Mwezi huu nimekataliwa na warembo 4 kwa sababu ya kuwa na nywele nyekundu

Jamani hali gani?

Niruke kwenye hoja yangu. Mimi ni mwanaume handsome tu safi, ninajua kuvaa na nina vihela vya kubadili mboga na tugari. Nimekuwa nikipata shida mno kupata mwanamke wa kuingia naye mahusianoni kwa sababu ya shida yangu ya nywele nyekundu.

Nina nywele nyekundu ndiyo, ila si kipili pili yaani zile za kujiviriga viriga na kuwa 'tim tim'. Nikichana zinachanika fresh na zinakuwa level safi tu, shida ni rangi yake nyekundu. Daaah! Yaani naandika huku nacheka na sijui kwa nini!

Simply tu nimegundua warembo wanaangalia mno nywele, na ndiyo maana vijana wengi wa sasa wanawekeza sana kwenye mitindo ya nywele na rangi. Siku hizi hakuna kitu kinachouzika madukani kama super blacks, zamani ilikuwa wateja ni wazee, ila nowadays ni vijana wenzetu ndiyo wateja.

Anyway nimejikubali na kuikubali hali yangu ya nywele, nimekataa kutumia super blacks na taka taka nyingine.

Kutokana na mazingira niliyokutana nao hawa mabinti, ilikuwa si rahisi kunijua kwa ukaribu hivyo hawakujua kuwa nina tuchenji, walianza kunihukumu kwa rangi ya nywele.

NB: Nimekubali yaishe ila nywele kupaka black ni big no. Najikubali, kwanza ukiwa mweupe na ukawa na nywele za kizungu (nyekundu) ni bonge la mvuto, mradi tu ziwe safi.

Ila kwa nyie weusi halafu mkawa na nywele nyekundu kwa kweli ni kituko mno (samahanini kwa kusema hili). Siku hizi kuna rate ya watu wengi weusi kuwa na nywele nyekundu, huo ni uchafu, ni kituko.

I think ukiwa mweusi na ukawa na nywele nyekundu super black itakufaa sana. Unlike kwa mtu mweupe kama mimi.

Mwenye kujua dawa tiririka weusi wapone.
pole, wewe ni mtu wa singida? singida kule kuna watu wengine wanakuwa weupe hadi nywele zinakuwa brown kidogo, ila ngozi yao ni ya kawaida, sio kwamba nawabagua ila kwa wema tu wengine huwa wanafikiri wana ulemavu wa ngozi. nyoa para tu nafikiri.
 
Mkuu hapa halinyolewi para wala nini
 
Pesa unazo za kutosha??
Au ni pesa zile za kulalamika huyu demu anapenda sana sana😏

Mpe vitu anavyotaka uongeze na ambavyo hajasema halafu urudi kutuambia😅😅
Acha kumtesa kijana mwenzanguu. Alafu acha kumwambia ukweliii🤣🤣🤣🤣
 
Wekundu wa nywele zako unawaogopesha wahisi labda una element za ualbino chief
 
Wewe tafuta hela tu. Nakupa yangu Sasa Mimi Ni mfupi wa futi 5, Nina kichwa cha bara (yaani chogo) , Nina kililipili kile chenyewe, Bado Ni mweusi tii na masikio kma ungo lakin baby zinaniita handsome boy tafuta hell tu acha kulalamika
 
Mbona uandishi wako unakukataa? Pesa haijifichi bhana. Wewe kajamba nani tu
 
We huna hela. Na kama unazo, basi bahili au unanuka mdomo. Full stop.
Ebana nywele nyekundu si uziweke fupi.
 
Back
Top Bottom