Mwenyezi Mungu awabariki marafiki kama hawa.

Mwenyezi Mungu awabariki marafiki kama hawa.

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,905
Reaction score
4,940
Ni mida ya saa kumi na moja saa za jioni kijana anampigia simu rafiki yake na kusema "samahani rafiki yangu ninashida na hela, mama yangu anaumwa na hapa nilipo sina pesa ya matibabu.

Rafiki anajibu "usijali!! Nipigie baada ya mechi saivi nipo kucheki game ya simba na yanga

Baada ya mechi anampigia anakuta sim imezimwa
Kama haamini hivi anapiga tena na tena lakini bado simu haipatikani

Anajaribu kuwatafuta marafiki zake wengine lakini wote wanasema hawana pesa.

Mikono nyuma huku machozi yakimlenga anaamua kurudi hospitalini
Ile anaingia wodini anakuta bahasha ya dawa imewekwa pembeni ya kitanda huku mama yake akiwa amelala

Anamuuliza mdogo wake mdogo wake anajibu "rafiki yako alikuja hapa akachukua maelezo ya daktari kisha akaenda kununua hizo dawa.
Na ametoka hapa muda si mrefu.

Kwa furaha kijana anamfuata rafiki yake na kumuuliza "vip ulikuwa wapi? Mbona ulinizimia simu?"

Kwa upole rafiki anamshika begani kisha anasema "nisamehe sana rafiki yangu sikuwa na pesa hivyo nikaamua kuuza simu yangu kwaajili ya kumnunulia mama yako dawa.

A FRIEND IN NEED IS A FRIEND INDEED.
 
Aiseeee. Huo ndio urafiki japokuwa unaweza fanyika kwa njia nyingine pia na si kwa kuuza simu Pekeee.

Wabarikiwe wote marafiki wa kweli na wazidi kuendelea kuwepo pia tuzidi kushikana kila uchwao pasi kuchokana kwa kuchukulia jambo uzito pindi tupatapo matatizo.
 
Kipindi napiga gambe nilikuwa tajiri wa marafiki kwa sababu ya ofa zangu , ila baada ya kuacha gambe marafiki wote wamenikimbia na nilikuja kuona kuwa sina rafiki wa karibu nilipopata ajali kwani familia yangu tu ndio iliyohangaika na uzima wangu mpaka niliposimama tena..
Leo anakuja mtu from nowhere analalamika shida eti sina kodi ya nyumba nisaidie rafiki yangu, huwa sijibu chochote nakausha tu maana hata mimi nina nyongo...........

Marafiki zangu kwa sasa ni familia yangu na ndugu zangu tuliozaliwa tumbo moja tu wengine watanisamehe kwa kweli.
 
Bahati mbaya sana ni kwamba marafiki wa hivi ni wachache sana!
 
Dah! Watu wa hivi bado wapo karne hii, hilli toleo la marafiki wa aina hii siku hizi hakuna.
 
Back
Top Bottom