Mwenyekiti wa CCM Rais Samia aongoza kikao cha Kamati kuu, je askofu Gwajima na Polepole wamepona?

Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa JMT mh Samia leo ameongoza kikao cha kamati kuu ya chama hicho Chamwino nje kidogo ya jiji la Dodoma.

Je, askofu Gwajima na Komredi Polepole na yule wakili msomi Jerry Slaa wamepona?

Tusubiri taarifa rasmi ya mwenezi komredi Shaka.
Shaka mropokaji na kujipendekeza ndio wanasababisha hali ya sintofahamiana ccm. Kama wamebadili itikadi na sera za ccm baada ya kuaga dunia magufuli watuambie kikao gani kinahusika. Wanachama wenye kukijua chama wanasimamia falsafa ya kimapinduzi ujamaa. Sasa hawa wenye kujaribu kuuza kwa mara ya pili mashirika muhimili wa uchumi kama tanesco wametoka wapi na nani anawaleta. Mashirika kama tanesco ttcl trc atc uda/udart kwanza hayauziki kwani waliyowahi kujidai kununua walitaka kuyaiba tu bila kulipa thamani yake. Huwezi fanya biashara kwa faida bila kukwaza maendeleo kwa kugeuza huduma ya mashirika haya biashara kabisa. Magufuli amefanya kazi kubwa kuyarejesha hayo mashirika na kuhakikisha yanaendeshwa kwa tija sasa wajanja wamekuja wanajifanya hawaoni ufanisi wanataka kufanya wizi kwa mara nyingine.
 
Duuh yule jamaa japo kuna kipindi alikuwa anasanua mambo ya kweli lakini kwa upande mwingine ni jitu la hovyo sana
Nilivyosikia ile sauti yake kwenye ile clip nilishangaa sana, nikasema kumbe ni rahisi mtu kujiingiza mwenyewe nyavuni.......nahisi alikuwa anatumika na watu waliomo kwenye security system hapa nchini.....
 
Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa JMT mh Samia leo ameongoza kikao cha kamati kuu ya chama hicho Chamwino nje kidogo ya jiji la Dodoma.

Je, askofu Gwajima na Komredi Polepole na yule wakili msomi Jerry Slaa wamepona?

Tusubiri taarifa rasmi ya mwenezi komredi Shaka.
Baada ya kifo cha Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Mhe. William Ole Nasha, moshi mweupe unaenda kutoka tena ikulu kwa staili ile ile ya "yure mupe, yure muruke"

Jicho lote sasa ni kwa Ridhiwani Kikwete ama Nape Nnauye. Ramli ya kisiasa inaonyesha tutegemee pia kuona mabadiliko mengine makubwa hata katika wizara zingine kubwa mbili ama tatu hivi. Mh! Mambo ya ndani na.....!

Kumbuka kuwa Madam President alikwisha sema kuwa aliweka tu kituo kidogo wakati ule, kwa hiyo nukta nukta bado kabisa hajaifikia. Kanda ya ziwa lazima muendelee kununa kwa mara nyingine tena.
 
Mtu anashindana na taasisi....taasisi yenyewe ni CCM....Khaaa 😳😳😳😳🤣

Ukweli una kawaida ya KUPANDA NGAZI ....MDOGOMDOGO......

#SiempreCCM
#NchiKwanza
 
Mwenyekiti wa CCM ambaye ni Rais wa JMT mh Samia leo ameongoza kikao cha kamati kuu ya chama hicho Chamwino nje kidogo ya jiji la Dodoma.

Je, askofu Gwajima na Komredi Polepole na yule wakili msomi Jerry Slaa wamepona?

Tusubiri taarifa rasmi ya mwenezi komredi Shaka.
Mbowe sio gaidi

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Wacha wafu wazikane. Kufukuzwa kwa Gwajima na Polepole hakutafanya maisha yawe mepesi kwa Mtanzania wa hali ya chini. Ikiwa tozo na mifumuko ya bei ipo pale pale, tofauti pekee tutakayoiona ni aidha CCM kuondoka madarakani ama kupata katiba mpya.
Mpaka hilo litokee hata wakimfukuza Samia mwenyewe sawa tu.
Kuendelea kuwaamini ccm kwa sasa ni sawa na kumwamini Daktari mfanyabiashara wa majeneza akutibu.
 
Back
Top Bottom