Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Elia Juma Kidavile, ametoa wito kwa vijana wa kuwanenea viongozi wao mazuri kutokana na juhudi kubwa wanazozifanya katika kuleta maendeleo kwa wananchi. akiongeza kuwa viongozi hao wamekuwa mstari wa mbele katika utekelezaji wa miradi mbalimbali , ikiwemo katika sekta za elimu, afya, na jamii, ambayo imesaidia kuboresha maisha ya wananchi.
Kidavile ameyasema hayo leo tarehe Aprili 3 , 2025 alipokuwa akizindua shina la bodaboda la UVCCM kata ya Mboliboli, tarafa ya Pawaga, Wilaya ya Iringa. Uzinduzi huo ni sehemu ya ziara ya kamati ya utekelezaji ya UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini.