Jifunzeni kufanya siasa za kistaraabu na kutatua matatizo yenu bila kusingizia watu wengine. Viongozi wa CHADEMA Mkoa wa Singida nimefanya nao kazi kwa muda mrefu na tulijenga urafiki, sio uadui.
Pamoja na kwamba tupo vyama tofauti kwa sasa, urafiki na undugu wetu haujaisha. Kwa hiyo tunaendelea kuwasiliana na kukutana inapobidi. Nilipokuwa Singida tulikutana na Shaban Limu, tukazungumza kama kawaida na kisha tukaenda kuwasalimia ndugu zetu waliopo gereza la Singida.
Nikutaarifu pia kwamba naendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa na Mhe. Mnyika katika kushughulikia tatizo la vijana wetu waliopo Singida na tunaendelea kuwasiliana kwa jambo hili. Bado nina marafiki wa kutosha makao makuu ya CHADEMA na tunazungumza na kubadilisha mawazo.
Tofauti zetu za kimsingi katika mambo ya kimtazamo, kiitikadi na kifalsafa hazina uhusiano kabisa na ubinafsi wetu kama binadamu. Siasa sio uadui, ni tofauti za kimtazamo, kiitikadi na kifalsafa.