Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa aimwagia sifa CHADEMA: | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa aimwagia sifa CHADEMA:

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Apr 18, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti wa baraza la vyama vyote vya siasa nchini Bwana Emmanuel Makaidi ameimwagia sifa kibao CHADEMA kwa kile alichodai ni mapambano yake ya kuondoa mswada wa katiba uliowasilishwa bubgeni.

  Makaidi ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha NLD Taifa amelieleza gazeti la Nipashe kwamba vita ya CHADEMA ndiyo iliyofanikisha serikali kusalimu amri.

  Alisema amevutiwa na viongozi wa CDM kwa jinsi wanavyoendesha mapambano ndani na nje ya bunge.

  Makaidi ambaye ametoka kwenye ziara ya chama chake mikoa ya kusini amedai kwamba kwa utafiti wake aliofanya amebaini asilia 80 ya wananchi ni wafuasi wa CHADEMA.

  Amedai anaamini ufuasi wa wananchi kwa chama hicho si kingine ila harakati zao zinazoonekana kuungwa mkono na watanzania wengi.

  Bwana Makaidi amesema hajatumwa na mtu yeyote kusema hayo ila ukweli usemwe hata kama ni mchungu kwani ndicho alichoshuhudia mikoani.

  SOURCE:SOMA NIPASHE LA LEO UKURASA WA NDANI
   
 2. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Huu ndio ukomavu..........kukubali kile anachofanya mwenzako na matokeo yake katika harakati zao

  Sio wale wengine wanakazi ya kutunga mashairi ya taarabu na kuimba tu..........

  Hope Lipuz na wenzako mmemsikia Makaidi japo najua mtakuja na hoja anajikomba aitwe CDM...

  Hongera Bwana Makaidi, walau umezungumza kwa utafiti wa Ziara yako Mikoani kitu chenye mashiko kuliko wanaopinga tu kikasuku....
   
 3. Dullo

  Dullo JF-Expert Member

  #3
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 24, 2009
  Messages: 252
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni ishara nzuri sana kwa kuonyesha ukomavu wako Bwana Makaidi, Bugup
   
 4. m

  mwanza_kwetu JF-Expert Member

  #4
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 684
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Thanks; umeona mwezi sasa Makaidi; huo ndio ukweli ila kwa CCM watakuwa wagumu sana kuu-swalow
   
 5. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #5
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ni tathmini nzuri sana, kwamba hatimaye mtu ambaye si wa CDM amekiri kuwa kuondolewa kwa muswada ule ni matokeo ya harakati za CDM... nadhani ukweli huu ulikuwa unafahamika na wale waliokuwa wanapiga meza siku ile mjengoni na kuimba....
  Ukweli huu utaendelea kusambaa kwa kadri tunavyoelekea kwenye katiba mpya!
   
 6. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #6
  Apr 18, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  atleast wameanza kuongea,ila wana chadema wasivimbe kichwa ila wachukue kama motisha kwao
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,966
  Trophy Points: 280
  Demokrasia imeanza kumea ndan ya mioyo ya wafalme[serikal]
   
 8. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #8
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Tungekuwa sote tuko hvi maskini nchi yetu isingekuwa maskin,YEEEES!tunahitaji watu waliotayari kuappreciate na kuzikubali hoja zenye ukweli hata kama zinatoka vyama mbadala,siyo wale wenzetu wenye kusema NDIYOOOO,hata wakiambiwa Tanzania iuzwe wanaendelea kusema NDIYOOOO, PUMBAVU ZAO,WANAFIKI WAKUBWA
   
 9. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  big up, good analysis
   
 10. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante mzee kwa kufanya kama tulivyokubaliana, uzuri ni kwamba kati ya hiyo asilimia 80 waliojiandisha kwenye daftari ya kudumu la wapiga kura ni asilimia 4 TU, na wanaopiga kura ni chini ya asilimia 2.
   
 11. Criss

  Criss JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 825
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwanza nimpongeze huyu Ndugu Emmanuel Makaidi kwa kuonyesha kua anajitegemea kiakili kwa kupongeza na pengine hata kukosoa patakapo stahili na najua huu ni mwanzo tu kwa heshima na umakini wa Chama,Viongozi hadi wanachama waChadema siku itafikia siku hata wale wavaa jezi wataikana CCM yao hadharani.
  Kubwa tunalo jivunia CHADEMA hatuendeshwi na sifa wala hatuvunjwi moyo na siasa za maji taka sisi tunachoangalia mahitaji ya msingi kwa jamii yetu yanatekelezwa?
  Haki za msingi zina zingatiwa?
  Na tukiona ndivyo sivyo tatapambana hadi kieleweke.
  NB:_Nampongeza kwa kuonyesha ukomavu kifikra na kama ana maanisha basi ni hatua nzuri kwake.
   
 12. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #12
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  NLD yaifagilia Chadema kuondolewa bungeni muswada wa Katiba mpya
  Na Romana Mallya  18th April 2011


  [​IMG]
  B-pepe  [​IMG]
  Chapa  [​IMG]
  Maoni
  [​IMG]
  Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi  Mwenyekiti wa Chama cha National League for Democracy (NLD), Dk. Emmanuel Makaidi, amesema kuondolewa kwa muswada wa kuundwa kwa tume ya kuratibu maoni ya Katiba mpya bungeni kumetokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
  Dk. Makaidi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini, alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kufika kwenye ofisi za NIPASHE zilizopo Mikocheni, jijini Dar es Salaam.
  Alikuwa akitoka katika ziara ya mikoa ya Mtwara na Lindi ambapo alisema ameamua kuipongeza Chadema kutokana na kuguswa na kazi nzuri inayofanywa hivi sasa na chama hicho ndani na nje ya Bunge.
  "Nimekuja hapa kulizungumzia hili sijatumwa na mtu, chama wala kikundi, Chadema wamenikuna endeleeni na kazi nzuri mnayoifanya kwa faida ya Watanzania, sio kawaida yangu kusifia lakini kwa hili nimeguswa, naongea hivi kama mwenyekiti wa chama changu lakini pia kama mwenyekiti wa vyama vyote nchini, " alisema na kuongeza:
  "Chadema msivunjike moyo kwa vitisho vya CCM kwa sababu kupitia utafiti wangu nilioufanya hivi karibuni kwenye mikoa hapa nchini nimebaini kuwa, mnaungwa mkono kwa asilimia 80 na Watanzania kuhusiana na jitihada zenu za kupigania maslahi ya wananchi, atakayebisha hili nitashindana naye kwa takwimu tu, mimi ni msomi hivyo siropoki," alisema.
  Dk. Makaidi alisema muswada uliotaka kupitishwa ili kuunda tume ya Katiba mpya ulilenga kuwasaliti Watanzania lakini jitihada zilizofanywa na Chadema ndizo zimesaidia kuuondoa bungeni na kuurudisha kwa wananchi.
  "Chadema kama Kambi Rasmi Bungeni kikiongozwa na kiongozi wake, Freeman Mbowe, kimefanya muswada huo kufa kifo cha mende, sitegemei kama muswada huu utarudishwa tena bungeni labda uje ukiwa na maudhui mapya," alisema.
  Akitoa maoni yake kuhusiana na mchakato huo unaoendelea hapa nchini kwa sasa, alisema wakati raia duniani wanataka kuhodhi mamlaka za nchi zao muswada ulikuwa unataka kuweka mamlaka hizo mikononi mwa Rais wa Tanzania.
  "Haya ni makosa na usaliti wa umma wa Watanzania, ombi langu kwa viongozi wa CCM na serikali yao, wajifunze kupitia matukio yanayotokea ulimwenguni kwa sasa, pamoja na nchi za Kifalme na Kiarabu kutaka kuhodhi mamlaka za nchi lakini wananchi wake wanataka kuziendesha kwa maslahi ya watu wote sio kikundi," alisema.
  Kutokana na upinzani mkali uliotokana na kelele, ukosoaji na vilio vya umma dhidi ya muswada huo, Ijumaa iliyopita serikali ililazimika kuuondoa kwenye orodha ya kuwasilishwa katika mkutano wa Tatu wa Bunge.

  :: IPPMEDIA
   
 13. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #13
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0


  Tutakachofanya ki kubadilisha lugha tu, kutoka kiingereza kwenda kiswahili lakini vifungu vyote vitabaki vile vile, na hili tulilijua toka mwanzo na hatukufanya bahati mbaya kuuweka kwa kiingereza.
   
 14. Y

  Ye Nyumbai Senior Member

  #14
  Apr 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu ndiye mwanasiasa na mpinzania wakweli anyeongea ukweli pale inapostahili,sio huyu mke wa ccm CUF kazi kumsifia mume waki hali akijua hafai kuitwa mume.

  Dk Makaidi ameongea kiume hasa!!!
   
 15. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #15
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135

  Ukweli utabaki kuwa ukweli, hakuna cha makubaliano hapa - hata hiyo analysis yako waliojiandikisha kupiga kura na watakaopiga kura inaonekana ni uchakachuaji wa hali ya juu (cdm ilipata kura zaidi ya mil 2 mwaka 2010 ambayo ni sawa na aslimia zaidi ya 5)
  unachakachua mchana kweupe, wewe endelea kujipa matumaini na takwimu za kiuchakachuaji lakini muda utakapofika utajionea mwenyewe
   
 16. E

  Edwin Mtei JF Gold Member

  #16
  Apr 18, 2011
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 181
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nilimfahamu Emmanuel Makaidi wakati ule (1993) tukijaribu kuhamasisha Wananchi wajiunge na vyama vyetu vipya: yeye akiongoza NLD na mimi CHADEMA. Namshukuru kwamba sasa ameona umahiri wa vijana walioridhi mikoba yetu.

  Kabla sijataafu kama Mwenyekiti nilijaribu kukaribisha waliokuwa na misimamo iliyofanana fanana na yetu ili tuimarishe upinzani dhidi CCM, hata tukafikia kuunda "UDETA" (Umoja wa Demokrasia Tanzania), lakini wahasimu wetu wakatu-derail. Ni furaha ilioje kwangu kwamba hivi karibuni Mabere Marando ametuunga mkono, na namkaribisha Emmanuel Makaidi afikirie uwezekano wa kuimarisha chama cha wazalendo wanaojali kwa dhati maslahi ya taifa lao na watu wake.

  Demokrasia na maendeleo ya kweli yatapatikana Tanzania tukiweza kuondoa ukiritimba wa CCM ktk uongozi wa nchi hii; na inaonekana sasa itawezekana hasa kama Mheshimiwa Makaidi na wafuasi wake watajiunga nasi pia.
   
 17. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #17
  Apr 18, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 12,000
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Safi kabisa
  Wameuona ukweli,na sasa wanatoa pongezi,YEEEP.
   
 18. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #18
  Apr 18, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  I wish i could there to share that happiness and smile in your face baada ya kusoma post hii.........i can feel the happiness in you mzee kwa kuanza kuona matunda ya kazi yako

  Tunakuombea maisha marefu ushuhudie vijana wakiendeleza ile kiu yako ya wakati ule.......

  Wish to see UDETA alive japo najua ni ngumu maana wengi sasa wanaangalia matumbo zaidi ya future ya tanzania yetu

  Hongera kwa kazi nzuri Mzee Mtei na waambie vijana waongeze juhudi na wasibweteke wala kuogopa na kutishika na maneno ya majambazi wachache wa Tanzania yetu
   
 19. M

  Marytina JF-Expert Member

  #19
  Apr 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,035
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  You have played ur part, Hongera sana Mzee, mawazo yako yamemea vichwani mwetu it is just a matter of time kuna siku hii nchi itabadilika
   
 20. G

  Gamba Jipya JF-Expert Member

  #20
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 403
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna watu wanadai hiki chama ni mali ya mtu fulani, lakini mara zote nimekuwa na nguvu zakukataa....

  Your autobiography was amazing, kudos
   
Loading...