Mwezi mbaya kwa mastaa Flora na Vick Kamata

wiseboy

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
2,930
3,299
Sakata la Mume wa mwimbaji FLORA MBASHA kumbaka shemeji yake mapya yaibuka Mume aelezea sababu za kufanya UKATILI huo..! Posted by Gumzo on May 29, 2014 JESHI la Polisi Mkoa wa Ilala jijini Dar es Salaam linamsaka kwa udi na uvumba Emmanuel Mbasha (pichani) ambaye ni mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kwa madai ya kumbaka shemeji yake mwenye miaka 17 (jina tunalo) ambaye ni yatima.

Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha anayetuhumiwa kwa ubakaji. Taarifa zilizopatikana ndani ya jeshi hilo kupitia vyanzo vyetu
makini zinadai kwamba mlalamikaji huyo alifika kituoni hapo Jumatatu iliyopita muda wa mchana na kufungua kesi yenye Kumbukumbu Na. TBT/
RB/3191/2014 na ya Jalada la Uchunguzi Na.

TBT/IR/1865/2014 akidai kufanyiwa unyama huo kwa siku mbili ( Ijumaa na Jumapili) wiki iliyopita nyumbani kwa Mbasha, Tabata-Kimanga, Dar. Ilidaiwa kuwa, Ijumaa iliyopita mlalamikiwa alifanya kitendo hicho sebuleni nyumbani na Jumapili ilidaiwa alitekeleza ukatili wake huo ndani ya gari lake hali
ambayo ilimfanya mlalamikaji kutoa taarifa Kituo cha Polisi, Tabara-Aroma jijini Dar. Mume wa mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha, Emmanuel Mbasha anayetafutwa na polisi kwa kosa la ubakaji. Iliendelea kudaiwa kuwa, kufuatia maumivu makali aliyoyapata mlalamikaji huyo ilibidi aende Hospitali ya Amana na kugundulika kuwa aliingiliwa kimapenzi na kumsababishia michubuko sehemu za siri.

HISTORIA YA MLALAMIyKAJI Mlalamikaji ni kati ya watoto mapacha waliozaliwa jijini Mwanza na mama ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Mama wa mtoto huyo (kwa sasa ni marehemu pamoja na mume wake) akiwa muumini wa Kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) aliamua kumtoa mtoto mmoja kwa mama mzazi wa Flora Mbasha kwa lengo la kumlea, wakati huo mtoto huyo alikuwa na miezi mitatu. Flora Mbasha akiwa na mumewe Emmanuel Mbasha.

Ikaelezwa kuwa, mama wa Flora alikaa na mtoto huyo akimsomesha hadi alipofika darasa la saba ambapo alimkabidhi kwa Flora na kuishi naye hadi alipofikwa na janga hilo. Maelezo zaidi yanasema Mbasha aliweza kufanya kitendo hicho kwa sababu mkewe (Flora) ameondoka nyumbani na kwenda kuishi hotelini kwa kile kilichodaiwa kwamba kuna ugomvi mkubwa ndani ya ndoa yao.

Taarifa zaidi zinadai kwa sasa Mbasha naye hayupo nyumbani kwake huku mlalamikaji yuko Hospitali ya Amana akiendelea kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ili kubaini kama ana maambukizi ya magonjwa ya zinaa au la! Wanandoa hao katika pozi. Kwa upande wake mlalamikaji huyo alipopigiwa simu juzi kwa lengo la kuthibitisha kuhusiana na sakata hilo alikiri na kusema amekwishatoa taarifa polisi kwa kitendo alichofanyiwa na mwenye nyumba huyo huyo.
 
Hawa mastaa wa bongo wala siyo vioo vya jamii bali ni majanga.
Ajipe moyo. Atayashinda
 

....hahaa mkuu hizi terminology za kanda ya ziwa hivi ni ndagu au ndago? kwa hiyo jamaa anatafta utajiri.....? hahaaa huoni kuna sehem wanadai flora kahamia hoteli no kugegedwa jamaa akaona isiwe tabu kajisevia ndani kwa ndani.
 
Hawa wazinzi wanaozuga na ulokole ni hatari sana kwenye jamii yetu. Bora uwe zinzi guberi na ujulukane kwa hilo, kuliko kuwa zinzi lokole, siku ya kiama utakuwa kuni.

....hivi si wale wanakuaga kwenye shooting vdeo na matamasha kwa pamoja? mwenye ka clip jaman.
 
Ka' mchezo hakana mwenyewe kwa hiyo anasubiri 30 years au ataishinda kesi kama ile nyimbo yao "jipe moyo utayashinda....."
 
Ninatoa mafunzo(seminar) kwa watu wanaotaka kuwa maarufu na hasa kutokana na injili ili waone hatari zinazowakabili mbele yao wajitahidi kuziepuka.Haya yote ni matokeo ya umaarufu kwake yeye na mkewe wakiwa hawajaandaliwa kuwa hivyo.Maamuzi aliyochukua mwanaume yanaonyesha udhaifu mkubwa!Angeenda kutafuta makurumbembe wa casino kuliko kulipiza kisasi kwa binti asiye na hatia

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Kwa Mwanamke mcha Mungu kuhama nyumba kwenda kukaa hotelini si maadili. Bola angehama chumba akiwa ndani ya nyumba yake au angeenda kukaa kwa ndugu au family friend kwa muda. Huko hotel tutajuaje alikua anafanywa nini? Na huyu mwanamme mkeo kaondoka nyumbani,unakaa na kisichana peke yenu cha nini? Peleka kwa ndugu kwa muda mpaka mkirekebisha mambo! Chakula angektla pale jirani Tabata Mawenzi bar,na hata hamu ikizidi vidada poa angeokota pale,na wala visingekua na noma kwani ni LKU- Lipia kadri unavyotumia!.Ulokole wa ku act mbaya sana.
 
Hawa wazinzi wanaozuga na ulokole ni hatari sana kwenye jamii yetu. Bora uwe zinzi guberi na ujulukane kwa hilo, kuliko kuwa zinzi lokole, siku ya kiama utakuwa kuni.

Mkuu Bujibuji umenikumbusha kisa cha jamaa mmoja alijifanya mlokole mara asali Winners Chapel mara Agape huku akiwa front kwa mambo ya sadaka na michango. Salalee kumbe mzinzi vimada 8, EPA yumo, na siku hizi kaacha mke wa ndoa katia ndani Koku.
 
Back
Top Bottom