaki marafiki wa hivo.

Nikifika rasmi nitakuja kuwaomba mnisaidie sehemu ya kupanga ambayo hapana usumbufu na wezi maana chumba mara nyingi itakua kinabaki chenyewe.

Watu wa Dar nawaomba msiache kuja kunipa mongozo wa jinsi ya kuishi kwenye jiji takatifu...

Mshana wewe utakua kiongozi namba moja wa kunionesha eneo la kuishi ili kuepuka kilio cha kuibiwa mara kwa mara..
Nitakuja kukufata external kama kawaida yangu...

Mwisho niwatakie kazi njemaaaa.
 
Mshana Jr na Mambo ya vibaka wapi na wapi! Huyo muombe akusetie firewalls za kudhibiti vigagula vya mtaani kwako!
 
Habari za majukumu wakubwa na wadogo..

Kama mada inavojieleza hapo juu.
Kama kawaida ukiwa umeolewa na serikali shuruti urushwe rushwe kama kama mpira wa mdako...

Kwa mara ya kwanza nilianza kufanyia kazi

Kigoma...Dodoma...Kigoma...Zanzibar... Na sasa hivi nakuja Dar rasmi. Nawaomba watu Dar mnipe ushirikiano wenu wa hali na mali.. Makaazi yangu yatakua Kigamboni..

Watu Kigamboni tutakua tunaonana na kupiga swaga mbili tatu.. Ila kwa wale vibaka mkae mbali na mimi sitaki marafiki wa hivo.

Nikifika rasmi nitakuja kuwaomba mnisaidie sehemu ya kupanga ambayo hapana usumbufu na wezi maana chumba mara nyingi itakua kinabaki chenyewe.

Watu wa Dar nawaomba msiache kuja kunipa mongozo wa jinsi ya kuishi kwenye jiji takatifu...

Mshana wewe utakua kiongozi namba moja wa kunionesha eneo la kuishi ili kuepuka kilio cha kuibiwa mara kwa mara..
Nitakuja kukufata external kama kawaida yangu...

Mwisho niwatakie kazi njemaaaa.
Njoo Big Stone mkuu mm ntakuwa mwenyeji wako. Ila kama ww ni mlevi bas ntaondoa ubalozi wangu kwako maana huwa sipend rafiki mlevi
 
Kero ya Kigamboni ni umeme kukatika katika ingawa ambaye yupo kule tangu 2010 atakwambia sasa hivi haukatiki.
Miaka hiyo umeme ulikua unakatika hadi wiki mbili siku hizi labda ni mara mbili au tano kwa mwezi.

Wamakonde, Waarabu na Wanafunzi wa Chuo ndiyo wengi.

Ukifika ukiulizia gesti ukiona unapelekwa gest ambayo hamtumii barabara ya lami ila mmeingia makazi ya watu na nje ni kama nyumba kataa.
Ni mbaya sana, kuanzia huduma mpaka samani zake.

Wanajeshi wa Navy hawatojisumbua na kukulinda jilinde mwenyewe, kua attention haswa haswa ukiwa pale Ferry usiku na maeneo ya huku mbele usiku wa manane.

Kuna siku pantoni litazingua kama utaamua kupanda fiber/ vimtumbwi jiridhishe kua hakuna meli inayoingia au kutoka. Walikufa watu zaidi ya 5 siku hiyo na haikutangazwa popote.

Hairuhusiwi kupiga picha ndani ya pantoni, ukikamatwa jifanye hujui kiswahili. Hairuhusiwi kuingia na mtungi wa gesi kwenye pantoni.

Nauli ya pantoni ni 200, nashauri uwe na hela inayochenjika kwa urahisi pia kama wameishiwa tiketi hautapita hadi wazipate upya. Kama ni askari utapita bila kulipa na hata mwendokasi hautalipia.
 
Back
Top Bottom