Mwenzenu nifahamisheni

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
576
NMB walikusanya pesa nyingi sana ya wananchi kwa maelezo kwamba wananchi wanunue hisa. Hata mimi nilinunua hisa za haja katika uwezo wangu, nikashawishi na wengine wakaingia pia. Niliwaambia wasiogope NMB sio DECI nyingine, maana wengine walishalizwa na serikali kwa kisingizio kwamba DECI ni haramu.

Nina wasiwasi sasa, muda mrefu siambiwi hatma ya hela yangu
 
Wasiwasi wangu unazidi kwa sababu hata niliowashawishi hawaniamini tena nikiwaambia mambo ambayo mimi nafikiri ni mambo ya kimsingi. Wamenivisha nguo ya ufisadi kama vile nami nashirikiana na NMB kuwapaisha hela yao kumbe hata mimi imekula kwangu.

Kuna tofauti gani sasa kati ya DECI na NMB? Nawasikia wanatoa misaada mamilioni kwa michezo ya mimpira, shuleni, wapi sijui.... lakini hata siku moja sijawasikia NMB wakisema gawio la wanahisa ni hela ngapi, achilia mbali kutoa cheti cha uthibitisho kwamba ninazo haki za hisa ngapi humo. Wakati tunanunua hisa, tulikuwa tunaandika jina la mtu fulani hivi pale NMB ati yeye ndiye zinapitia kwake kisheria. Kulikoni? DECI nao walikuwa na lugha tamu sana, lakini kwa kuwa serikali hawakukubaliana nao wakazimwa na hadi leo sijui hata kesi inaendeleaje maana sisikii ikitajwa.

Kuna yeyote anayejua? Kuna mashirika mengi yanasemasema habari ya hisa kuuzwa, nikisikia nakuwa kama majambazi mengine yanakuja kwa mkono wa serikali vile. Serikali badala ya kuangalia haki za mwananchi anayehangaika kusimama zinalindwa kumbe wako bussy na kuchaguliwa waende tena kukalia viti vilevile wanavyokoromea usingizi. Kipindi hiki nikidhani wangesemea pesa ya wananchi walala hoi, ya DECI na watu kama NMB hao feki. Lakini hata kunong'ona hamna! Hata mmoja, wanaelezea kupeleka bahari Kalenga na kujenga barabara za hewani tu.
 
Kunahitajika elimu ya kutosha kuhusu uwekezaji katika hisa. Unaponunua hisa ujue kabisa kuwa kampuni ikipata hasara na wewe umepata hasara na inapopatkana faida na wewe unapata faida kwa sababu na wewe ni mmiliki wa kampuni hiyo kwa asilimia japo chache. Kwa upande wa NMB sijajua, lakini kila mwaka lazima kunafanyika hesabu na kuona msimamo wa faida na hasara, bila kusahau vikao vya wanahisa kusomewa na kujadili mapato ya mwaka, ikiwemo gawio la faida au hasara(kama ipo), wewe umenunua hisa mwaka gani? na kama haujawahi kualikwa kwenye mkutano wa wenye hisa, na hauna doc yeyote kuonesha kuwa unamiliki hisa NMB hiyo inatia mashaka!!!!!!!!! Hata hivyo suala kama hilo sidhani kama kulileta hapa JF kabla haujaenda NMB kwenyewe kujua kulikoni, nadhani hii pia inatia mashaka kuhusu usiriazi wako katika kuwekeza na kuheshimu pesa yako!! (sorry for that sir!). Pia ikumbukwe kuwa, hisa zako unaweza kuzipiga bei muda wowote unaotaka (kama bei itakuwa imepanda unaweza kupata kafaida kidogo)

Mimi nina hisa chache TWIGA CEMENT, na TCC na kila muda nakwa updated kuhusu mwenendo wa soko.
 
NMB walikusanya pesa nyingi sana ya wananchi kwa maelezo kwamba wananchi wanunue hisa. Hata mimi nilinunua hisa za haja katika uwezo wangu, nikashawishi na wengine wakaingia pia. Niliwaambia wasiogope NMB sio DECI nyingine, maana wengine walishalizwa na serikali kwa kisingizio kwamba DECI ni haramu.

Nina wasiwasi sasa, muda mrefu siambiwi hatma ya hela yangu

Acha utani wewe, wenzio mbona wanakula gawio kama kawa!
 
Kama utakuwa umeingizwa mjini, basi utakuwa umekutana na wataalamu kiboko. Hapo uliposema kisheria hela inapitia kwa mtu, embu nena NMB uulize vizuri, isijekuwa uliingizwa mjini.
 
Kama utakuwa umeingizwa mjini, basi utakuwa umekutana na wataalamu kiboko. Hapo uliposema kisheria hela inapitia kwa mtu, embu nena NMB uulize vizuri, isijekuwa uliingizwa mjini.

Kama hujawahi pata dividend au kualikwa ktk mkutano wao,basi hiyo ni DECI kwako tu. Gawio jamaa wametoa mpaka nicol ambao ni wanahisa wa NMB nao waligawiwa zao,iweje ukose?
Nenda NMB kawaulize.
 
Na inabidi kuwaelemisha watu kuhusu hisa na aina zake. Kuna nyingine ukinunua hata kampuni ikilifilisika utapata gawiwo. inaofikia hatua ya kuifilishi kama inafilisika lazima wenye hisa wenye hisa salama walipwe, kwa hiyo unaponua hisa ni lazima uwe na uhakika kuwa hisa za kampuni unayonunua zisiwe uchi, ziwe salama, lakini za namna hii nazo bei yake si ndogo ni kubwa kuliko za kawaida.
 
hata mie nilinunua hisa NMB lakini nilishaziuza siku nyingi na fwedhwa ishaliwa. ukiangalia bei ya hisa za NMB sokoni sa hivi zinazidi kushuka kila kukicha.
 
Kunahitajika elimu ya kutosha kuhusu uwekezaji katika hisa. Unaponunua hisa ujue kabisa kuwa kampuni ikipata hasara na wewe umepata hasara na inapopatkana faida na wewe unapata faida kwa sababu na wewe ni mmiliki wa kampuni hiyo kwa asilimia japo chache. Kwa upande wa NMB sijajua, lakini kila mwaka lazima kunafanyika hesabu na kuona msimamo wa faida na hasara, bila kusahau vikao vya wanahisa kusomewa na kujadili mapato ya mwaka, ikiwemo gawio la faida au hasara(kama ipo), wewe umenunua hisa mwaka gani? na kama haujawahi kualikwa kwenye mkutano wa wenye hisa, na hauna doc yeyote kuonesha kuwa unamiliki hisa NMB hiyo inatia mashaka!!!!!!!!! Hata hivyo suala kama hilo sidhani kama kulileta hapa JF kabla haujaenda NMB kwenyewe kujua kulikoni, nadhani hii pia inatia mashaka kuhusu usiriazi wako katika kuwekeza na kuheshimu pesa yako!! (sorry for that sir!). Pia ikumbukwe kuwa, hisa zako unaweza kuzipiga bei muda wowote unaotaka (kama bei itakuwa imepanda unaweza kupata kafaida kidogo)

Mimi nina hisa chache TWIGA CEMENT, na TCC na kila muda nakwa updated kuhusu mwenendo wa soko.

Hapo pekundu Amoeba umekosea. Kwani upelelezi ni lazima uanzie wapi? Nilidhani mtu anaweza kukusanya taarifa regardless ameanzia wapi. Kwenda NMB ni wazo lako zuri tu ambalo sidhani kama linahitaji jazba kumshauri mtu. Kama kukosa seriousness, unadhani nimeleta insha hapa JF? Au unataka niamini kwamba hapa JF hakuna wenye mawazo mbadala kuliko ya kwangu na ya kwako? Wewe ungeandika nini kuhusu hili suala kama usingesoma mada yangu? Mbona wenzako wameeleza uzoefu wao vizuri tu, ambao kupitia wao nimepanuliwa zaidi kulikoni ningekaa kimya? Umefyongo mzee, pole lakini. hata hivyo maelezo yako yamenifundisha namna ya kupokea mawazo mbalimbali ya watu tofauti tofauti, maana tunatofautiana sana binadamu jinsi ya kujieleza na kuelewa tunachoambizana.

Wote walionielimisha nawashukuru sana, bado naendelea kupokea mawazo zaidi ikiwa yatakuwapo. Ikumbukwe kwamba sijawa peke yangu niliyepatwa na hili kwa NMB, wapo wengi ninaowafahamu, achilia nisiowafahamu. Sikununua hisa hizo shimoni Kariakoo, bali ndani ya benki ya NMB na aliyeniuzia ni mfanyakazi rasmi aliyekaa kaunta mahsusi kwa kazi hiyo. Wazo la kuwauliza NMB lipo siku nyingi tu na nilishawahi kuwauliza nikaambiwa niendelee kusubiri kwani walikuwa bado hawajayafanyia kazi kwa watu wote. Hata hivyo nitaenda tena, sasa hivi nikiwa na mawazo mapya niliyopata kupitia kwenu.
 
Kuna sababu nyingi sana zinazopelekewa watu kununua Hisa, and swala la gawio bado ni decisions za Kampuni Husika, Labda kama you are among Preference shares (ambazo baada ya kampuni husika, faida kwa wana hisa wa preference share hupata gawio lao), though naamini hizi zetu mara nyingi ni za kawaida.

Kutoa gawio au kutotoa ni uamuzi wa kampuni kulingana na taratibu walizoziweka. ( kama wanataka thamani zaidi kwa share (they will pay dividend) or else wanaweza wasitoe.

Elimu zaidi inahitajika ili watu waelewe zaidi Juu na shares.
 
Kuwa na subira, kuwekeza kwenye Hisa yahitaji muda.

Na usiangalie Gawio tu kuna capital gain pia ambayo unaipata bila wewe kufahamu.
 
Back
Top Bottom