Mwenyekiti NEC ni Shemeji wa Lowassa - Janga kubwa sana

tatizo sura zile zile pasco, yaani tanzania hakuna vichwa vingine?????? hasira ahgaaa!!!! mara mia ningesikia mkuu pasco, au mwanakijiji or fair player au waberoyo or kimbunga kaa!! changes we need more!!
Mkuu mabadiliko ya kweli yatatokana na katiba. Kenya baada ya katiba mpya wana mwenyekiti wa tume kijana wa miaka 40 yaani ameibadili tume kabisaaa. Mambo yote sasa hivi ni .com. Vituo vinafungwa saa kumi na mbili matokeo rasmi saa mbili usiku siku hiyohiyo (uchaguzi mdogo). Hakuna cha kuuliza Harambee house (magogoni) kwamba watangaze ama la. Kama umebwaga uwe wa chama twawala ama pingamizi unachanwa live.

Kuongoza tume ambayo haiko huru utaishia kukosa uhuru!
 
Mwenye sifa kama za Jaji ni anayeweza kuteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu. Wako wengi hawa, mfano, hawa wanaoitwa Mawakili wa Kujitegemea( maana yake siijui!), Mawakili wa Serikali, Wanasheria waandamizi, ...

Kwa hiyo mkuu unataka kusema kwamba jaji mstaafu hana sifa ya kuwa jaji? Nadhani nikuelewe hivi jaji mstaaafu alikuwa jaji na akiwa jaji angestahili kuwa mwenyekiti wa tume sawa na ambao wana sifa za kuwa jaji kama ulivyowataja. Lakini baada ya kustaafu si jaji tena na hawezi kuwa na sifa ya kuwa jaji kwa kuwa amestaafu na hawezi kurudia ujaji ndio maana anaitwa jaji mstaafu na si jaji! Kuna umuhimu wa kupata tafsiri ya mahakama. Huenda kuna makosa ya kisheria kiwateua majaji wastaafu.
 
Nikiwa natoka sherehe za Noel Bethlehemu nimekutana na jaji mmoja maarufu nchini katika ndenge tuliyosafiri pamoja kurudi nyumbani , katika mazungumzo yake ameniambia amekerwa sana na uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa NEC bwana LUBUVA kuwa ni mkakati wa Kikwete kumuandalia fisadi mwenzake katika chama chochote atakachokwenda kushinda uraisi. Mambo ambayo ameyafanya ni kumchagua Lubuva AMBAYE NI KAKA WA MKE WA LOWASA kufanikisha hilo.

Lingine aliloniambia ni kuwa kulikuwa na mkakati wa kumchoma sindano ya Mionzi Dr.Slaa wakati alipoenda kutibiwa mkono muhimbili, na kuwanyamazisha wote wanaompinga.

Zaidi akaniambia kuwa mahakama hapa TZ inaogozwa na CCM na si serikali na wala haiwezi kuwa huru kwenye kesi yenye maslahi na CCM

Binafsi nimesikitika sana ,WADAU kama kuna mtu ana habari zaidi juu ya hii mada atujuze ili tuitazame nchi yetu itakuwaje huko mbeleni

Can you believe the source?
 
Tatizo ni JK. Hakuna lolote analolifanya,likawa na credibility na ya 100%. Yaani likakosa elements za usanii au uchakakachuaji ndani yake. Haiwezekani kwa hili la Lubuva atakuwa amecheza tayari mchezo wake
 
Tena bwana Pasco ni jambo la kushukuru sana kuwa mteuliwa wa nafasi hiyo ni mkristo maana kama angekuwa ni mwislamu tungeanza na uislamu wake then ndio mambo ya ukaribu na Lowasa ndio yangefuata

lakini kwa kuwa yupo upande wa Dini yetu sasa tunatafuta vigezo vingine vya kumsema na kumkataa.

nadhani tusitake kila kiongozi ateuliwe kwa matakwa yetu sisi,ndio maana tumepewa nafasi ya kuchaguwa wabunge lakini baada ya mwezi tunawashushia lawama hao tulio wachaguwa,ikimaanisha chaguo letu halikuwa sahihi,je juu ya hilo nani wa kumlaumu mwenzake? maana Mh Raisi tupo wa kumlaumu,vipi juu ya hao tuwachaguao sisi wenyewe?
 
Mkuu mabadiliko ya kweli yatatokana na katiba. Kenya baada ya katiba mpya wana mwenyekiti wa tume kijana wa miaka 40 yaani ameibadili tume kabisaaa. Mambo yote sasa hivi ni .com. Vituo vinafungwa saa kumi na mbili matokeo rasmi saa mbili usiku siku hiyohiyo (uchaguzi mdogo). Hakuna cha kuuliza Harambee house (magogoni) kwamba watangaze ama la. Kama umebwaga uwe wa chama twawala ama pingamizi unachanwa live.

Kuongoza tume ambayo haiko huru utaishia kukosa uhuru!
Yule kijana sijui ana asili ya Usomali. Anafanyakazi nzuri sana. Kenya ina UKABILA wa hali juu sana lakini kijana huyu ameimudu vizuri tume ile. KATBA yao ni nzuri kwa kweli. Kuteuana kishikaji, kirafiki, kindugu, kimtandao, kumekwisha kabisa.
Tungeichukua tu KATIBA ile na kubadili pale inapotaja Kenya tuweke Tanzania halafu tukabaki na machache ya Zanzibar na Muungano.
 
Mkuu naunga mkono hoja ya NEC kuongozwa na mtanzania mwenye taaluma nyengine, kwa mfano uganda mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ni mhandisi.

Kitu ambacho sina uhakika na ningependa uthibitisho ni kama kweli sheria inataka mwenyekiti wa NEC awe mwanasheria.
Sio tu mwanasheria tena jaji mstaafu mzee aliyechoka ambaye anatakiwa kupumzika na kuwa adviser
 
Yule kijana sijui ana asili ya Usomali. Anafanyakazi nzuri sana. Kenya ina UKABILA wa hali juu sana lakini kijana huyu ameimudu vizuri tume ile. KATBA yao ni nzuri kwa kweli. Kuteuana kishikaji, kirafiki, kindugu, kimtandao, kumekwisha kabisa.
Tungeichukua tu KATIBA ile na kubadili pale inapotaja Kenya tuweke Tanzania halafu tukabaki na machache ya Zanzibar na Muungano.

Kijana ni mkenya mwenye asili ya somalia ila siyo kama mzee wa TBR.
 
Kwa hiyo mkuu unataka kusema kwamba jaji mstaafu hana sifa ya kuwa jaji? Nadhani nikuelewe hivi jaji mstaaafu alikuwa jaji na akiwa jaji angestahili kuwa mwenyekiti wa tume sawa na ambao wana sifa za kuwa jaji kama ulivyowataja. Lakini baada ya kustaafu si jaji tena na hawezi kuwa na sifa ya kuwa jaji kwa kuwa amestaafu na hawezi kurudia ujaji ndio maana anaitwa jaji mstaafu na si jaji! Kuna umuhimu wa kupata tafsiri ya mahakama. Huenda kuna makosa ya kisheria kiwateua majaji wastaafu.
Jaji anabaki kuwa Jaji hata akistaafu au kuteuliwa kwenye nafasi nyingine kwa mfano AG wetu wa sasa bado ni Jaji. Sipingi uteuzi wa Lubuva hata kama angekuwa baba ya Lowasa. Sifa anazo lakini amechoka!
 
Mkuu AG anaitwa Jaji Werema. Mwenyekiti NEC anaitwa Jaji Mstaafu Lubuva. Hicho kisifa cha mstaafu kinanipa shida
 
Damian Lubuva ameshachoka sana - Hafai kuwa "kiongozi" wa chombo chochote cha serikali au public for that matter!
 
Mtolewa, na radhi za usalama wa taifa, jw, jeshi la polisi, raisi, wanawake na wazee na wanaume suruali wasio weza kufanya maamuzi sahihi pale wanapo pewa kofia, tishet na ubwabwa ambao ndiyo wengi zaid
 
Mkuu AG anaitwa Jaji Werema. Mwenyekiti NEC anaitwa Jaji Mstaafu Lubuva. Hicho kisifa cha mstaafu kinanipa shida
Hicho kisifa hakimwondolei sifa ya Ujaji na hivyo kuwa Mwenyekiti wa Tume hii. Umri na afya yake ndivyo vinanitatiza mimi. Yupo Makamu na MaCamishna wengine watamsaidia angalau tufikie KATIBA MPYA.
 
Huyu wa Tabora hana shule. Tapeli na mwizi wa kawaida tu. Bastola yake ya Igunga alirudishiwa?
Kwani walimpoka chombo chake cha ulinzi? Nitapita pale Saigon nimuulize nikimkosa hapo najua atakuwa pale mtaa wa kaluta tabora anacheza bao!
 
Nakubaliana na wewe ktk uandaaji wa safu,ni kweli juu ya hilo Watz tunaweza kuliongelea lakini bado sina hakika kama malengo ya Mh Raisi ni kumwandalia njia Mh E Lowasa kwani mpaka sasa hatuna hakika kama huyu bwana atagombea hiyo nafasi ama la,maana waliowengi wanasema Raisi ajae ni kutoka upande wa pili wa Tz,kwa hiyo mantiki ya lubuva kuwepo pale kwa ajili ya lowasa bado yawezekana ikawa ama isiwe tusubiri mda ukifika tutaelewa tu

Heeeeh! haya makubwa.... hivi urais kimekua kitu cha kuangalia mtu anatokea pande zipi? this is nonsense tunahitaji rais atakayetukwamua na hili lindi la shida na umaskini na sio mtu baki tu kisa katoka pande za pili.. this is stupidity wanaotetea huu ujinga na washindwe!:nono:
 
duh mkuu huyo jaji amepata wapi umaarufu wakati anasema mahakama inaongozwa na ccm!

haya mambo yako wazi,jamaa mbona kajaza ndugu na marafiki, kawambwa mpwa ghasia ndugu mama salma! Na wewe taja wa kwako, ni msululu mrefu hadi waliomsaidia kushinda, imagine wasimamizi wa kura!
 
Tena bwana Pasco ni jambo la kushukuru sana kuwa mteuliwa wa nafasi hiyo ni mkristo maana kama angekuwa ni mwislamu tungeanza na uislamu wake then ndio mambo ya ukaribu na Lowasa ndio yangefuata

lakini kwa kuwa yupo upande wa Dini yetu sasa tunatafuta vigezo vingine vya kumsema na kumkataa.

nadhani tusitake kila kiongozi ateuliwe kwa matakwa yetu sisi,ndio maana tumepewa nafasi ya kuchaguwa wabunge lakini baada ya mwezi tunawashushia lawama hao tulio wachaguwa,ikimaanisha chaguo letu halikuwa sahihi,je juu ya hilo nani wa kumlaumu mwenzake? maana Mh Raisi tupo wa kumlaumu,vipi juu ya hao tuwachaguao sisi wenyewe?

unaonaje kama aliyemteua naye angekuwa mkristo? Pangekuwa patamu ee?
 
Back
Top Bottom