Habari za jioni!
Jamani mwenzenu jana nimezinguana na Baba watoto, katika purukushani nikamwambia niachee nitikise kibiriti....akanijibu subiri, sijakaa vizuri imeingia sms "Mimi Baba kidogoli nimekuacha Mamy K talaka 1, sio mke wangu"
Yani hapa nipo nipo sijui nilie, sijui nicheke, nahisi kisukari si kisukari, covid si covid....!
Wanazuoni njooni mnishauri hiyo si talaka tayari? Hivi kweli mkeo unayempenda akikwambia niache unamwambia hivo, kuna mapenzi hapo?
Nipeni ushauri manake kesho anarudi nyumbani najua ataanza kunibembeleza na kunambia hakuwa anamaanisha, kuna mapenzi hapa?