Mwenyekiti wa CCM Dr. Magufuli kukiuka agizo la Rais, kufanya mkutano Kahama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,244
103,937
Mwenyekiti wa CCM Rais Magufuli, ameonekana kukiuka agizo la Rais Magufuli la kukataza kufanya siasa majukwaani.Imeripotiwa kuwa rais anategemea kufanya mkutano mkubwa wa kisiasa mjini Kahama kuwashukuru wananzengo kwa kumchagua kwa kura nyingi!!Aidha ikumbukwe kuwa wabunge wawili wa UKAWA walishikiliwa na polisi kwa kufanya mikutano ya hadhara....Mungu ibariki UKUTA,Mungu ibariki UKAWA

Huu ni Mkutano wa Kisiasa kwa sababu kuwashukuru wananchi kumchagua kuwa Rais chini ya CCM, ni siasa. Hiyo ni kinyume na agizo lake la kutokufanya siasa mpaka 2020 akisaidiwa na policcm. Huku kunaitwa kukurupuka na kujichanganya.
Basi na Wapinzani nao wafanye Mikutano ya hadhara kuwashukuru wananchi kuwachagua kuwa Wabunge na Madiwani na kumpa Mgombea Urais kura milioni 6 ambazo ni nyingi zaidi ya alizopata Kikwete 2010.

JPM baba vipi, mbona unajikanganya?


MY TAKE
Kwa kuwa ni mkutano wa kisiasa kinyume na katazo la Rais Magufuli, hakuna haja sasa ya BAVICHA na UKUTA kusaidia polisi kuhakikisha agizo la Rais linatekelezwa? Polisi wa Mara iliwashikilia wabunge wa UKAWA Mara kwa kufanya mkutano. Polisi wa Shinyanga/Kahama toeni tamko mapema. BAVICHA toeni tamko la kusaidia polisi
 
Wabadili gia angani mtaweweseka sana awamu hii.. RAIS TULIYEnaye Watanzania ndio tunamskia yeye na chama chake nyie wengine na mafisadi wenu tupishen

Hahahaha naona unaota ndoto!! Ivi ni watanzania gan wanaomsikia magu kwasasa nihawa mama ntilie, machnga na bodaboda wanafukuzwa na kuporwa mali zao na polis kila siku? Au kuna wengne? Mkuu unaweza ukawa peko yako.
 
hahahaha naona unaota ndoto!! Ivi ni watanzania gan wanaomsikia magu kwasasa nihawa mama ntilie, machnga na bodaboda wanafukuzwa na kuporwa mali zao na polis kila siku? Au kuna wengne? Mkuu unaweza ukawa peko yako

Aaah wp... Wewe ndio uko tofauti na sisi
Kwa Taarifa yako Watanzania wengi wanyonge tumeshukuru kumpata magufuli kwani wazi wazi ameonyeshwa kukerwa na vitendo viovu... Upinzani mlikosea sana kuwapa chama chenu mafisadi


Hapa kazi
 
Jamaa anawaogopa sana wapinzani, demokrasia ni kukosoana ili mambo yaende
"Kukosoana" kwa mikutano ya hadhara na maandamano, ndiyo "demokrasia", karne hii! Kichekesho cha mwaka.

CHADEMA tuacheni Watanzania tujenge nchi yetu. Mna wabunge na halmashauri kadhaa mnaongoza, hamasisheni maendeleo mjijengee imani na heshima kwa wananchi.

LAKINI ya UKUTA ni uchochezi na bila shaka mtapambana na vyombo vya salama.
 
Ujinga wenu ni kuamin kuwa kila asiye upande wenu mafisadi wa chadema basi atakuwa team lumumba..... Kwa taarifa yako tupo mamilion ya Watanzania tusiye na chama ila tu namuunga mkono baba magufuli..... Go on Mr president
Usiwaongelee watu...Hayo mamilioni umefanya lini sensa?

Sema tu wewe upo upande fulani...Mkuu binadamu watu wa ajabu sana mkuu!!Halafu unafikiri kuna watu hawampendi JPM?Watu wananung'unika huku kuwabana bana "wenzie wanasiasa"...Mimi ni mmoja wa watu wanaokubali sana harakati za huyu jamaa,ila ili ya kukimbizana na "Vi-UKAWA" ni kama anajishushia pumzi...

Unajuwa mtu mwenye tumbo la kuja.mba ni kumiacha ajambe hewa chafu itoke...Akiitoa anakuwa huru,hata kama kujamba kwake hakujamaliza tumbo lake kuuma...Angewaacha tu hawa jamaa wabweteke,wafanye siasa...Raia tutaona tu maendeleo kimyakimya!!Asikimbizane na Vyama...Binadamu hutafuta kile anachokosa hata kama kinapatikana kwa tabu
 
Ujinga wenu ni kuamin kuwa kila asiye upande wenu mafisadi wa chadema basi atakuwa team lumumba..... Kwa taarifa yako tupo mamilion ya Watanzania tusiye na chama ila tu namuunga mkono baba magufuli..... Go on Mr president
Tatizo ni pale unapokuwa na mawazo tenge ...na kujitoa ufaham kuwa zuzu.....japo unamacho huoni masikio pia wala huoni....Nyie wote ni Lumumba buku saba mnakana tu.......hao mafisadi wafikisheni mahakamani...........tunataka wale wa Escrow ,richmond,meremeta, kiwira na lugumi wafikishwe mahakamani sio kuja kuanza kullamika humu kama wehu.....mwambieni Mwakyembe ...ile mahakama ya mafisadi ianze na hao...........na ikimaliza ije kwa wale wezi wa mali za chama .....jana mkuu alikuwa anawaongelea.....
 
  • Thanks
Reactions: J C
Mwaka huu tutaona mengi...misukule ya lumumba itakuja humu.....na kuanza kutetea upuzi.....
Tumeona na kusikia mengi, tupo palepale kwa sababu ya siasa za unafiki, km:
1) Orodha ya mafisadi
2) Operesheni Sangara
3) Movement for change
4) UKAWA
5) Mabadiliko ya kuzungusha mikono
6) Mbendebende chaliiiii, nk
7) sasa ni UKUTA

DU!!!! TAFAKARI CHUKUA HATU
 
Amakweli miaka mitano tumepatikana yaan Rais anaanza kufanya mikutano ya kisiasa, ntashangaa kuona hvyo....
 
Rais John Magufuli anatarajia kufanya ziara wilayani Kahama mkoani Shinyanga ambako atafanya mkutano wa hadhara kuwashukuru wananchi kwa kumpigia kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliopita.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkulu alisema jana kwamba Rais Magufuli atawasili Kahama Jumamosi jioni kabla ya kufanya mkutano wa hadhara Jumapili.

Nkulu aliwataka wananchi wa Kahama na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi kumlaki kiongozi huyo katika ziara hiyo ambayo alisema: “Lengo lake ni kuwapongeza wananchi wa Kahama kwa kumpa kura nyingi katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika mwaka jana"

Chanzo: MWANANCHI
 
Siku zote unapozungumza katazo fulani jiangalie kwanza wewe Kama utaweza kutekeleza hilo katazo lako.

Bila shaka hapo "mtukufu" wetu atakuwa anaenda kinyume na katazo lake(mikutano ya kisiasa) ...Siasa ni mikutano huwezi ukafanyia siasa chumbani.
 
Back
Top Bottom