Kamati ya Bunge Utawala Yaridhishwa na Jitihada za Mlengwa wa TASAF Wilayani Uyui

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,890
939
KAMATI YA BUNGE YA UTAWALA YARIDHISHWA NA JITIHADA ZA MLENGWA WA TASAF WILAYANI UYUI NA KUMCHANGIA 530,000/= KUMUWEZESHA KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA KUISHI.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo amesema kamati yake imeridhishwa na jitihada za mlengwa wa TASAF Kata ya Magiri Wilayani Uyui, Bi. Amina Abdallah kwa kutumia vizuri ruzuku anayoipokea kuanza ujenzi wa nyumba bora ya kuishi, kitendo ambacho kimewashawishi wajumbe wa kamati hiyo kumchangia fedha kiasi cha shilingi 530,000/= ili kuuunga mkono jitihada za mlengwa huyo.

Mhe. Kyombo amesema hayo akiwa katika Kata ya Migiri Wilayani Uyui mkoani Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya kamati hiyo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika wilaya hiyo.

Mhe. Kyombo amesema kitendo cha Mlengwa huyo wa TASAF Bi. Amina Abdallah kujenga nyumba na kufungua mgabiashara ya kilinge cha kuuza kahawa kimetoa somo la nidhamu ya matumizi ya fedha kwa walengwa wengine licha ya kupata kiasi kidogo cha ruzuku.

Mhe. Kyombo amesema kuwa, kazi inayofanywa na TASAF kwa usimamizi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika kuzikwamua kaya maskini inaonekana kwa macho kupitia namna walengwa walivyoboresha maisha yao.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Jenista Mhagama amesema kitendo cha wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria kuguswa na kumchangia mlengwa wa TASAF, Bi. Amina Abdallah kimezingatia utu na nia ya dhati ya wajumbe wa kamati hiyo kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita za kuboresha maisha ya kaya maskini nchini kupitia TASAF.

Aidha, Mhe. Mhagama amuelekeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa nyumba ya mlengwa huyo wa TASAF inakamilika kwa wakati na kuahidi kuwa atarejea tena katika makazi ya mlengwa huyo ili kujiridhisha na utekelezaji wa maelekezo yake.

Naye, Mlengwa huyo wa TASAF Bi. Amina Abdallah amesema, ruzuku ya TASAF imemuwezesha kujenga nyumba bora ya kuishi.

WhatsApp Image 2023-03-15 at 23.40.58.jpeg
FrP8vItXwAE-nu8.jpg
FrP8qnVXsAAgSfw.jpg
WhatsApp Image 2023-03-15 at 23.40.59(1).jpeg
 
Back
Top Bottom