Rucho Ongiri
Member
- Dec 23, 2011
- 7
- 3
Mie nadhani hoja siyo aliyeteuliwa anatoka kabila gani, shemeji, mkwe, mume, kaka, mjomba au ndugu wa nani. Hoja ni je, pamoja na sifa anao uwezo kifikra, kimaadili na nguvu kimwili wa kutekeleza majukumu yake katika kipindi hiki cha www.com.
Huu ndio mjadala tunaotakiwa kuwa nao. Mwanzoni mwa mwaka huu niliwahi kuandika makala katika gazeti moja magazeti ya kila siku ya Kiswahili nchini nikielezea baadhi ya matatizo yanayolikabili Taifa letu changa (tumeadhimisha miaka 50 juzi, kwa Tanganyika), kuwa ni nafasi nyingi za uteuzi kutawaliwa na siasa yetu kushikiliwa na wastaafu ambao huchukulia vyeo na nyadhifa wanazokabidhiwa kama sehemu ya kujipumzisha baada ya kazi ngumu serikalini au kwenye ashirika na taasisi za umma.
Viongozi na wanasiasa wastaafu hawajishughulishi kuchangamsha bongo zao wala hawana rekodi (Legacy) wanayolenga kuacha nyuma yao katika majukumu mapya wanayokabidhiwa baada ya kustaafu. Hawa mara nyingi hawataki matatizo na watu wala hawapendi mijadala mikali yenye changamoto. HIVI KAMA JAJI MAKAME KACHOKA, JE, LUBUVA NDIYE MBADALA YAKE MWENYE NGUVU YA KUHIMILI CHANGAMOTO ZILIZO MBELE YA NEC ? Tujadili....