Gamba Jipya
JF-Expert Member
- Apr 16, 2011
- 401
- 80
Nilimfahamu Emmanuel Makaidi wakati ule (1993) tukijaribu kuhamasisha Wananchi wajiunge na vyama vyetu vipya: yeye akiongoza NLD na mimi CHADEMA. Namshukuru kwamba sasa ameona umahiri wa vijana walioridhi mikoba yetu.
Kabla sijataafu kama Mwenyekiti nilijaribu kukaribisha waliokuwa na misimamo iliyofanana fanana na yetu ili tuimarishe upinzani dhidi CCM, hata tukafikia kuunda "UDETA" (Umoja wa Demokrasia Tanzania), lakini wahasimu wetu wakatu-derail. Ni furaha ilioje kwangu kwamba hivi karibuni Mabere Marando ametuunga mkono, na namkaribisha Emmanuel Makaidi afikirie uwezekano wa kuimarisha chama cha wazalendo wanaojali kwa dhati maslahi ya taifa lao na watu wake.
Demokrasia na maendeleo ya kweli yatapatikana Tanzania tukiweza kuondoa ukiritimba wa CCM ktk uongozi wa nchi hii; na inaonekana sasa itawezekana hasa kama Mheshimiwa Makaidi na wafuasi wake watajiunga nasi pia.
Shikamoo Mzee,
Je unazungumziaje urudishwaji wa nyumba za serikali?
Naomba maoni yako.