Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,777
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Jacobs Mwambegele, amepinga madai kuwa wananchi na vyama vya siasa hawana imani na tume hiyo, akisisitiza kuwa wadau wote muhimu wanashirikishwa kikamilifu katika maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Akijibu swali la mwandishi aliyemuuliza kuhusu madai kuwa vyama vya upinzani vimepoteza imani kwa INEC na namna wanavyojipanga kurejesha uaminifu huo, Mwambegele amesema hoja hiyo haina msingi.
“Sikubali kabisa kwamba wananchi wala vyama vya siasa hawana imani na Tume. Hapa tunashirikisha wadau, wananchi na vyombo vya habari. Tarehe 27 Julai tulianza na vyama vya siasa isipokuwa chama kimoja, na kila mchangiaji alianza kwa kushukuru kazi inayofanywa na Tume,” amesema Mwambegele.
Ameongeza kuwa amekutana na viongozi wa vyama hivyo na wamekubali kazi ya Tume, ingawa anakiri kuwa wapo wanaoweza kuonesha kutoridhika na baadhi ya mambo.
“Kuchukua idadi hiyo ndogo na kuonesha kana kwamba Tume haikubaliki si kweli. Yawezekana wanaosema hivyo ni kwa kutoelewa Sheria au Kanuni, au kutofanya tafiti,” amesisitiza.
Kauli hiyo ameitoa leo Agosti 2 katika Mkutano wa Kitaifa wa INEC na waandishi wa habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unaofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Chanzo Bongo FM