Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Gambia akimbilia Nje ya nchi kuhofia Usalama wake.

Gambia aipa kisogo nchi yake
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Gambia, Alieu Momar Njai amekimbia ili kuyanusuru maisha yake katika wakati ambapo hali inatisha katika nchi hiyo ndogo ya Afrika Magharibi. Vituo viwili vyengine vya radio vimefungwa.

36869637_303.jpg

Alieu Momar Njai ndie aliyemtangaza Adama Barrow kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais wa decemba mosi iliyopita, lakini rais Yahya Jammeh amekataa kung'atuka na badala yake kutuma madai mahakamani kwa hoja za udanganyifu. Mpwa wa Alieu Momar Njai, Modou Njai ameliambia shirika la habari la Ujerumani dpa kwamba mjombaake amekimbia kwasababu ya vitisho dhidi ya usalama wake.

"Hakutaka kuondoka....lakini amelazimishwa na familia" amesema Modou Njai.

Kabla ya hapo vikosi vya usalama viliizingira ofisi ya tume ya uchaguzi na kuwakatalia ruhusa ya kuingia ofisi watumishi wa ofisi hiyo kwa wiki kadhaa. Hata hivyo wanajeshi hao wameshalihama eneo hilo hivi sasa.

Chanzo: DW idhaa ya kiswahili
Rais wa gambia kuna taifa kubwa nyuma yake so bure
 
Taarifa za awali zilidai ni kweli alikubali kuachia kiti, tatizo likaja kwa Rais mteule kuanza mbwembwe kwamba atawashughulia viongozi waliomtangulia ambaye anamlenga Jameh, hata ningekua mm sitoki hahah!
Hizo sio sababu. Itakua wale washikaji zake wajeda wale wengi amecheza nao tangia utoto wale wamempa kiburi.. Kwani zanzibar nani alitishiwa kufungwa mbona jecha akatumika.. Africans bado sana na tunatia aibu sasa wafanyakazi tunataabika nchi haina hela maana zanzibar inabidi tuipige tafu wafadhili wamesusa.
 
Taarifa za awali zilidai ni kweli alikubali kuachia kiti, tatizo likaja kwa Rais mteule kuanza mbwembwe kwamba atawashughulia viongozi waliomtangulia ambaye anamlenga Jameh, hata ningekua mm sitoki hahah!

Kwa hiyo msifanye ujinga mnapo pata nafasi cheo ni dhamana
 
Taarifa za awali zilidai ni kweli alikubali kuachia kiti, tatizo likaja kwa Rais mteule kuanza mbwembwe kwamba atawashughulia viongozi waliomtangulia ambaye anamlenga Jameh, hata ningekua mm sitoki hahah!

Hata Mimi navuruga Kete tuanze upya kucheza Draft! Mambo ya Usengerema spendi
 
Viongozi wa Africa wengi wana tatizo la kurithi tabia za kung'ang'ania madarakani hasa nchi zilizowahi kutawaliwa na ufaransa bado sijajua tatizo ni nini hasa.
Usikurupuke, gambia haikutawaliwa na ufaransa Ni waingereza na imekuwa chini ya malkia kama zilivyo jamaica etc.
Itumieni Google vizuri kujisomea ili mkija hapa tufanye uchambuzi yakinifu
 
Na hii kauli ya rais mteule adama barroh ndo imekuwa tisho kwa rais jammeh ila tangu mwanzo nilishangaa imekuwaje.....kimempata nini jammeh dikteta kukubali matokeo ya vigololi kirahisi vile........ila hii tabia ya kungangania madaraka naona viongozi wa afrika wanarithishana kama sio kuambukizana
1324b2e688389fc3c35bd1ff0642708e.jpg

7802c0f909097449cd80991391c44290.jpg

Wakati Jammeh anakubali matokeo nilikuwa nafuatilia twitter,nikakutana na tweet ya huyu jamaa nilicheka sana

Ila ndio kilichotokea
 
Viongozi wa Africa wengi wana tatizo la kurithi tabia za kung'ang'ania madarakani hasa nchi zilizowahi kutawaliwa na ufaransa bado sijajua tatizo ni nini hasa.

Hii inaonyesha Muingereza alikuwa/ni mtawala mzuri(commendable administrator) kwani kote alipotawala he imparted administrative skills kwa hayo mataifa tofauti na Ufaransa.
 
Back
Top Bottom