Sinai
JF-Expert Member
- Jan 20, 2011
- 288
- 47
Katika gazeti la Tanzania Daima, kuna habari inamhusu Jenister Mhagama ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Bunge huduma za jamii. Huyu mama kama mwenyekiti, alikuwa anajaribu kuizuia kamati yake isitembelee kiwanda cha Jambo Plastics, swali langu ni je huyu mama anamaslahi gani na hiki kiwanda? Kwanini ajaribu kufanya jaribio la kuzuia wabunge wasitembelee hicho kiwanda? Au ndo yale yale ya CCM kulinda mafisadi? Naomba kutoa hoja!